Mheshimiwa Pius Msekwa yuko wapi jamani?

Koala

Member
Aug 28, 2011
97
107
Leo nimejikuta namkumbuka mzee huyu,Spika mstaafu.Mzee alikuwa jembe sana ktk hekima na uongozi wa Bunge letu tukufu.Natamani kujua yuko wapi na anajishughulisha na nini hv sasa!?
 
Jamani Mzee Wetu kapumzika anakula pension yake ya ustaafu taratiiibuuu...tafadhari tumuacheni apumzike.
 
Huyu Mzee Ana Historia iliyotukuka Nchini lakini Hana Makuu kabisa

Ngoja tuwasaidie Vijana wamfahamu vizuri Huyu Gwiji na Nguli mkimya wa Siasa hapa Nchini

1) Alikuwa Katibu wa kwanza wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1964

2) Alikuwa Mwnykt wa Kamati ya kuchagua Jina la Nchi na baada ya kukusanya Maoni mbalimbali ndio waliamua iitwe TANZANIA baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanziba ( October, 1964)

3) Katibu Mkuu wa Kwanza wa Chama cha Mapinduzi 1977

4) Spika wa Kwanza wa Bunge la Tanzania baada ya kurudishwa Vyama vingi 1995

5) Ndie Alietayarisha Mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

6) Ni Miongoni mwa Wanafunzi mahiri wa Mwalimu Nyerere wakati akifundisha Pugu Secondari Miaka ya 1940s

7) Ndie alipendekeza Kijana ( wakati huo) Jakaya Mrisho Kikwete awe Katibu wa Harmonisation TANU na ASP Kisiwandui Znz na ndio ikawa mwanzo wa kujulikana kwa Jakaya ngazi ya Taifa kutokana na ubora wa ile kazi akiwa Kijana wa 27years tu 1977
 
Huyu Mzee Ana Historia iliyotukuka Nchini lakini Hana Makuu kabisa

1) Alikuwa Katibu wa kwanza wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1964

2) Alikuwa Mwenyektwa Kamati ya kuchagua Jina la Nchi na baada ya kukusanya Maoni mbalimbali ndio waliamua iitwe TANZANIA baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanziba ( October, 1964)

3) Katibu Mkuu wa Kwanza wa Chama cha Mapinduzi 1977

4) Spika wa Kwanza wa Bunge la Tanzania baada ya kurudishwa Vyama vingi 1995

5) Ndie Alietayarisha Mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

6) Ni Miongoni mwa Wanafunzi wa Mwalimu Nyerere wakati akifundisha Pugu Secondari Miaka ya 1940s
Duuh,hv kumbe alihusika mpk kwenye hati ya muungano?
 
Nakumbuka wkt akiwa mbunge wa Ukerewe alijenga rami inaanzia kanisa la romani katoliki mpk mjini Nansio
 
Hakuna alicho isaidia Wilaya yake tofauti na viongozi wengine waliopata lidhaa toka kwa wananchi wao. Hadi leo Ukerewe imebaki kua maskn naya kusktisha sn. Bashe kaanza mwaka juzi ona anayo yafanya jimbon kwake. Ona Msuya na wengine. Apumzike tu
 
Uko sawa mkaruka, hata mahande, kazirankanda, malegea mpaka centre (nansio) wanaheshimu mchango wake ,
Ila najua hawezi kuja.kumsahau mama Mongela, Hakika hawa watu 2 waliofanya kazi Nzuro sana UK...ila machemli ndo alivurunda kabisa. Vip ka GI lugola yupo??

Nakumbuka wkt akiwa mbunge wa Ukerewe alijenga rami inaanzia kanisa la romani katoliki mpk mjini Nansio
 
Back
Top Bottom