Mkuu Rose Marie - Uliyoyaongea yana ukweli nusu. Nitafafanua -:
Ni kweli nchi ndogo ndogo kama Tanzania zinatakiwa kuwa angalifu na jinsi zinavyojihusisha na China. Tahadhari zinazotolewa na Marekani kwa mataifa ya Africa kuhusu the dangers of Chinese Neo Colonialism ni za kweli na tunahitaji kuzizingatia. Nchi zinazoendelea kama Tanzania zinatakiwa kuwa makini sana na jinsi zinavyosaini mikataba ya kibiashara na hatimae kufanya biashara na China. Mikataba mingi huwa haitufaidishi vyakutosha na pia hutuumiza kiuchumi, kijamii na kiafya. Bidhaa zao (wachina) nyingi hazina ubora na nyingine zina madhara ya kiafya. Haya, pamoja na mambo mengine mengi, ni mambo ambayo tunatakiwa kuyaangalia kwa makini sana.
Jambo moja ulilokosea kwenye tathmini yako ni pale uliposema kwamba MIAKA 10 IJAYO CHINA ITATAWALA DUNIA. Based on extensive research that I have done, concerning future global super powers, ushahidi unaonyesha kuwa China will never rule the world, nor will it become the world super power. That will never happen in the next 100 years. Kwa mujibu wa kitabu kiitwacho The Next 100 Years by Michael Friedman, China will never rule the world due to the following key factors -:
- China haina millitary bases nchi za nje. Hakuna nchi yoyote itakayoweza kutawala dunia bila kuwa na military bases nchi za nje. Marekani na mataifa mengine machache sana yana military bases kwenye nchi nyingine duniani na hivyo kujihakikishia usalama na uwezo mkubwa wa kujilinda, kujihami na kupigana. Bila kuwa na uwezo huo hakuna nchi yoyote itakayoweza kutawala dunia. Ili kutawala dunia ni lazima nchi iwe na vitu viwili vya msingi- nguvu za kijeshi na nguvu za kiuchumi. Mambo hayo lazima yawepo yote mawili na yaende sambamba kama hands and gloves.
- China ni nchi masikini sana in interior China. China ni nchi tajiri kwenye majimbo machache sana likiwemo Beijing, Shanghai na Guangzho. Other than those few states the rest of China is extremely poor, dry and weak. Ukifanya average kimsingi China bado ni taifa masikini.
- Utajiri wa China ni artificial. Utajiri wa China umetokana na wizi wa utaalamu na technologia. Karibu kila Kila kitu wanachojivunia wachina wameiga au kuiba (ujuzi, utaalamu na technologia) kutoka mataifa ya magharibi. Uchumi unaotegemea wizi wa utalaamu na technologia sio utajiri wenye nguvu nawa kudumu. Wachina hawafanyi researchs and innovation. Huwa wanasubiri kuiba tu.
Kuna sababu nyingine nyingi, ila based on those few, it suffice to conclude that China will never rule the world in the next 100 years.
Nawakilisha!
Muya Kamota
Cleveland Ohio.
Ni vema tukaelewa China itatawala Dunia miaka 10 ijayo na hakuna wa kuzuia hilo,Iwapo Marekani itafanikiwa kujitenga na Ulaya wakashindwa kufikia muhafaka juu ya bajeti mambo yanaweza kuwa mapema zaidi,Nchi iliyokuwa maskini kabisa miaka 30 iliyopita leo hii wanaongoza kuwa na uchumi imara,viwanda vingi visivyo na hesabu,investor kila pembe ya dunia.
Tuelewe uchumi wa China kwa sasa hivi umefika zaidi ya $2 trillion kulinganisha na tanzania ambayo imesimama kwenye $900million,,,,,,,,,,hakuna Biashara yoyote ile duniani ambayo haijakumbwa na uoga kuhusu China
Marekani walipotuonya kuhusu China ku recolonize Africa hawakukosea lakini na wao wamejaa uoga wa kuja kutawaliwa na China,,,,,kwa jinsi ninavyowajua Wachina watakuwa radhi kuangamiza baadhi ya mataifa duniani hasa waafrica ili wapate wanachokitaka
tunachokiona Tanzania ni cha mtoto kulinganisha na wanachokifanya mataifa mengine ya kiafrica kama Angola na Botswana,kusema kweli katika Africa ni Kaburu wa Africa Kusini pekee ameweza kuwa tishio kwa mchina items of investment
kazi tunayo hatuna pa kukimbilia zaidi ya kuamka usingizini na kujaribu kupunguza makali ya Mchini kwenye kutawala Dunia