Spurs yasaka kumaliza uteja kwa Man United
Saturday, 15 January 2011 09:12
LONDON,England
WAKATI Ryan Giggs na Paul Scholes walipotoka nje ya uwanja kwa kujikongoja baada ya kipigo cha mabao 3-1 pale White Hart Lane mwaka 2001 ingekuwa vigumu kuamini kwamba wawili hao wangekuwa wakiendelea kuichezea Manchester United kwa miaka 10 mingine.
Wanaweza wasiamini kuwa Spurs wameshindwa kuwafunga tena katika mara 19 walizokutana sasa watakakuwa wakijaribu kufanya hivyo katika muogo huu.
Hiyo ndio rekodi iliyokuwa nayo timu hiyo ya London dhidi ya klabu wanayokutana nayo Jumapili nyumbani hicho ndicho kitu wanachotakiwa kukibadilisha kama kweli wamezamilia kuingia kwenye nne bora na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
United inaongoza ligi kwa pointi 44 katika michezo 20, pointi mbili zaidi kwa Manchester City iliyocheza mechi mbili zaidi.
Arsenal ya tatu na pointi 40, Spurs ya nne na pointi 36, huku mabingwa watetezi Chelsea wamebaki nafasi ya tano kwa pointi 35, zote zikiwa zinacheza mechi 21.
An emotional appearance against his old club by David Beckham, who missed the 2001 fixture, will not now happen as the former England captainís loan deal with Spurs looks ever-more likely to be more of an extended training session.
Scholes atakuwa nje ya uwanja akishudia mchezo huo akiwa bado anasubuliwa na matatizo ya nyonga yaliyompata tangu mwezi Novemba, lakini Giggs anauwezo kuwepo uwanjani.
Pia, Wayne Rooney na Nemanja Vidic watashuka dimbani ili kuimalisha kikosi hicho kilichokuwa kinayumba katika wiki za hivi karibuni.
Spurs wanategemea kasi yao walioanza nayo msimu huu itawasaidia kurudia kile walichokifanya miaka 10 iliyopita.
Wamepoteza mechi moja tu nyumbani dhidi ya Wigan Athletic, huku United ikiwa imepata sare saba na kushinda mechi mbili ugenini.
Liverpool imeingia kwenye rekodi mbaya ya kufungwa mechi nane, sare mbili na kushinda moja kati ya mechi 11 walizocheza pamoja na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Blackpool, Jumatano.
Matunda ya Kenny Dalglish bado hayajaanza kuonekana baada ya kuanza kazi kwa kufungwa kwenye Kombe la FA palet Old Trafford, lakini anaweza kujirekebisha katika mchezo wake wa kwanza nyumbani dhidi ya mahasimu wao Everton.
Liverpool, iliyomtimua Roy Hodgson Jumamosi iliyopita kwa sasa inashika nafasi ya 13, ikiwa na pointi 25 nne zaidi kwa timu zilizokuwa kwenye janga la kushuka daraja.
Everton ipo juu yao kwa nafasi moja kwa tofauti ya mabao ya kushindi hivyo kuifanya mechi hiyo kuwa wazi zaidi kwa mahasimu hao wa jiji la Liverpool.
Liverpool itacheza bila ya Steven Gerrard, aliyefungiwa kutokana na kadi nyekundu aliyopata dhidi ya United.
Chelsea pia watakuwa na ndoto ya kurudi kwenye kasi yao ya mwanzo wa msimu baada ya kuichakaza Ipswich Town 7-0, watakapokuwa wenyeji wa Blackburn Rovers leo.
Mabao mawili na kiwango cha juu alichokionyesha Daniel Sturridge inaweza kumsaidia kuendelea kuwawake wakongwe Didier Drogba na Nicolas Anelka benchi kutokana na kushuka kwa viwango vyao hivi karibuni.
Arsenal, ilichapwa 1-0 na Ipswich kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Ligi Jumatano iliyopita, leo wanashuka dimbani kuikabili West Ham United.