Mheshimiwa Rais Magufuli unda tume haraka kuchunguza mikataba ya gesi

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Baada ya kusikia ripoti ya mchanga wa Dhahabu Mheshimiwa Rais Magufuli naona ni jambo la busara kuunda tume kuchunguza Mikataba ya gesi kwani kuna dalili na huko tunapigwa. Hata gharama ya ujenzi wa bomba una utata mkubwa.
Mungu akubariki na Mungu Ibariki Tanzania
 
Mikataba yote sio ya Gesi tu.

Na sheria ya hiyo mikataba ibadilishwe ili Taifa liweze kunufaika na Rasilimali zake
 
Hahaaaah tume kuchunguza mkataba wa gesi...yeye mwenyewe si alikuwa sehemu ya bunge wakati huo mkataba unapitishwa kwa hati ya dharula bungeni na akapiga kura ya ndiyoooo
tena kuna mgombea mmoja akasema tutafaidi gesi yetu yeye akaja kumjibu: gesi tumewapa wachina wafanye uchunguzi miaka saba
 
Hizo zote zitakuwa mbwembwe, kama ana nia atueleze mikataba yote ikoje. Amekuwa waziri kwa miaka 20 (?) Msitudanganye kuwa hajui mazingaombwe waliyokuwa wanafanya.
 
Akili ya kichadema kichwa kikubwa busara 00000 sasa yeye alipokua waziri unazani angefanya nini mtu mmoja kila zama na mambo yake kama serikali zilizopita zilikua more corrupt usitegemee angefanya kitu, kumbukeni Amina chifupa alichofanyiwa pindi anapigania kuhusu madawa ya kulevya je alidumu?jiulize hivyo kila zama na mambo yake mwacheni rais apambane hakika tutashinda achanani na miakili ya kijinga isiyo na tija kwa taifa
 
Rais, amesema kote huko na mikataba yote sasa hivi ni kufanyika Kwa uwazi.

Na amesema kampuni itakayoishitaki serikali mahala popote pale Basi isahau kuwekeza hapo Tanzania.

Hapa, hadi watanzania waliohusika kutupiga watachukuliwa hatua sitahiki popote pale walipo.

JPM, Hapa kazi tu.
 
Akili ya kichadema kichwa kikubwa busara 00000 sasa yeye alipokua waziri unazani angefanya nini mtu mmoja kila zama na mambo yake kama serikali zilizopita zilikua more corrupt usitegemee angefanya kitu, kumbukeni Amina chifupa alichofanyiwa pindi anapigania kuhusu madawa ya kulevya je alidumu?jiulize hivyo kila zama na mambo yake mwacheni rais apambane hakika tutashinda achanani na miakili ya kijinga isiyo na tija kwa taifa

Na kuanzia sasa ndiyo tutaona watu wenye kupigania maslahi ya nchi yetu.

Maana sasa hivi ni Taifa tunapigana na mabepari, sasa kama kweli tu wazalendo ndiyo tutumie vyama na mambo mengine kusaidia nchi yetu na watanzania Kwa pamoja.
 
huko lazima tunapigwa. lile bunge la wagonga meza lilipitisha kwa hati ya dharura zile sheria za gesi. naunga mkono hoja...
 
Hahaaaah tume kuchunguza mkataba wa gesi...yeye mwenyewe si alikuwa sehemu ya bunge wakati huo mkataba unapitishwa kwa hati ya dharula bungeni na akapiga kura ya ndiyoooo
Kwahiyo yeye peke yake angefanya sheria ipite hujui ni majority ndio wanapitisha
 
Back
Top Bottom