Ndugu zangu,
Katika kuadhimisha miaka kumi ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, CCM na miaka 20 ya Azimio la Arusha, Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikubali kufanya mahojiano ya kipekee na ya aina yake na Mhariri wa gazeti la Uhuru. Huo ulikuwa ni mwaka 1987.
Katika mahojiano yale, Mwalimu Nyerere, akiwa mwenyekiti wa CCM, hakusita kutamka bayana, kuwa Chama alichokuwa akikiongoza kilikuwa na kasoro na mapungufu mengi.
Mwalimu aliona kupungua kwa moyo wa kujitolea. Aliona dalili za kupungua kwa maadili ya uongozi. Mwalimu aliona mioyo ya kimamluki ilivyoanza kuingia na kuenea ndani ya CCM na nchi yetu. Hayati Mwalimu Nyerere alifikia kumtamkia mhariri yule wa gazeti, kuwa;
“ Tumewapa uongozi watu wasiofaa. Nadhani wengi ndani ya Chama tumeanza kuutambua ubovu huu. Hatua ya kwanza ya kutibu maradhi ni kuyatambua.” Alitamka Mwalimu.
Ndio, Mwalimu aliona mbali, hii leo viongozi wanaofanya matendo maovu na ya kimamluki ndani ya vyama vya siasa na nchi kwa ujumla ndio wale aliowatabiri Mwalimu Nyerere miaka 39 iliyopita.
Nimepata kukumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Na wanadamu hatupaswi kuwa vipofu wa historia yetu wenyewe.
Kuifumbia macho historia yako ni kujiandalia njia ya kutumbukia korongoni, kwa kujitakia. Tunapoadhimisha miaka 50 ya Azimio na miaka 40 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, tuna lazima ya kuipitia na kuitafakari historia yetu.
Kwa macho makavu na maangavu, tuangalie nyuma tulikota. Tuangalia tulipo sasa. Ndio, tufanye hivyo ili tuutafute mwelekeo mwema wa nchi yetu hata kwa miaka mingine hamsini ijayo.
Majuzi hapa nilipata kuhojiwa na mtangazaji wa Redio iitwayo Arusha One. Mtangazaji yule kijana alitaka kujua mtazamo wangu juu ya mwelekeo wa siasa.
Nilimwambia, kuwa kwa ilivyo sasa Chama Cha Mapinduzi ndicho kilicho na nguvu na ushawishi mkubwa kuliko vyama vingine vyote kwa pamoja. Maana, CCM inajivunia kuwa na dola. Na CCM haijaikamata dola kwa mabavu, bali kwa kura. Hivyo, nguvu ya umma. Kwamba vyama vya upinzani vina kila sababu ya kama CCM, navyo kuwekeza kwa watu.
Ni lazima vyama na zaidi viongozi wake waaminike kwa wananchi wengi ambao ndio wapiga kura. Hata kama kuna watakaonipinga, lakini, ni ukweli, kwa ilivyo sasa CCM bado ina mtaji mkubwa wa imani kwa wananchi wanyonge walio wengi. Na Serikali hii ya sasa ya John Magufuli, inakipa nafasi Chama Cha Mapinduzi kulirejea jukumu lake la kihistoria, la kuwa kimbiilio la Wanyonge.
Ingawa hivyo, tuna maswali mengi ya kujiuliza, moja kuu ni hili; Je, ni nchi ya namna gani tutayotaka kuijenga na hata kuvirithisha vizazi vijavyo? Kwa maneno mengine; ni jamii gani tunayotaka kuijenga?
Sisi wa ’ Kizazi Cha Azimio’ tulikuwa wadogo sana katika miaka kumi ya mwanzo ya uhuru na hata utekelezaji wa Azimio la Arusha.
Nimezaliwa Ilala, Dar es Salaam, Machi 11, 1966. Nilikuwa sijatimiza miaka kumi siku ile ya Februari 5, 1977 Chama Cha Mapinduzi kilipozaliwa.
Nakumbuka, pamoja na watoto wenzangu, kuwepo pale Ilala Bomani kushuhudia tukio lile la kihistoria. Barabara ya Uhuru ilifungwa. Ilikuwa ni sherehe kubwa. Hata tuliokuwa watoto wakati huo, tulijawa na matumaini ya mustakabali ulio bora kwa nchi yetu.
Na hili Chama Cha Mapinduzi kiwe bora zaidi, na Serikali iwe makini zaidi, basi, uhahitajika upinzani makini.
Maana, siku zote, mamlaka bila upinzani huzaa kiburi na majigambo. Huzaa hali ya kutokujali na kukosa usikivu. Taratibu, huzaa hali ya kujisikia u-bwana mkubwa. Hali hii ikiachwa ikaendelea, basi, husababisha madhara makubwa kwa nchi. Huleta hasara kubwa kwa nchi, kiuchumi na kijamii.
Maggid Mjengwa,
Iringa.