Miaka 50 ya uhuru mnamkumbuka Kigoma Ally Malima?

Watetezi wa Malima kwa Unafiki siwawezi hadi leo hamkubali kuwa kutumia namba kwenye mitihani ni utaratibu uliokuwepo kabla malima hajawa waziri? Kweli nyie vichwa panzi

Yaani hawa watu ni wa ajabu sana,wakishajazwa ujinga na mapunguani wenzao hawataki kufanya utafiti ili waijue kweli, wao watabaki kung'ang'ania upuuzi usio na msingi, suala hili namba/majina lilishafafanuliwa toka zamani kwa ushahidi ulio wazi kuwa matumizi ya namba badala ya majina yalianza kitambo kabla hata huyo marehemu MDINI malima hajawa waziri wa elimu!
Kusema kweli genge la watu hawa linakera sana, hawana hoja za maana za kujenga taifa bali kuwagawa wananchi kwa misingi ya imani. katika moja ya hotuba zake Kikwete alishawahi sema "kuna watu wanatamani nchi hii iwe ya kikristo na wengine wanatamani sana nchi hii iwe ya kiislam na akasema jambo hilo haliwezekani na mtu akijaribu kulazimisha itatokea vita ambayo mshindi hatopatikana", kwa hiyo wapumbavu wote wenye mawazo mgando kama hayo waache mara moja na tushirikiane katika kujenga taifa letu, tunajikita kwenye mambo yasiyo na msingi, tunatumia bongo na akili zetu kujadili mambo ya kijinga yasiyo na tija badala ya kujadili mambo ya maana na yenye manufaa kwa taifa letu na matokeo yake nchi ndogo na zilizokuwa na matatizo kama Rwanda n.k zinatupita kiuchumi kwa kuwa wamejua nini maana ya umoja na mshikamano bila kujali tofauti zao!
 
Allah akulipe kheri Prof, akusamehe madhambi yako, aku rehemu na akuingize peponi kwa Rehema zako.AAMIIN

Hapo kwenye red ndo pa kumuombea sana maana dhambi ya UDINI aliyoipanda bado yatutafuna mpaka sasa! kama kuwa muasisi wa udini ingekuwa sifa njema basi naye angeenziwa kwa kupewa nishani kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru!!
 

mjinga ni mjinga tu yani wewe unamuona malima ni mdini ungeona uchaguzi ulivyo fanyika huku Arusha wala usinge yazungumza hayo uliyo yaandika wacha ushabiki waingereza wana msemo unao sema [everybody is fundamental in his beleave]kwahiyo Malima alikuwa na haki ya kutetea dini yake kama alivyofanya DIKTETA NYERERE kulinda ukatoliki
 
well summarized! nadhani mleta mada atakua keshaelewa!

 
Simkumbuki, alikuwa nani vile? Na miongoni mwa Watzania milioni 40, anahusika vipi na miaka 50 ya uhuru ?
 

==================
Waislamu mpeni tuzo ya miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika!!!!
 
..mimi namuona Malima alikuwa ni opportunist.

..wakati wa Mwalimu Nyerere, Prof.Malima aliandika waraka mkali kwenda kwa Mwalimu akiwaita wasaliti wale wote waliokuwa wakipendekeza mabadiliko na marekebisho ya uchumi.

..ilipokuja awamu ya Mzee Ali Mwinyi, Prof.Malima akabadilka na kuwa kinara wa utekelezaji wa mabadiliko yaleyale aliyokuwa akiyapinga wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

..katika awamu ya Mzee Ali Mwinyi, Prof.Malima aliibuka tena na waraka ambao alikuwa akidai Waislamu wanadhulumiwa ktk kupata nafasi za kuendelea na masomo sekondari. kitu cha kusikitisha ni kwamba hakuwa amefanya utafiti juu ya suala hilo, na hata hakutoa mapendekezo yoyote yale ya kurekebisha kasoro zilizokuwepo ktk mfumo wetu wa elimu.
 

Alitoa mapendekezo ambayo yalitufanya waislam wengi kwenda sekondari kati ya mwaka 1987/1988 unlike many years

Kama kuna waislamu wamefaulu darasa la saba 1987/1988..ni kazi kubwa aliyofanya Malima, kuweka namba badala ya jina

Hata hivyo mfumo huu wa HAKI uliwaudhi sana jamii (ILIYOZOEA KUPENDELEWA ya Wakristo) Malima akawa adui wao akiwemo nyerere..hakushiriki hata mazishi yake

Mungu amuweke mahala pema
 
Topical,

..I really doubt it kama kweli Waislamu wanafaulu kutokana na hatua alizochukua Prof.Malima.

..hebu nenda Mkuranga kwenye jimbo lake la uchaguzi halafu uniambie sekta ya elimu ina hali gani.

..ninachokumbuka mimi ni kwamba Malima alianzisha mtindo wa double session na pia alifuta mtihani wa kidato cha pili.

..inawezekana double session iliongeza idadi ya wanafunzi wa Kiislamu wanaofaulu, lakini percentage wise mambo yako vilevile.

..hili tatizo ni KUBWA na VERY COMPLEX na linahitaji umakini zaidi ktk kulizungumzia na kulishughulikia kuliko alivyofanya Prof.Malima na serikali inavyoendelea kufanya sasa hivi.
 

Huwezi kuangalia mafanikio ya Maalim kwa jimbo la mkuranga..unaangalia kwa nchi nzima (HOLISTIC Approach)

Mtindo wa namba ndio uliowasaidia waislam specifically mwaka 1987/1988 ambayo matokeo ya mwaka huu (nenda wizarani) ni tofauti sana na miaka yote

Serikali kwa kutopenda haki wakaacha mfumo huo immediately alipofukuzwa kazi Malima

yes, matatizo yanaweza kuwa complex lakini hilo la upendeleo unaofanywa na maofisa wa wizara ni ONE of the major factor
 


una hakika Malima Sr alikuwa mbunge wa Mkuranga?
 
Marcus,

..Prof.Malima alikuwa mbunge wa Kisarawe.

..Adam Malima ambaye ni mtoto wa Prof ni mbunge wa Mkuranga.

..sasa kwa ajili ya discussion yetu hebu tujaribu kuona Prof alifanya nini kuboresha elimu jimboni[kisarawe] kwake alipotokea.

..manaake huko ndiko alikuwa na uwezo na ushawishi wa kuleta mabadiliko aliyokuwa akiyapigania ktk masuala ya elimu.


Topical,

..nambari za mtihani zilikuwepo kabla Malima hajaingia wizara ya elimu.

..sijui kwanini wasomi wazima na elimu zenu mnaamua kupotosha waziwazi.
 
Hivi wanaosema Malima alijenga Msikiti alijenga wapi, au alitenga chumba kwa ajili ya ibada na kama ni hivyo kwa nini waseme alijenga?
 
Mbona huku mashuleni wanafunzi wa kiislam bado wananyanyaswa kwa kuzuiliwa kuvaa hijab,fursa ya vipindi vya dini na sala ya Ijumaa bado ni kikwazo kikubwa,,mti wenye matunda daima hupigwa mawe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…