Mheshimiwa Rais Samia, wasaidie Vijana wako wenye sifa lakini wamekosa nafasi kujiunga na Jeshi la Polisi

bugembe

Senior Member
Sep 13, 2021
116
316
Mheshimiwa Rais, mimi ni Mstaafu Serikalini. Niliitumikia Serikali kwenye Idara ya Afya kwa muda wa miaka 39 mpaka nilipostaafu mwaka 2019. Katika kipindi chote hiko, nimesaidia kuwalea Vijana watatu wa kike ambao Wazazi wao waliniletea Mjini nisaidie kuwasomesha kutokana na wao kukosa fedha au kutokuwa na mwamko wa kuwasomesha. Nililibeba jukumu hilo kama Mzazi.

Mabinti wawili niliwasomesha mpaka walipomaliza Kidato cha Nne mwaka 2014. Wakaendelea na Kidato cha Tano na kumaliza Kidato cha Sita mwaka 2017. Wote wakachaguliwa kwenda JKT kwa mujibu wa Sheria. Matokeo yalipotoka mmoja alipata Division One na mwingine Division Two.

Baada ya kumaliza Mikataba yao huko JKT, wamekuwa wakijihusisha na shughuli ndogondogo kwani uwezo wa Mstaafu mimi kuwalipia Ada Chuo Kikuu sina kwa sasa maana walijaribu kuomba mikopo (Loan Board) lakini hawakupata. Mnamo mwezi August 2021, Jeshi la Polisi lilitangaza Ajita kwa vijana wenye Elimu ya Kidato cha 4, 6 na Chuo Kikuu.

Vijana wangu hawa waliomba nafasi hizo LAKINI wote WAMEKOSA kisa walifaulu sana (Division One na Two). Kijana wa Tatu yeye nilimsomesha mpaka Kidato cha Nne na alipata Division Four (Point 27), pia alipitia JKT lakini nae AMEKOSA nafasi hizo kisa alipata Point 27 na wanaotakiwa ni wenye kuanzia Point 29-32!!.

Mheshimiwa Rais wewe ni Mama, ni kweli kama Nchi tumefikia huko kwamba KUFAULU ni disqualification ya kupata kazi!!!
TAFADHALI Mheshimiwa Rais, tengua utaratibu huo wa Jeshi la Polisi. Ni vema wangewaita wote wenye 1-4 waje wapambane kwenye Usaili na sio kuwabagua waliofeli.

NAKUOMBA Mheshimiwa Rais liangalie suala hili kwa jicho la huruma
 
Kumbe mnataka ajira za kidhalimu huku mkikataa kutetea demokrasia kwa nguvu mnayotumia kuomba kazi za hovyo, pambaneni na hali zenu upolisi sio kazi ni utumwa tu , kama mtu yuko sawasawa kichwani hawezi kuwaza kuwa polisi
 
Kumbe mnataka ajira za kidhalimu huku mkikataa kutetea demokrasia kwa nguvu mnayotumia kuomba kazi za hovyo, pambaneni na hali zenu upolisi sio kazi ni utumwa tu , kama mtu yuko sawasawa kichwani hawezi kuwaza kuwa polisi
Nimeona kuna sehemu huko wanakuandama....
 
waambie waombe kazi zingine.

tunataka iron boys/girls ambao tukiwaambia piga watapiga bila reasoning!

hao dv I na II watakuja kuanza harakati za kisomi mwisho Wa siku waharibu kazi.

huoni walimu Wa msingi wenye dv fooo na siriiii mbovumbovu walivyo watiifi kwa wakubwa? huwezi kuwalinganisha na walimu wa seko wenye one na two zao Kali za fomu4 na six lakin walienda ualimu Si kwa kupenda wao bali mkopo na umasini Wa kwao. wanawasumbua sana viongoz wao hata uwapigeje biti hawaelewi wala kuogopa.

Nasisitiza polisi tunataka dv fooooo na zero ya 34.

ova
 
Back
Top Bottom