Miaka saba jela kwa kujeruhi mwanawe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,054
2,000
MAHAKAMA ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, imemhukumu Mohammed Masud (30), mkazi wa Kijiji cha Mnazi Mmoja wilayani humo kutumikia adhabu ya miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kujemruhi mtoto wake.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Honorius Kando, baada ya mshitakiwa kukiri kufanya kosa hilo.

Hakimu Kando alisema mahakama yake imechukua uamuzi wa kumhukumu kifungo hicho baada ya mtuhumiwa kukiri kufanya kosa kwa kumchoma moto aliouwasha kwa kutumia kuni katika miguu yake na kumsababishia ulemavu wa muda.

Alisema kitendo kilichofanywa na mzazi huyo ni ukatili uliopindukia, hivyo adhabu hiyo ni fundisho kwake na watu wengine ambao wamekuwa na tabia za kufanya vitendo vya aina hiyo.

Awali, akimsomea mashtaka hayo ya jinai namba 163/2020, Mwendesha Mashtaka ambaye pia ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Stephen Msongaleli, alidai kuwa, katika tukio hilo, mtuhumiwa huyo alimchoma moto na kumsababishia maumivu makali na majeraha katika vikanyagio vya mguu mtoto wake mwenye umri wa miaka saba(jina tunalihifadhi).

Inspekta Msongaleli alidai kuwa hilo ni kosa la kwanza kutekelezwa na mtuhumiwa huyo, lakini aliiomba mahakama kumpatia adhabu kali ili liwe fundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa na tabia za kutesa watoto katika jamii.

Alidai taarifa zilizotolewa na maofisa tabibu wa hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru anakotibiwa majeruhi huyo, zinabainisha kuwa hadi sasa, mtoto huyo hawezi kutembea kwa kutumia miguu yake jambo ambalo halikubaliki.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Rehema Nyanda, alidai mahakamani kuwa mtoto huyo aligundulika kufanyiwa ukatili huo Machi 15 mwaka huu baada ya majirani kutoa taarifa za kupotea kwa mtoto huyo.
Nyanza aliiomba mahakama hiyo kutoa maelekezo ya mtoto huyo kupelekwa kwa mama yake mzazi mkoani Lindi ili kuepuka vitendo hivyo vya ukatili.

Akijitetea kabla ya hukumu hiyo, Masud aliomba mahakama hiyo kumwachia huru kwa madai kuwa katika tukio hilo alikuwa anamwadhibu mtoto wake baada ya kutuhumiwa na majirani zake kuwa amekuwa na tabia za udokozi.

NIPASHE
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
12,895
2,000
Hao Ni MABEBERU Wanaingilia Mambo Ya Ndani Ya Familia Ya Mtu Mwingine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom