Kuwa rais wa nchi ni sawa na baba wa familia, rais ni kiongozi ambaye anatakiwa kuwa karibu na wananchi awaongoze kwa amani na upendo huku busara, hekima ikitamalaki sawa na unapokuwa baba wa familia. Lakini hii ni tofauti kwa rais wetu kila anaposimama kutoa maamuzi anatoa kwa hasira kana kwamba kuna ugomvi na watu.
Rais wetu amekuwa mtu wa hasira kuu, chuki na visasi kwa makundi tofauti ya wananchi kila analolifanya linalalamikiwa na wananchi. Swali la kujiuliza hasira hii, chuki hii, visasi hivi vinatoka wapi? Tumemkosea nini sisi wananchi mpaka atuongoze namna hii, cha kustaajabisha hata wateule wake wameiga style hii ya uongozi wamekuwa watu wa kufoka foka tu hata pasipo na ulazima wa kufoka.
Walioko karibu na rais wetu wamwambie apunguze ukali, chuki na visasi maana nchi hii haitaendelea kama atakuwa mtu wa hasira, chuki na visasi ajifunze kusamehe na atumie busara na hekima katika kuongoza watu. Na akumbuke kwamba anaongoza watu wazima na sio watoto.