Michepuko kushika kasi, nani wa kufanya mabadiliko? jibu ni wewe.

Kwa mtazamo wako, ni jinsia ipi inaongoza kwa kuchepuka? usipendelee tafadhali.

  • wanaume

    Votes: 0 0.0%
  • wanawake

    Votes: 2 100.0%

  • Total voters
    2

MWANASIASA HURU

Senior Member
Oct 4, 2012
180
240
habari zenu wadau,

naamini wengi wenu ni wazima na buheri wa afya kama ukiweza kufika kusoma mada hii.


niende kwenye mada tajwa.

Kumekua na wimbi kubwa la wanandoa wengi kutoka nje ya ndoa zao na kufuata penzi kwingineko (kuchepuka).
Tabia hii imeshamiri kwa siku za hivi karibuni mpaka kwa watu wengine wanaona ni jambo la kawaida kufanya hivyo. Dini nyingi zinapinga tabia/vitando hivi ila wengi hata wanaoamini wanaonekana kujitoa ufahamu na kuendelea kuchepuka.

Ndoa nyingi zinavunjika, watu wanapata maradhi ya kujitafutia kupitia michepuko yao, watu wanaumizwa mioyo, watoto wa familia wanateseka kwa kupata huduma duni kisa michepuko, uchumi wa familia unadorora kwa baba kuchepuka, wake wanakosa kuheshimu waume zao kisa kapata mchepuko wenye kiburi cha pesa, baadhi ya kina dada wanaacha kutafuta ndoa zao kisa kuna mume wa mwenzie anamchepukia na mambo kedekede, hakuna amani ndani ya ndoa, kisa MICHEPUKO.

Kwa wanaume nadhani wanaongoza kama utafiti ungefanywa, na wakifumaniwa wanaona kwao ni jambo la kawaida ila akifumaniwa mwanamke, panaweza kuchimbika, wanawake wengine hupoteza maisha kwenye fumanizi. Ni kweli mke anauma sana, sana tena sana kama nijuavyo maana hata kwa wale wakristo, biblia imeandika katika methali. ila mume pia anauma jamani, tuwaonee huruma hawa wake zetu, mioyo yao ni ya nyama pia.

Chanzo cha tatizo huwa ni wengi wetu kushindwa kutimiza majukumu yetu ya ndani na ya nje. namaanisha majukumu yote ikiwemo kuridhishana na kutoa huduma zote au kwa kadiri iwezekanavyo muhimu kumuweka mke au mume mahali pa kujisikia ana mme au ana mke kwa mke na mme.

Mwanaume akiulizwa kwanini anachepuka, wengi hawana majibu yenye mantiki, wengi wao huvutwa na rangi, umbile, sura, mng'ao, na vingine vidogo vidogo. Wengine ni ulevi na mob saikoloji ndo inawaendesha. ila kama kila mwanaume angemjali mkewe na kumlisha vizuri na kumthamini na kumpa mahitaji muhimu ikiwemo kumnunulia pamba za kumtosha, kumpa hela ya saluni, kutoa mahitaji madogo madogo ya nyumbani na kumpa muda wa kukaa nae kusikiliza hisia zake ama kushare nae idea mbalimbali, kila mmoja angeona mke wake ni mzuri na wazo la kuchepuka lisingekuwepo.

Wanawake wengi hawana makuu, wanaitaji muda wako uwe nae, umsifie kila anapojaribu kufanya jambo, hata kama si kubwa, akivaa mwambie wife umependeza, ukiamka msalimie kwa upendo, mwambie unampenda kila saa na umaanishe, kabla hamjalala tumia dakika chache kuongea nae kwa sauti ya mahaba flani mwambie 'mke wangu nakupenda' mweleze thamani yake kwako, asubui kabla ya kwenda kazini muage kwa kumbusu na kumwachia tabasamu tamu, mchana mpigie simu walao mara mbili mwulize anaendeleaje awe nyumbani ama ni ofisini haijalishi. siku moja moja mletee kazawadi hata kama ni kadogo kisha umpe wakati akishakupokea, mwambie umemmisi mchana wote. na mwngine mengi kama utakavyoweza kujiongeza kutokana na hali yenu ya kimaisha, ukifanya hivi hata kama alikua mzembe ataanza kujirekebisha, na utamuona mkeo ni mzuri kuliko yule wa ofisini kwako na kamwe mkeo hatakumbuka kuchepuka believe me. unless otherwise.

Kwa Mwanamke, wengi wao watasema hawaridhiki, ila wengi wamekosa care tu, wengine tamaa ya pesa, wengine wanafuata uzuri wa mwanaume which is nonsense na wengine wanashindwa tu kukwepa viunzi wanavyowekewa na wataalamu wa kuchepuka wasio na aibu, wala uchungu wa pesa atakazotumia, wala muda watakaopoteza. But kwa mwanamke siriaz simama na uitetee ndoa yako mwenyewe. wakati mwingine unahitaji kupambana na mabadiliko ya kimaisha, pambana na tabia yako pia, kama huwenzi kusifia mumeo jifunze, ukiona wanaume wengine wanpendeza tafuta namna nae awe hivyo, jipendekeze kwa mumeo, mwandalie vitu muhimu kabla ya muda kisha mwambie, mfano maji ya kuoga, chai kabla ya kwenda kazini n.k.
jipendezeshe pia si kila wakati wewe ni mchafu, hata kama ni mama wanyumbani na unauza kagenge, chukua muda wa kujiweka nadhifu mumeo akija avutiwe nawe, hii inaitwa courtship, tunaitaji kufanya kila siku.

wote wake kwa waume tujenge misingi ya imani, tuwe wa kwanza kutatua tatizo likitokea, ukiona unataka kuchepuka uwe mume au mke, jiulize unakosa nini na unafuata nini na utafanyaje ili mkeo au mumeo awe kama hicho unachotaka kukifuata. tafuta suluisho la moja kwa moja na uishi kwa amani. wanaume wengine wana wake wazuri kuliko michepuko yao ila tu wameshindwa kuwaweka wake zao waonekane nadhifu na wenye mvuto kwa kuwahudumia.

huu ni wakati wa mabadiliko, wanaume tubadilike, wanawake pia tufanye majukumu yetu tuache maisha ya kwenye muvie yenye stress, see your wife as a Queen and your husband as a King to women and men respectively.

nawasilisha
 
Weee acha kabisa mvhepuko ni mtamu tho mashariti mengi kama mikopo ya nmb
"Hakika mchepuko ni mtamu". Haya ni mawazo nilipata kusikia toka kwa mtu mzima kabisa. Na anajisifu anavyotumia mda wake wa mwisho wa wiki na mchepuko wake.
Watu wenye fikra kama hizo ni wapumbavu tu, hata bible imeainisha wazi kabisa...!
 
dunia imeharibika sana mkuu lakini isiwe sababu ya kuchepuka kama fasheni ,,,,,,,mchepuko una hasara kubwa kuliko faida zake
 
Mimi nitatoa yangu ya moyoni baadaye kidogo, kuchangia mambo ya mchepuko asubuh asubuh ni mkosi tosha nami nataka nikatafute hela kwanza.
 
Kuchepuka unapiga game as if hautapiga tena.Romance ya nguvu yaani raha sana
 
Back
Top Bottom