Miaka 22 iliyopita...

harder king

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
3,968
Reaction score
6,920
Habari wana jf

Ikiwa ni siku mpya na kila mtu akiwa kwenye purukushani za maisha tukiyandaa kesho mpya..hatuna budi kumwambia Mungu asante.

Lengo la Mimi kuleta mkasa huu hapa jamvini n pamoja na kujifunza na kuwatia moyo walio kata tamaa kimaisha

Twende kwenye point!
Miaka 22 iliyopita..

Nikiwa na umri wa kuanza darasa la kwanza niliyafuraia maisha japo hayakua ya kifahari ila uwepo Wa wazazi ulifanya familia yetu kua familia kamili..
Maisha yalisonga nakumbuka ugomvi Wa wazazi ulipelekea mama kuondoka na kutuacha na baba huku familia ikia na watoto wanne mimi nikiwa wa pili..

Baba alichukua jukumu la kutuhudumia kwa kila kitu ikiwemo kutupikia..kiufupi alichukua nafasi ya baba na mama.

Japo yeye na mama walitafuta suluisho sisi watoto hatukujua walikoishia na mambo yao ila mama hakurudi!

Mwaka moja baada ya mama kuondoka 'jumba' bovu lilizidi kuiangukia familia yetu baada ya baba kupatwa na tatizo la kiakili na kufanya ashindwe kutuhudumia kwa chochote na alivyoona hali yake inakua mbaya alituita Mimi na dada kwa kua ndio kidogo tulikua na uwelewa na alitueleza juu ya hali yake na alituambia hawezi tena kutusaidia kwa lolote na alitushauri tuende kwa wazee wake(babu na bibi yetu)tukalelewe huko ad atakapo kua sawa.
Tulimtii baba na tuliondoka sisi na wadogo zetu kuelekea kwa wazee

Tulianza maisha mapya tukiungana na watoto wa ndugu waliokua kwa babu Na bibi..kwakua hapakua mbali na kwetu tulikia tukimjulia baba hali kila tunapokua na mda
Hali ya baba ilibadilika na kua mbaya Zaid kwani ilifikia mahali baba anatembea barabaran hakiwa hajielewi huku akiongea maneno yasiyo eleweka.
Niliumia sana kila nilipokua nakutana na baba sikua na cha kumsaidia zaidi ya kulia..
Siku zilisonga na baba alipotea kabisa pale kijijini na kila tulipoenda kumtembelea nyumbani hatukumkuta..siku,miezi na miaka ilikatika bila kumuona baba wala mama japo mama alikua kwao lakini uwezekano Wa sisi kumuona ulikua mdogo..
Maisha na wazee hayakua mabaya wala mazuri kwani ndugu zetu tuliowakuta wazazi wao walikua na kipato tofauti na sisi..ilifanya kuwepo na matabaka kati yetu na wale tuiowakuta..kauli za kejeli kama kuitwa watoto Wa masikini na maneno makali tulizizoea

Mtu pekee aliekua akinitia moyo ni babu..huyu mzee alinipenda kwa kweli nakumbuka ilikua kila nikitoka shule alinikwepesha kufanya kazi ngumu..wakati wenzangu wanapangiwa kazi mimi niliambiwa nikachunge mifugo na Mara kwa mara babu alinitembelea machungoni..babu yangu alipenda sana utani na kila alivyonitembelea alipenda kuniimbia kanyimbo ka kunitania na baada ya kuakikisha nimecheka vya kutisha aliniita na kuniambia nikae Karibu nae..babu alipenda sana kunishauri kuhusu maisha na hali ya familia ya mwanae(baba) alinieleza jinzi anavyo washauri ndugu Wa baba watafute njia za kumsaidia baba..zaidi alinishauri nizingatie sana masomo kwani jukumu la kuiokoa familia yangu lipo mikononi mwangu..Nilikua na umri Mdogo lakini kila siku babu alikua karibu na mimi kunitia moyo..

Nakumbuka ilikua wkend mimi na ndugu wengine tulienda porini kukata majani..tuliporejea nyumbani tulikuta hali isiyo ya kawaida kwa wazee kwani kulikua na watu wengi.
Tulitua mizigo yetu na kutaka kujua nini kinachoendelea..tuliambia babu ameanguka shambani..ghafla nilijiisi mwili wote wa baridi machozi yalinitoka na nlipoteza matumaini ya kua na Furaha tena..

Walimpeleka babu hospital..badae daktar alisena babu alipatwa na kiarusi (strock)
Baada ya mda babu kua hospitality aliruhusiwa ila hakua akiweza kutembea peke yake aliitaji msaada Wa mtu kushikwa mkono..

Baada ya babu kufanyiwa mazoez ya viungo aliweza kutembea huku akisaidiwa na fimbo..angalau Furaha ya kua na babu karibu ilinirejelea tena ukaribu uliongezeka maana hakua akifanya kazi zaidi ya kutembe tembea na mara nyingi siku za wkend tulishinda wote..nakumbuka babu Mara nyingi alipenda kuniambi 'kumbuka umezaliwa wakiume peke yako hii vita unatakiwa upigane ushinde' kiukweli sikuelewa maana ya Yale maneno japo sasa naelewa!
Siku zilienda na nilimaliza darasa la saba nakumbuka babu aliniambia nichague kuendelea na masomo au anitafutie kazi kwa ndugu waliopo mimi..binafsi sikuona umuhimu Wa kusoma maana at a dada yangu ndugu walishindwa mlipia ada akiwa form1..nlichagua kutafutiwa kazi na ckutaka kusikia nimefaulu kujiunga na kidato..

Siku naondoka kijijini babu aliniita na kuniambia 'mjuu wangu kumbuka huendako na huikumbuke familia yako..kumbuka huna baba wala mama na jukumu la kuirejesha familia yako lipo mikononi mwako'

Nilikuja mjini nikiwa na umri mdogo ila sikua Mdogo kiakili kwani kauli za babu zilinikomaza kiakili.

Siku zote sikuacha kuwakumbuka wazazi wangu nliishi nikiwa MTU Wa mawazo na wakati mwingine nilijikuta nikilia mwenyewe kila nikiikumbuka familia yetu, nilijiisi mm ni yatima japo wazazi wapo..

Nilifanya kazi kwenye mazingira magumu ila sikukata tamaa..niliishi na maneno ya babu kichwani yalio nifanya nizidi kua jasiri..baada miaka miwili nilienda kuwatembelea wazee kijijini..babu alifurai sana kuniona na hakuacha kunitania kwa kuniimbia kale kawimbo cha tangu nikiwa Mdogo..babu aliniuliza juu ya familia yangu na aliniambia tena jukumu lipo mikononi mwangu..nakumbuka ilishatimia miaka kumi yangu wazazi wetu wapotee kwenye upeo Wa macho yetu
Babu aliniambia ni wakati sasa Wa mm kujenga upya makazi ya wazazi wangu
kwan ndio njia pekee ya kuwafanya warudi ata kama wapo mbali yy atajua
jinzi ya kuwapata..
Nilirudi mjina kupambana,, nikiwa na miaka17 nilifanikiwa kuyajenga tena makazi ya wazazi wangu japo hayakua yakisasa..
Kwa ushirikiano Wa babu tulifanikiwa kumpata mama na badae mama alitoa ushirikiano Wa kumpata baba..

Walau sasa maisha ya Furaha yalirejea na Mzigo nliokua nao ulianza kua mwepesa japo baba hakua amepona tatizo lake ila uwepo wake ulifanya mimi na ndugu zangu kuishi kama wengine tukiwa na Furaha na wazazi wetu...
Maisha yalisonga dunia yetu nikiwa nyepesi..na mpaka sasa tupo na wazazi wetu na kwakua ndugu zangu hawakubaki nyuma kupambana na maisha nao sasa wanajitegemea wakiwa na uwezo kama kaka yao.

Ni zaidi ya miaka 18 tangu nilipo Maliza kuwapigania wazazi wangu na badae ndugu zangu

SHUKRANI KWA BABU YANGU KIPENZI NATAMANI LEO WEWE NA BIBI MNGEKUWE MLE MATUNDA YA WAJUKUU ZENU HAKIKA MLISIMAMA KUAKIKISHA NASI TUNAKUA WATU KWENYE JAMII
MMETANGULIA LAKINI BADO MNAISHI NA SISI NAFSINI MWETU..

Sio mbona na nyie mkashare mikasa yenu mliopitia na badae kufanikiwa kusonga mbele.

Nb.Mimi sio mwandishi mzuri japo simzuii mtu kuja na povu humu!

young kilimanjaro
 
wengine hatukusoma sio kwa kudhamiria /
usawa uligoma ila ndio vichwa vya familia/
 
Umeingia jf kwa elimu ya msingi?, manake hujaelezea kama ulifanikuwa kuendelea na sekondari hadi .
 
wengine hatukusoma sio kwa kudhamiria /
usawa uligoma ila ndio vichwa vya familia/
Kweli kabisa mkuu hua namini kila mtu ana sehemu yake duniani mhimu nikupambana uipate kwa wakati.

young kilimanjaro
 
wewe ni tunu aliyoiona babu yako.. wengine wanawaza bakora kuwa ndo suruhisho.. nimependa njia aliyotumia babu yako kukupata na ukamuelewa + mazingira na tunu ya shauku iliyojificha ndani yako..
alikutoa pembeni ili usiangamie kisha akakuunda ili uje kuwa suruhisho kwa wale wengine. good logic.. utu uzima dawa
 
Umeingia jf kwa elimu ya msingi?, manake hujaelezea kama ulifanikuwa kuendelea na sekondari hadi .
Ni kweli humu nimeingia na elimu ya msingi..sikufanikiwa kuendelea na shule japo nilijiendeleza kupitia mitandao ya kijamii na kwa marafiki pia nilitumia dictionary kuijua lugha ya wazungu kidogo
Niseme tu sijutii kuikosa elimu!

young kilimanjaro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…