digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,756
- 17,279
Wakuu habari zenu, natumaini mu wazima wa afya
Naomba tuongelee maendeleo na juhudi za muheshimiwa Rais Magufuli katika kuhakikisha taifa letu linakuwa na maendeleo na kulifanya taifa letu kuwa na uchumi imara.
Katika hoja yangu naomba nijikite kwenye miradi mikubwa ambayo inampaisha na kumuweka kileleni mh JPM, baadhi ya miradi hiyo ni kama mradi wa umeme, reli, ununuzi wa ndege na ujenzi wa daraja la Busisi (Sengerema Mwanza), miradi hii yote imeiburiwa katika awamu ya tano. Hofu yangu na watanzania wapenda maendeleo ni kuwa baadhi ya miradi inayofanyika katika awamu hii huenda isimufurahishe Rais wa awamu ya sita na hivyo kuamua kuachana nayo naye kuja na miradi yake.
Hivyo naona kuna haja kubwa ya kubadili ukomo na kuruhusu Rais kuendelea kukaa madaraka kwa angalau miaka 15, hii itamfanya Mh Rais kukamilisha miradi yote mikubwa iliyoanzishwa katika awamu yake ya tank ili kuepuka Rais wa awamu ya sita kuja na mipango mingine na kuweka kando miradi hii iliyopo.
Tofauti na hapo kama hakutakuwa na mabadiliko ya mihula ya urais, naomba mheshimiwa Rais akazane sana ili anapomaliza miaka kumi ahakikishe miradi yote iliyokuwa chini ya utawala wake imekamilika
Ahsanteni