Mhusika wa ESCROW aachiwa huru na mahakama ya Kisutu

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Ofisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru Ofisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko baada ya kumuona hana hatia katika tuhuma za kupokea rushwa ya Sh40.4 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa zamani wa IPTL, James Rugemalira.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema Mahakama imemuachia huru Saliboko baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake pasipo kuacha shaka yoyote.

Hakimu alisema licha ya kumwachia huru, upande ambao haujaridhika unaweza kukata rufani.

Alisema mshtakiwa huyo aliposomewa shtaka kwa mara ya kwanza alikana na kwamba, wakati wa usikilizwaji Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dennis Lekayo alipeleka mashahidi watatu.

Saliboko aliyekuwa anatetewa wa Wakili Jamhuri Johnson wakati wa kujitetea alifanya hivyo mwenyewe.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu alisema shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka ambaye alikuwa mpelelezi mkuu, Emmanuel Koroso, alieleza kwamba alijiridhisha kuwa fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya Saliboko na pia hakuwa na maelezo mazuri kuonyesha namna alivyozipokea.

Hakimu huyo alisema mashahidi wawili kutoka Benki ya Mkombozi walithibitisha Saliboko alifungua akaunti kama mteja wao na fedha hizo ziliingizwa katika akaunti yake na kuzitoa mara tatu,

Saliboko alikubali kufungua akaunti katika benki hiyo na kuingiziwa fedha hizo na Rugemalira ambaye alikuwa na makubaliano naye ya kumtafutia shamba katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam ili aendeleze biashara zake.

Hakimu alisema kwa mujibu wa Sheria za Takukuru mtoa rushwa na mpokeaji wote ni wakosaji na kuhoji kama kweli ilikuwa rushwa kwa nini Rugemarila hakupelekwa mahakamani kushtakiwa maana ni mtoaji.
 
Serikali walikurupuka hapo wanakuwa kama hawajui sheria jamani. Unampelekaje mahakamani mtu mmoja wakati watuhumiwa wapo wawili na wote wanapatikana ki urahishi.
 
Na wale majaji nao walipewa kwa ajili ya kujenga mahakama maana ruge alitaka afungue biashara za mahakama
 
Duh hii ndio tanzania
Hapa hamna kesi hata moja ambayo serikali itashinda...wakati mazingira ya rushwa yanaonekana kabisa hata wale makamishna wa tra na wale wa brella wote watashinda na ruge nae kwanini hajashtakiwa?? Hivi na ile ya wale majaji kuundiwa jopo vipi mrejesho wake au ndio yalishaisha..
 
Hakimu alisema kwa mujibu wa Sheria za Takukuru mtoa rushwa na mpokeaji wote ni wakosaji na kuhoji kama kweli ilikuwa rushwa kwa nini Rugemarila hakupelekwa mahakamani kushtakiwa maana ni mtoaji.

Huyu hakimu naye vipi? Unamwingizaje Rugemalila mtu ambaye hayuko kwenye hati ya mashtaka kama mshtakiwa kwenye mashtaka yaliyokuwa mbele yake? Yeye ilibidi ashughulike tu na huyo aliye mbele yake.Kazi ya hakimu si kutunga kesi kwa mtu asiyekuwepo kwenye hati ya mashtaka kama mshtakiwa.
 
Kwa hali hiyo basi
Hapa hamna kesi hata moja ambayo serikali itashinda...wakati mazingira ya rushwa yanaonekana kabisa hata wale makamishna wa tra na wale wa brella wote watashinda na ruge nae kwanini hajashtakiwa?? Hivi na ile ya wale majaji kuundiwa jopo vipi mrejesho wake au ndio yalishaisha..
Kwa maana hiyo basi na mwendesha mashtaka WA serikali aongezwe kwenye list ya Majipu
 
Afu hao hao DPP na PCCB wanasema tuwataje mafisadi......
Mi naona PCCB ifutwe tu
 
Kuna haja ya kubadilisha mfumo wa mawakili wa serikali. Kesi walizoshinda na walizo shindwa ziwekwe wazi na wakili wa wilaya na mkoa wawe wanagombea.

Hakuna haja ya kuwa na mawakili wa serikali wanashindwa kesi kila halafu bado wanapandishwa vyeo.
 
Hapa hamna kesi hata moja ambayo serikali itashinda...wakati mazingira ya rushwa yanaonekana kabisa hata wale makamishna wa tra na wale wa brella wote watashinda na ruge nae kwanini hajashtakiwa?? Hivi na ile ya wale majaji kuundiwa jopo vipi mrejesho wake au ndio yalishaisha..

Niliwahi kusema humu, Beyond No Doubt ni msumari wa moto kwa kesi nyingi. Na jambo hilo limewekwa na mahakama kote duniani ili kutenda haki, maana watu wengi wangefungwa kama kipengele hicho kisingekuawepo.

Hivyo kabla ya kufungua kesi, ni budi mfunguaji au mwendesha mashtaka ajiridhishe kama ushahidi wa kutosha upo. Kule The Hague, hali imekua kama hiyo, Wakenya walifunguliwa kesi za kusababisha vurugu baada ya uchaguzi. Kwa sasa ni wawili tu wamebaki, wengine wote Mahakama haikuona cha kuwashtaki nacho hasa ushahidi!
 
Huyu hakimu naye vipi? Unamwingizaje Rugemalila mtu ambaye hayuko kwenye hati ya mashtaka kama mshtakiwa kwenye mashtaka yaliyokuwa mbele yake? Yeye ilibidi ashughulike tu na huyo aliye mbele yake.Kazi ya hakimu si kutunga kesi kwa mtu asiyekuwepo kwenye hati ya mashtaka kama mshtakiwa.
Wewe kila kitu mradi kinalaumu utendaji wa vyombo vya setikali unatetea. Hivi hata hili la Takukuru ambalo hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza sheria hawezi kufanya nalo unalitetea?
Wewe ni sawa na mashine ya kunyolea, inanyoa kote bila aibu
 
Kisheria huwezi mfikisha Mahakamani mpokea rushwa ukamuacha mtoa rushwa!

Kesi za ki pu mba vu kabisa hizi za trial and error!Bila Ruge hamna kesi
 
Alafu kule Geita Mwizi wa Kuku kachomwa moto na Wananchi wenye hasira,alikuwa Mwanafunzi wa Shule ya Msingi aliacha Shule akiwa Darasa la Tatu alienda kumwibia Mwalimu wake so sad.
 
Serikali walikurupuka hapo wanakuwa kama hawajui sheria jamani. Unampelekaje mahakamani mtu mmoja wakati watuhumiwa wapo wawili na wote wanapatikana ki urahishi.
kweli walikurupuka huwezi kumshinda mtu kesi kwa ushahidi wa kufungua akaunti na kupewa pesi na mtu! Unaona walivyogeuza kibao cha malengo ya kupewa hiyo pesa?!! Mi mtu ambaye huwa naona asingeweza kuruka hiyo kamba alikuwa ni Chenge ambaye kwa mtazamo wangu naona moja kwa moja alipokea ile pesa ikiwa ni rushwa kwa kuwa alifanikisha IPTL kupata ule mkataba mbovu kwa wakati huo alivyokuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
 
Niliwahi kusema humu, Beyond No Doubt ni msumari wa moto kwa kesi nyingi. Na jambo hilo limewekwa na mahakama kote duniani ili kutenda haki, maana watu wengi wangefungwa kama kipengele hicho kisingekuawepo.

Hivyo kabla ya kufungua kesi, ni budi mfunguaji au mwendesha mashtaka ajiridhishe kama ushahidi wa kutosha upo. Kule The Hague, hali imekua kama hiyo, Wakenya walifunguliwa kesi za kusababisha vurugu baada ya uchaguzi. Kwa sasa ni wawili tu wamebaki, wengine wote Mahakama haikuona cha kuwashtaki nacho hasa ushahidi!
Ndivyo wenzetu wanavyofanya ili ufunguliwe charges public prosecutor na police wawe na ushahidi kamili hata kama mtu anafahamika ni kala rushwa or anafanya irregularities inabidi wawe na supportive documents au ushahidi wa kimazingira. ila hapa tanzania imekua wanakurupuka mtu anakamatwa hana hata hatia hawana ushahidi wowote unamkuta mtu anakaa mahabusu muda mrefu mwsho wa siku anaachiwa ushahidi hamna...huo muda mtu aliokaa mahabusu wanaulipaje sasa?????
 
kweli walikurupuka huwezi kumshinda mtu kesi kwa ushahidi wa kufungua akaunti na kupewa pesi na mtu! Unaona walivyogeuza kibao cha malengo ya kupewa hiyo pesa?!! Mi mtu ambaye huwa naona asingeweza kuruka hiyo kamba alikuwa ni Chenge ambaye kwa mtazamo wangu naona moja kwa moja alipokea ile pesa ikiwa ni rushwa kwa kuwa alifanikisha IPTL kupata ule mkataba mbovu kwa wakati huo alivyokuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
Huyu ilibid angeshtakiwa kuhusiana na ushiriki wake kwenye kusajil kampun hewa kwaio hapo ruge alikua analipa
fadhira
 
Ndivyo wenzetu wanavyofanya ili ufunguliwe charges public prosecutor na police wawe na ushahidi kamili hata kama mtu anafahamika ni kala rushwa or anafanya irregularities inabidi wawe na supportive documents au ushahidi wa kimazingira. ila hapa tanzania imekua wanakurupuka mtu anakamatwa hana hata hatia hawana ushahidi wowote unamkuta mtu anakaa mahabusu muda mrefu mwsho wa siku anaachiwa ushahidi hamna...huo muda mtu aliokaa mahabusu wanaulipaje sasa?????
Tatizo ni siasa kuingia hadi kwenye mambo yasiyo ya kisiasa. Mi naona hata majeshi, sheria navyo vinaathiriwa na siasa. Hebu tujiulize hili tamko la juzi la kwamba mafisadi na wahujumu uchumi watafirisiwa, hivi hiyo sheria ya kutaifisha mali za wahujumu uchumi haikuwepo? Au ilikuwa likizo?
 
Hii ndy Tanzania!subirini na hao wakina masamaki na wenzake utaskiaaa ushindi waooo
 
Back
Top Bottom