Miamala inapogeuka kuwa kero

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,061
24,486
Kutokana na kukua kwa teknolojia kumepelekea kurahisishwa kwa mambo mengi na hasa kwenye sekta ya mawasiliano na uchukuzi, licha ya hayo makampuni mengi na benki hutumia teknolojia hasa kwenye suala la kununua bidhaa, malipo ya bili, kutuma na kupokea fedha, njia hii imekuwa msaada kwa wengi japo ina changamoto zake.

Wakati mwingine hizi huduma za kufanya miamala zinaweza kugeuka na kuwa kero hata mtu ukachukia kabisa na kutamani kuachana na hiyo miamala. Kwa upande wangu kero inakuwa pale ambapo unatuma fedha au unahamisha fedha na kisha fedha kuhama kwenye akaunti bila kufika sehemu husika kwa wakati au wakati mwingine kurudi kwenye akaunti lakini kwa kuchelewa.

Hili limenitokea mara kadhaa kwamba nilikuwa ninahamisha fedha kwa njia ya sim banking kwenda kwenye namba ya simu lakini hela haikufika kwenye ile namba na ilikuwa ni dharura. Nilipowapigia simu wahusika ni majibu rahisi tu walitoa kwamba hela imenasa kwenye mtandao na haitaweza kwenda tena kwenye namba husika badala yake itarudishwa baada ya masaa24.

Jambo ambalo lilisababisha usumbufu. Hivi kweli muamala niliufanya kwa sababu ya shida kwa wakati huo sasa wanaposema hela imekwama na mda wa kuipata ni baada ya masaa24, wanamaanisha nini? Je kama sina fedha nyingine kwa wakati huo au nimehamisha hela yote kwenye akaunti ndio ikakwama kwa uzembe hayo masaa24 ntasaidika vipi? Na ni kwanini hela ikikwama hawatoi taarifa mpaka mteja apige simu? Huduma wanaanzisha wao sisi ndio wateja, iweje umnyanyase mteja na fedha zake. Haya mabenki NMB, CRDB na benk nyingine hizi huduma zenu za simu huwa wakati mwingine mnaboa wateja wenu.
 
Mkuu yaan kama umeniona mm Leo hii mpaka nmevurugana na customer manager Pesa nilitoa kutoka bank kuja mpesa tareh 23/07 lakn mpaka sasa wanazungusha tu mara sijui mtandao ulisumbua yaan manina hawa jamaa wezi hatar
 
Daah..yaani mkuu hizi huduma zao zinakuwa za kichoko sana!!
Eti wanajibu ni taratibu za kazi..
Ni bora kukawa hata na sheria ya kuwakaba hawa jamaa pale inapotokea delay isiyokuwa na kichwa wala miguu na kumsababishia mteja usumbufu!
Wao kwa kuwa wamezoea kukaa na maburungutu ya fedha hawajui wengine huwa wanapataje hizo fedha..
Mimi nliwauliza hivi angekuwa yeye ndio mteja kisha ikamtokea hivo na hana chochote angefanyaje..
Hakunipa jibu...
 
Kutokana na kukua kwa teknolojia kumepelekea kurahisishwa kwa mambo mengi na hasa kwenye sekta ya mawasiliano na uchukuzi, licha ya hayo makampuni mengi na benki hutumia teknolojia hasa kwenye suala la kununua bidhaa, malipo ya bili, kutuma na kupokea fedha, njia hii imekuwa msaada kwa wengi japo ina changamoto zake.

Wakati mwingine hizi huduma za kufanya miamala zinaweza kugeuka na kuwa kero hata mtu ukachukia kabisa na kutamani kuachana na hiyo miamala. Kwa upande wangu kero inakuwa pale ambapo unatuma fedha au unahamisha fedha na kisha fedha kuhama kwenye akaunti bila kufika sehemu husika kwa wakati au wakati mwingine kurudi kwenye akaunti lakini kwa kuchelewa.

Hili limenitokea mara kadhaa kwamba nilikuwa ninahamisha fedha kwa njia ya sim banking kwenda kwenye namba ya simu lakini hela haikufika kwenye ile namba na ilikuwa ni dharura. Nilipowapigia simu wahusika ni majibu rahisi tu walitoa kwamba hela imenasa kwenye mtandao na haitaweza kwenda tena kwenye namba husika badala yake itarudishwa baada ya masaa24.

Jambo ambalo lilisababisha usumbufu. Hivi kweli muamala niliufanya kwa sababu ya shida kwa wakati huo sasa wanaposema hela imekwama na mda wa kuipata ni baada ya masaa24, wanamaanisha nini? Je kama sina fedha nyingine kwa wakati huo au nimehamisha hela yote kwenye akaunti ndio ikakwama kwa uzembe hayo masaa24 ntasaidika vipi? Na ni kwanini hela ikikwama hawatoi taarifa mpaka mteja apige simu? Huduma wanaanzisha wao sisi ndio wateja, iweje umnyanyase mteja na fedha zake. Haya mabenki NMB, CRDB na benk nyingine hizi huduma zenu za simu huwa wakati mwingine mnaboa wateja wenu.
Dah yaani nmb ndo inachosha mno hakuna sehemu moja ya kuweza peleka tatizo na likatatuliwa!yaaani miamala ikikwama tegemea mwezi!ukipiga simu kama umepata tatizo mida ya usiku ni shida mno kupata kituo cha huduma kwa wateja!jamani nmb bank tuelimishane tupeleke wapi kero zetu?huduma ni mbovu na sehemu ya kupeleka malalamiko hakuna ni shida mnooo!tuoneane huruma nmb bank!mteja ni mfalme tusikilizane basiiii
 
Wanaboa kweli yani...
Pesa yako unanyanyaswa...
 
Back
Top Bottom