Miaka 50 ya uhuru ni ubadhirifu mtupu

Timor

Member
Feb 4, 2009
48
32
Nimetembelea mabanda mbali mbali tangu Wizara na mashirika mbali mbali wameanza kuonyesha tulikofikia miaka 50 ya Uhuru TANZANIA BARA. Nimeongea na watu mbali mbali, waonyeshaji na watendaji mbali mbali wa serikali na kujionea mwenyewe yale yanayoendelea.

Ukweli ni uharibifu na ubadhirifu mkubwa wa fedha na mali za serikali.Mathalani Wizara mmoja iko Dodoma inafanya maonesho ya siku tano Dar, Washiriki wote @ anapewa pair ya sare ya kila siku hadi dreva,kisha anapewa posho @80,000/=,Halafu wanapewa lunch kila siku nk.Ukija kwenye gharama za kuandaa vipeperushi ni mara tatu ya bei ya kawaida acha publicity materials zingine na Impress mbali mbali.Lakini ukiangalia impact ya maonesho yenyewe ni almost hakuna! Sasa wizara zote,Gharama za magari na vyombo vingine nk.Kwa ujumla kiasi kikubwa sana cha fedha kinatumika kuandaa maonesho hayo! Nenda kila Wizara ,Taasisi, wakala wa serikali uone hayo mahesabu yalivyo kaa,Hapo hapo watoto wetu hapa hapa jijini wanakaa chini hawana madawadi,Hospitali hazina dawa.Maji mitaani hakuna-Umeme ndo mgogoro wa kupindukia nk nk.TUTAFIKA KWA JINSI HII???
 
Kwa nchi yetu ilivyo sasa na tabia ya kula bila kuwa na uoga,hii nayo ni project nyingine ya watu kutengeneza mamilioni. Watch out and see!
 
Uhuru hakika ungesherehekewa kwa hayo mafungu kupelekwa kwenye shule na hospitali halafu siku ya uhuru ingefanywa tathmini ya kilichofanyika kweli tungepiga hatua sherehe zingepambwa na taarifa ya kilichofanyika tuu!!
 
Tangu nimckie mr msoga kwenye hotuba yake juu ya miaka 50 ya uhuru,nikajioj on ma mind,kumbe we are on the semu boti
 
Back
Top Bottom