Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,180
- 24,798
Kutokana na kukua kwa teknolojia kumepelekea kurahisishwa kwa mambo mengi na hasa kwenye sekta ya mawasiliano na uchukuzi, licha ya hayo makampuni mengi na benki hutumia teknolojia hasa kwenye suala la kununua bidhaa, malipo ya bili, kutuma na kupokea fedha, njia hii imekuwa msaada kwa wengi japo ina changamoto zake.
Wakati mwingine hizi huduma za kufanya miamala zinaweza kugeuka na kuwa kero hata mtu ukachukia kabisa na kutamani kuachana na hiyo miamala. Kwa upande wangu kero inakuwa pale ambapo unatuma fedha au unahamisha fedha na kisha fedha kuhama kwenye akaunti bila kufika sehemu husika kwa wakati au wakati mwingine kurudi kwenye akaunti lakini kwa kuchelewa.
Hili limenitokea mara kadhaa kwamba nilikuwa ninahamisha fedha kwa njia ya sim banking kwenda kwenye namba ya simu lakini hela haikufika kwenye ile namba na ilikuwa ni dharura. Nilipowapigia simu wahusika ni majibu rahisi tu walitoa kwamba hela imenasa kwenye mtandao na haitaweza kwenda tena kwenye namba husika badala yake itarudishwa baada ya masaa24.
Jambo ambalo lilisababisha usumbufu. Hivi kweli muamala niliufanya kwa sababu ya shida kwa wakati huo sasa wanaposema hela imekwama na mda wa kuipata ni baada ya masaa24, wanamaanisha nini? Je kama sina fedha nyingine kwa wakati huo au nimehamisha hela yote kwenye akaunti ndio ikakwama kwa uzembe hayo masaa24 ntasaidika vipi? Na ni kwanini hela ikikwama hawatoi taarifa mpaka mteja apige simu? Huduma wanaanzisha wao sisi ndio wateja, iweje umnyanyase mteja na fedha zake. Haya mabenki NMB, CRDB na benk nyingine hizi huduma zenu za simu huwa wakati mwingine mnaboa wateja wenu.