Dogo Janja aipua nyingine mpya
na Dina Ismail
MSANII wa hip hop nchini kutoka kundi la Tip Top Connection, Abdulaziz Chende, maarufu kama ‘Dogo Janja, amekamilisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘I get Money'.
Meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale, alisema jijini Dar es Salaam juzi kuwa, wimbo huo amemshirikisha Godzilla na wakati wowote utaanza kurushwa hewani.
Alisema, pamoja na ‘singo' hiyo, msanii huyo yupo katika hatua za mwisho katika kukamilisha kurekodi albamu yake ya kwanza ambayo itaingia sokoni hivi karibuni.
"Unajua Dogo Janja tayari ameshaanza masomo yake pale Makongo Sekondari, hivyo tunafanya haraka kuhakikisha anamalizia albamu kabla masomo hayajachanganya ili aweze kutulia na mambo ya kitabu," alisema Tale.
Dogo Janja, msanii mwenye umri mdogo kuliko wote kati ya wasanii waotamba sasa, bado singo yake mpya ‘Anajua' aliyowashirikisha wakali kutoka Tip Top Connection Madee na Tundaman inaendelea kufanya vema.