Mheshimiwa RC Makonda Hakika Wewe ni Kiongozi Mwenye Maono

Nolelo Nobert

Member
Mar 22, 2016
22
18
Kwa Takribani mwaka mmoja nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu utendaji wa Kiongozi Makonda tangu alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni mpaka hivi karibuni alipoteuliwa na mheshimiwa raisi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Nikirejea kwenye kwenye kichwa cha habari, kwa nini nsema ni kiongozi mwenye maono;
Mosi, Tangu alipoteuliwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,alianza kazi kwa kasi ya ajabu kwa kutatua kero mbalimbali za wananchi hasa akigusa maeneo ambayo ndio yalikuwa na changamoto nyingi, mfano ajira kwa Vijana, kutatua miggogoro ya ardhi na kulipa suala la elimu kipaumbele kwa kuongeza shule katika wilaya kinondoni na kuwawezesha walimu kusafiri bure ilikuwahi majukumu ya kkazi. Binafisi kwangu nilmuona ni kiongozi mwenye upekee sana na anastahili pongezi za pekee na hakika Mheshimiwa raisi alimuona na kumuona anafaa kumuongezea majukumu kwa utendaji wake uliotukuka.

Kama tunakumbuka nyuma kidogo, Mheshimiwa Makonda aliandaa kongamano kubwa la vijana katika viwanja vya Leaders club,ilikuweza kujadili kwa pamoja suala la uhaba wa ajira kwa Vijana. Mheshimiwa Makonda aliona mbali, nakufanya jitihada za kuwa kutanisha vijana ili wao wajadili mbinu na kuona kwa pamoja fursa zilizopo katika kutengeneza ajira, Hakika ni jambo la kipekee na linapaswa kuona ni kiasi gani lilikuwa na tija kwa vijana.

Vilevile Mheshimiwa hakuishia hapo tu, pia alianzisha fursa kemu kemu kwa vijana, mfano tamasha la kutafuta vipaji kwa vijana wa kinondoni.Niweze kusema mpaka sasa baadhi ya vijana wameweza kujiajili katika sekta hiyo,Hakika hatuna budi kumpongeza kwa jitihada zake Mheshimiwa Makonda.
Hayo ni machache niliyotaja kati ya mengi ambayo mheshimiwa Makonda ameyafanya katika kipindi cha wadhifa wake wa ukuu wa wilaya ya Kinondoni.

Baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John P Magufuri kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Makonda kwa kasi,morali na weledi ule ule, ameanza kwa kasi ya ajabu katka utendaji wake kwa nafasi aliyopewa.

Hapa nitapenda kujadili mikakati tisa ambayo Makonda amekuja nayo katika kubadili jiji la Dar es salaam na kuwa na mwonekano wa kisasa, ingawaje wadau mbalimbali wamejitokeza na kukosoa mikakati hii, lakini mimi binafsi bado ni muumini kwamba, mheshimiwa atafanikisha mikakati hiyo pindi kila mmoja wetu atakapo muunga mkono na sio kubeza jitihaha zake.
Katika kujadili mikakati hii,sitajadili mikakati yote nitajikita zaidi katika suala la kuweka Mji wa Dar es salaam safi,
  1. Usafi, katika mkakati huu wa usafi Mheshimiwa Makonda,ameanzisha Mashindano ya Mtaa Msafi katika mkoa wa Dar es salaam, kwamba mtaa utakoshinda utazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 20 za kitanzania na balozi wa mtaa husika atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 5 na zoezi hili litaanyika kila baada ya miezi mitatu na umeahidi kutoa pikipiki kwa maafisa wa wa porisi katika kanda maalumu ya Dar kuweza kuwa fuatilia wale watakaokuwa wanatupa takataka ovyo (real great and sound promising). Katika utekelezaji wa mkakati huu wa kuweka jiji la Dar es salaam kuwa safi,hakika Makonda atafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, ili kufanikisha hili kunapaswa kuweka misingi imara ya utekelezaji wake ili mkakaki huu uweze kuwa na tija,
  • hapa nitatoa ushauri kwa Mheshimiwa Makonda namna ya utekelezaji wa mkakati huu.
- Katika kuweka Mtaa msafi, sio tu kufagia na kuzibua mitaro, kwa uelewa wangu wananchi wengi wana hitaji elimu ya uhifadhi bora wa taka, kwa maana ya kutenganisha taka,elimu ya urejeshaji,Upunguzaji na kurejea Matumizi, hii ni elimu muhimu sana kwa wakazi wa jiji la Dar, ukizingatia miundo mbinu si rafiki katika suala la taka.Uhalisia juu ya hilo tunaweza tukajikumbusha yakiyotokea siku ya tarehe 9 disemba, usafi ulifanyika lakini taka zikashindwa mahali pa kwenda kutokana na uhaba wa miundo mbinu iliyopo katka jiji.Ndio maana bado na sisitiza elimu hii kwanza,mosi, inapunguza uzalishaji wa taka na kuonyesha fursa zinazopatikana katka takaambazi zinaweza kuongeza kipato kwa wananchi pia. Ukizingatia jiji la Dar essalaam kwa siku linazalisha taka kiasi cha tani 4,342 na asilimia 40 ndizo hupelekwa dampo, hivyo nyingine hubakia mitaa na kutupwa kwenye vyanzo vya maji na sehemu za wazi na hapo ndio mwanza wa jiji kuonekana chafu.

Hivyo ni vema wakatafutwa wataalamu katika utoaji wa elimu hii,ili wahusishwe katka mkakati huu, mfano kuna mashirika mengi ya kijamii mmfano Nipe Fagio,Borda, Roots nad shoots na mashirika mengi yanayotoa elimu juu ya Mazingira na yaliyobobea katka masuala ya utoaji wa Elimu,hivyo ungetumia kamati husika kubaini mashirika hayo nakuyashirikisha katika mkakati huu.

- Ilikuweza kufanya mkakati huu, uwe na tija zaidi, ni kuhakikisha huduma ya uzoaji wa taka inakuwa yakujitosheleza,kwa maana mitaa mingi haina mtoa huduma/ Mkandarasi wa kuzoa taka,ndio maana suala la taka linakuwa changamoto katika mitaa mingi. hivyo Manispaa husika kwa kushirikiana na viongozi wa mitaa, wsimamiwe ili kuhakikasha wanapata mkandarasi anayeweza kutoa huduma ya uhakika, kwa kufanya hivyo ni nina imani mkakati huu utafanikiwa.

- Wanachi wahimizwe suala la ulipaji wa ada ya taka kwa wakati na bila usumbufu.

- Sheria zisimamiwe ipasavyo ilikuwaadhibu wale watakao patikana na makosa ya uchafuzi wa mazingira.

- Kuandaa vikundi vya kijamii vyenye hamasa ya kuleta mabaliko katika jamii, viweze kusimamia zoezi hili, kwa kufanya haya hakika tutapata Dar es salaam safi
.

Mheshimiwa Makonda umekuja na mikakati mingi ambayo yote ina tija kubwa katika kuchochea maendeleo katika jiji la Dar es salaam. Hakika unahitaji ushiriki wetu wa dhati ili kufanikisha maendeleo ya jiji letu.

Wako Mdau wa Mazingira.

VIVA MAKONDA....!!!!!!!!

 
Mkuu,
Umeandika mengi, unaweza ukaweka na data ili hoja zako ziwe valid.

● Mfano, Unasema amesaidia "ajira kwa vijana", Je! ni vijana wangapi wamepatiwa ajira na Makonda?

●Kulikuwa na migogoro mingapi ya ardhi!? Makonda kamaliza mingapi?

Ogopa sana mtu anaefanya kazi na media 24/7
 
Mimi hainiingii akilini sheria zote za kusimamia ustaarabu katika jiji zimevurugwa na hakuna wa kukemea! Pita barabara zote za kariakoo mwenda kwa miguu huna pa kutembea kupata mahitaji muhimu bila bugudha! Barabara zote zimegeuzwa masoko! Pita barabara ya uhuru njia za watembea kwa miguu zimekuwa ni sehemu ya maduka, sehemu za kuweka generators na packing za magari!

Huwa kwa ulofa wangu najiuliza ni kiasi gani mtu analipa kuweka standby generators yake permanently njia ya waenda kwa miguu kwa miaka mitano?? Nenda mbagala barabara ya mabilioni inazuiwa na dala dala na biashara katikati ya barabara! Mtu unakaa foleni masaa matatu hakuna anayeona? Yapo mengi ila haya ni madogo na rahisi kuyafanyia kazi
 
Nataka niongezee ushauri kwa mheshimiwa makonda kama anapita humu
auangalie ushauri wangu na kuupima,kama utafaa nami naamini unafaa;

Nashauri kila soko linalopokea bidhaa kutoka shamba ambazo huja
na takataka nyingi mfano nyasi,majani ya migomba n.k
yajenge sehemu za kuchomea taka taka hizo(incenerators) kama zile za kwenye
mahospitali,hizi zitasaidia kupunguza mzigo mkubwa wa taka
zinazopelekwa kwenye madampo.Gharama ya kujenga sehemu
hizo siyo kubwa kama tunavyodhani ukilinganisha na usombaji wa hizo
takataka kwenda dampo.Ni rahisi kusomba majivu kuliko manyasi(volume wise).

Hili likifanyika kwa sehemu kubwa takataka nyingi
kwenye masoko zitapungua na usafi utadumishwa.
 
Back
Top Bottom