Mi natoa ONYO: Kuna Member wa Humu JF ana mahusiano na mchumba wangu. Tusije Kulaumiana Bure

Kwa nini uile peke yako!!Kwani alizaliwa kwa ajili yako huyo? Acha ubinafsi!!
 
Nimelazimika kusema hili ingawa najua wengine mnaweza kukebehi na kunidhihaki. Haina shida nimeamua kusema iwe kama angalizo maana kuna siku nitakuja tu kufanya reference. Sisi wengine hatujui sana kuzungumza au kurushiana maneno. Hii naweka tu kama ushahidi ili nikimfanya mtu kama ambacho nilimfanya shababy mmoja mwaka 2015 tusilaumiane.

Mimi nina mchumba ambaye kwa sasa ni mwezi wa 5 nipo naye. Kazi zangu ni za safari safari sana, so kila wakati nakuwa safarini ili niandae mazingira mazuri ya maisha yetu ya ndo hasa ukichukulia ye mchumba wangu amemaliza chuo mwaka wa 2 sasa hana kazi. Yeye ana muda mwingi sana so anakuwa home na sometime mishe mishe zake ila ni muda sasa naona amezoeana na member mmoja humu ndani ambaye amekuwa mara nyingi akiuza sana chai na habari zake za ajabu ajabu. Ni mhuni na baradhuli tu huyo member wala si mtu wa staha hata kidogo mimi ni mtu mstaraabu sana na mpole.

Nilianza kuona kila mara huyo member akianzisha thread huyu mchumba wangu analike na anachangia sana na huwa akisoma anasoma anacheka mpaka machozi yanamtoka muda wote akiwa nami anajisahau anaaanza kusoma threads za huyo jamaa baadaye nikamwambia mi sipendi anavyokuwa occupied sana na huyo jamaa mpaka anajisahau anasema "ila wanaume wengine bwana yaani ukikaa na huyu kaka itakuwa mtu hata stress huana unacheka tu" hilo liliniudhi maana asili yangu mimi ni mtu ambaye nipo serious na sina sana stories hasa za kipuuzi puuzi kama za huyo member humu ndani za ngono na jinsi wanavyotendana na wanawake.

Siku moja kweli ananiambia hebu siku moja nasi tujaribu hii style ya .... nikashangaa katamka jina nikamwambia kwa upole kuwa kwa nini anakuwa obsessed na huyo jamaa mhuni na malaya?" akaniambia "aaah.. Nawe baby una mind vitu vidogo tu mtu mwenyewe hata simjui" juzi juzi hapa akawa ananambia unajua good girls wanapenda sana bad boys..sikutilia maanani lakini nlianza kuona mashaka pale nilipoona anasema anataka aonane na huyo mtuniliingia kwenye inbox texts zake jamiiforums nikakuta anawasiliana naye sana wanacheka wanataniana na sometime wanachat maneno mpaka huyu mchumba anasema ameloana hili lilinikwaza hasa anaposema "wee..naomba nikuone live maana una vituko sana"

Nimeamua kuwa hili suala niliweke wazi huyu dada mimi nlishamhudumia sana chuo mpaka amemaliza ni mimi nlikuwa natoa ada kumwonesha tu kuwa nipo serious pesa za kutoka kwa wazazi wake alikuwa anatumia kufanyia mambo yake na nilimruhusu nikamwambia basi aangalie kama anaweza zifanyia kazi flan ya kuzalisha, she didnt do anything progressive with the money.

Leo hii mwendawazimu mmoja humu ndani anataka kuja kufanya masikhara na mchumba wangu its ok..mi naweza kumwachia ila afaham atarudisha pesa zangu zote nlizotumia kama si direct bas itakuwa indirect najua kwa nini nasema hivi na simtishii...yeye si mwanaume?ajaribu tu kumgusa huyu mchumba wangu kimapenzi atanifahamu kuna post iliwekwa humu kama sikosei mwaka jana..Kuna mtu alifanywa kitu kibaya sana kudandia wake za watu gharama aliyolipa ilikuwa kubwa na mpaka sasa anaendeleakulipa toka mwaka 2015.

Nimetoa tu hili kama angalizo.
Chizi maarifa umeongea kwa uchungu mkali sana,kweli kumegewa kunauma.
 
nmegundua nyie watu mnaniombea mabaya sana..hamwoni kwua sasa ndo mnampa uthibitisho kabisa????????????????????????? nmewakosea nini mimi jamani mpaka mnaniombea mabaya hivi.......................
Naona mkuu biti limekuingia sasa
 
Ahahaha kama hadi analoa akiongea na mm basi jua ananipenda!
Mruhusu aje kuniona kidogo au kama vipi njoo nae tutafune mishikaki wote hapa Kurasini ghetto
 
Pole Sana. Punguza wivu bado hujamuoa, nae bado anatafuta labda wewe si type yake.
 
Muongo mleta thread mara nimemjua mchumba wangu kwa miez mitano hapohapo nilimlipia ada kipindi yupo chuo na kamaliza chuo miaka miwili iliyopita! Arrgggg which is which
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom