Miaka 50 ya ndoa

Miaka 50 ya ndoa

Mr. JF

Member
Joined
Dec 14, 2015
Posts
79
Reaction score
107
Habari za jumapili wana MMU,
Napenda kuuliza jambo moja kuhusiana na hii dhana ya hizi marriage anniversaries.
Lets say ulifunga ndoa miaka 50 iliyopita, lakini baada ya kufunga ndoa, mlikaa miaka 10 mkaachana, kila mtu akaendelea na maisha yake (possibly mume ukawa na mke mwingine au mke akawa na mume mwingine), baada ya miaka 15, ikatokea mkaamua kurudiana, mkaanza kuishi tena kama mume na mke, swali ni je, mtajitanabaisha kwamba mna miaka 25 ya ndoa while 15 mliitumia mkiwa mmetengana? Na mkiendelea kuishi hadi ikatimia miaka 50 tangu mmefunga ndoa, je mna uhalali wa kusema ndoa yenu ina miaka 50?? Nawasilisha!
 
Kwani ndoa ni nini?

Kuna mambo saba:
-mwoaji
-mwolewaji
-mwozeshaji
-mashahidi
-mahari
-tamko la kisheria kuhusu kuozeshwa kwa mwoaji na mwolewaji
-kufanya tendo kamili la ngono (procretive-in-type-sex) angalau mara moja mara baada ya tamko la kisheria kutolewa.

Kwa hiyo, umesahau tofauti kati ya kutengana bila kutalikiana na kutebgana kwa kutalikiana.
Bila talaka ndoa inakuwa hai...
Isipokuwa kwa wale wasiojaribiwa, mengine yoye yanakuwa ni majaribu...
Mchana mwema.
 
Hapo hakuna ndoa ya kuacha na kurudiana,yaani mnaachana mara kadhaa na kurudiana mara kadhaa
 
Hahahah..!! kiukweli mzee kazingua, haifiki 50
 
Nahisi kuna mtu unamuongea hapa![emoji1]......ila jua kwenye siasa kuna mengi!
 
Hivi second honeymoon itakuwa wapi,kwa mnaofahamu?
 
kuna vitu viwili hapo kwa mujibu wa mtoa mada kuna miaka 50 ya ndoa akimaanisha tarehe ya kufunga ndoa na la pili ni maisha ndani ya iyo ndoa inawezekana maisha ndani ya iyo ndoa yasitimie umri sawa wa iyo ndoa mana wenda yalikua yanakatishwa katishwa
 
Hiyo ni sherehe mahusisi kabisa kwani hakuna aliyeenda kuoa / kuolewa
inaitwa Silver Anniversary itafuata ya miaka 75 Diamond
siku hizi ninyi vijana wa kizee hamtaziweza hizi
 
Kwa mimi naefahamu nini maana ya ndoa nakataa(kwa imani yangu)hakuna ndoa za kihuni kama hizo,labda kama zikawa ndoa za wakuu wa wilaya au jadi.ndoa inakamilika pale wahusika wanapokuwa wana share yote kwa pamoja si'tofauti na hivyo kwa Wakristo ndoa ndivyo ilivyo ila siku hizi kuna ujanja ujanja mara mke kaondoka kwao mara karudi kwa mumewe alimradi imekuwa vurugu,ila kiimani ndoa iliyoamriwa ni ile mnakaa pamoja mnavumiliana hadi mmoja atakapotangulia unless imetokea kufumaniana uzinzi!
 
kuna vitu viwili hapo kwa mujibu wa mtoa mada kuna miaka 50 ya ndoa akimaanisha tarehe ya kufunga ndoa na la pili ni maisha ndani ya iyo ndoa inawezekana maisha ndani ya iyo ndoa yasitimie umri sawa wa iyo ndoa mana wenda yalikua yanakatishwa katishwa
You got it right
 
Back
Top Bottom