Mtemi02
JF-Expert Member
- May 1, 2020
- 320
- 221
Leo nikiwa mmoja kati ya abiria watatu kwenye bajaji abiria wenzangu wawili ambao inaonekana wanafahamiana na wapo route moja wamenikuta ndani ya bajaji wanaonekana kuvaa nadhifu na maongezi yao yanaonesha hawa ni watumishi wa umma. Na dereva wa bajaji nae ni mtumishi tena alijitambulisha kuwa ni mwalimu.
Abiria wenzangu wao ndio waliingia huku wakiwa na stori za kulaumu mshahara sijui nyongeza ndogo, mara hakuna madaraja nk. Dereva akasema "Yani nyie acheni Mimi mwaka wa sita huu tangu niajiriwe sijapanda daraja, tangu nimeajiriwa Aprili mwaka 2014 niko D hadi leo. Alafu Mkuu wa Shule anataka nifundishe vipindi vya jioni, siwezi kufanya huo ujinga, mimi ikifika saa nane nawahi bajaji yangu"
Mmoja wa abiria akadakia "mwanangu hata Mimi tumeajiriwa mwaka mmoja na kimsingi mwaka kesho tungekuwa F. Jamaa sio fair hata kidogo, ukijifanya uko bize na kazi lazima ufe masikini". Huyu jamaa hadi nashuka kwenye bajaji sikujua anafanya kazi gani pamoja na kuwa hawakusema mishahara yao ila wanasema tu D, E na F.
Yule abiria mwingine akasema yeye alipanda E mwaka jana ila analalamika pia. Waliongea mambo mengi sana mmoja anasema akipata nafasi ya kusimamia uchaguzi anajua atakachofanya. Nilistuka, bahati mbaya siwafahamu maana kuvuruga uchaguzi sio jambo jema.
Nikapata wasiwasi kama hawa jamaa wanahudumia watu wengi kama vile walimu, Watendaji kata, Maafisa mifugo nk nahisi watakuwa wanalipua tu huko kazini na hawatilii mkazo kazi yao. Maana wameongea mambo mengi tena kwa hasira kana kwamba wanalipa kisasi kwa wasiohusika.
Wito wangu mnaohusika fuatilieni mwenendo wa watumishi wenu maana inawezekana kuna makosa yanafanywa makusudi huko alafu wanaoteseka ni wengine.
Mungu Ibariki Tanzania - MITz