Michael Jackson special thread....

el nino

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
4,712
5,033
Tukutane hapa mashabiki wa Mfalme wa Pop na mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi duniani kwa mujibu Guiness book of records kwaajili ya kushare habari zake, picha, historia na zaidi ya yote zawadi ya muziki wake aliotuachia hapa Duniani.

Historia yake.

Alizaliwa mwaka 1958 mwezi wa 8 huko indiana USA, mtoto wa 8 katika familia iliyobarikiwa vipaji vikubwa kupeleka kuundwa kwa kundi maarufu la Jackson 5, ambapo yeye alijiunga na kaka zake na kuanza shughuli za muziki miaka ya 1960's akiwa na umri mdogo sana ila kipaji chake kilipelekea kuushangaza ulimwengu kwa kuwa kinara wa kundi la Jackson 5 lililopata mafanikio makubwa sana Duniani.

Michael kuanza shughuli za muziki akiwa mdogo kulipekea yeye kuwa Supastaa mkubwa sana duniani akiwa mdogo kitu ambacho kiliathiri sana maisha yake ya baadae ambapo alikuja kudai umaarufu ulifanya aisienjoy kabisa utoto wake maana alikuwa hawezi kucheza kama watoto wengine hivyo kusihi maisha ya kipweke hivyo kutopata raha yeyote ya utoto kama watoto wengine.

Kingine alikuwa chini ya ulinzi mkali wa baba yake ( Joseph Jackson) ambaye alikuwa hataki utani kabisa.

Itaendelea
pBhH0Cz6AeOO.jpg
pBgrmTEcAO7h.jpg



Michael alipata mafanikio makubwa sana akiwa na Jackson 5, aliizunguka dunia kwa kufanya tour kibao huku wakisumbua kwa vibao vikali kama 'ABC', 'Can you feel it' 'shake your body' bila kusahau 'ill be there', kusema za ukweli Jackson 5 ilikuwa haikamatiki miaka ya 1970's.

Akiwa ndani ya Jackson 5 na kaka zake Michael Jackson alikuwa akitoa album zake binafsi ambazo zilifanya vizuri sana, ukiacha zote album yake ya mwaka 1979 ijulikanayo kama 'off the wall' ilitikisa dunia kwa vibao vikali na vya kusuuza mioyo, unaweza kusema hii album ilibadilisha maisha yake maana hii ndiyo album yake ya kwanza kuwa produced na mtaaalam "Quincy Jones" ambaye alisimamia show nzima kwa kuhakikisha vibao vikali kama 'Dont stop till you get enough' na 'Rock with you' vinasumbua kumbi zote kubwa za disco na chati kubwa za muziki marekani na duniani kwa ujumla.

Michael Jackson hakuwa mtu wa kuridhika na mafanikio hata kidogo, baada ya kutengeneza album ya 'off the wall' wengi walidhani amefikia climax au kilele cha mafanikio na uwezo wake, kumbe Michael ndio kwanza alikuwa anaanza kazi, Jackson 5 na mafanikio yake binafsi havikumridhisha hata kidogo, alikuwa anaitaka aiteke dunia ya muziki aiweke kiganjani mwake zaidi ya Elvis presley, alitaka akitumbuiza awakamate watu zaidi ya James brown na perfomers wengine wakali, hivyo basi alidhamiria kabisa kuwa atakuja na album kali sana kiasi kwamba atazishika jamii zote sio 'wazungu' au watu weusi peke yao!

Ifahamike kabisa mwaka 1979 Michael Jackson aliona kama thamani ya kipaji chake inachukuliwa poa hasa na wazungu, maana alitoswa na majarida mengi alipoyataka yamuweke kwenye cover story likiwemo jarida kubwa la Rolling stone, hili lilimuumiza sana michael akiwa kijana mdogo na mtu mweusi aliyeamini ana kipaji kikubwa lakini hakithaminiwi kwa kupewa angalau tuzo kubwa licha ya mauzo yake makubwa



Thriller era... ..(1982)

Hiki ndicho kipindi historia ya muziki wa dunia ilibadilishwa kabisa, kabla ya hiki kipindi, wasanii weusi walikuwa hawachezwi sana kwenye radio na tv ambazo zilikuwa zinaonyesha content za wazungu kama MTV!

Ukiachana na hayo pia ilikuwa ngumu kabisa majarida makubwa ya burudani na sanaa kwa ujumla kumuweka mtu mweusi kwenye front page, walikuwa wanadai mtu mweusi hauzi, hivyo basi ukiona myu mweusi yupo kwenye cover la jarida kubwa huko marekani ujue kuwa kuna mtu mweusi alitokea ambaye ilishindikana kuzuia kipaji chake na umaarufu wake katika jamii zote za watu weusi huko marekani hivyo kupelekea kubadilisha historia kabisa katika uwanja mzima wa burudani Us na duniani kwa ujumla.

Katika mchakato wa kuitengeneza album ya thriller, michael aliingia chimbo akiwa na dhamira ya kuwaonyesha adabu wote waliomdharau, Michael alikuwa perfectionist maana baada ya kurekodi karibia album nzima alitokwa na machozi baada ya kutoridhishwa na vibao hivyo, ikapelekea Michael na Quincy jones kuvifanyia remix vibao vyote vya kwenye album ya thriller ili kuhakikisha kitu kitakachotoka kiwe ambacho hakijawahi kushuhudiwa tokea kuumbwa kwa misinfi ya duni..

Itaendelea
 
Earth song.
Beat it
Give in to me.
Who is it?
Liberian gal.
R u not alone.
Hizi ni ngoma sichoki kuziskiliza toka kitambo sana hadi kesho kutwa nazifeel sana
 
Earth song.
Beat it
Give in to me.
Who is it?
Liberian gal.
R u not alone.
Hizi ni ngoma sichoki kuziskiliza toka kitambo sana hadi kesho kutwa nazifeel sana
hiyo give it to me ..acha kabisaaaa"""
 
ghost""

smooth criminal

who is t

Liberian girl

stranger in the Moscow

scream

man in the Miroor

cry

human nature

health song""

who is bad

dangerous

blood in the dancing floor

dirt Diana

I'll be there

you will be there

heal the word

you rock my world

jam

they dont care about us ""

acha kabisaaa huyo mtu ..hana mfano
 
Jamaa huyu alikua kichwa sana

Akipiga matamasha ya kutisha watu wanalia na kuanguka chalii...wadada wanadata...he was truly gifted...

Kwanza anaandaa show ya ukweli yaani haiibi mtu kwa kubabaisha....

Ur not alone akiimba wadada wanaanguka dah
 
Jamaa huyu alikua kichwa sana

Akipiga matamasha ya kutisha watu wanalia na kuanguka chalii...wadada wanadata...he was truly gifted...

Kwanza anaandaa show ya ukweli yaani haiibi mtu kwa kubabaisha....

Ur not alone akiimba wadada wanaanguka dah
Kuna show moja bab kubwa aliipiga Munich Germany cjui ilikuwa mwaka gan vile daaah!!! eeh bhana eeeh
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote


Mungu Humpa Ampendaye
Mungu Hana Choyo
Mungu Hakupi Vyote
 
Ni ukweli usiopingika,MJ alikuwa much talented.Nyimbo zake ziligusa nyanja nyingi!Kuna kitu kinaitwa keep the faith,ukisikiliza huu wimbo walahi kama unakumbana na magumu kwa wakati huo,hakika unapata matumaini!Huyu King nammiss sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom