Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903



Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani Fredrick Sumaye leo amehudhuria Kongamano la Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Mbeya lililokwenda sambamba na Mahafali ya CHASO leo tarehe 10 Juni 2017 yaliyofanyika katika ukumbi wa Mtenda Jijini Mbeya.
Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na Katibu wa BAVICHA Taifa Julius Mwita, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, Katibu Mwenezi wa BAVICHA Taifa Edward Simbeye na viongozi mbalimbali wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Songwe.
Katika kongamano hilo mgeni rasmi Mheshimiwa Fredrick Sumaye aliwakabidhi vyeti wahitimu kutoka vyuo mbalimbali vya Mbeya ambao ni wana CHADEMA Students Organisation (CHASO) pia katika tukio hilo alikuwepo mwanaharakati wa wanafunzi wa vyuo vikuu na vijana Alphonce Lusako ambaye alipata fursa ya kukinadi kitabu chake cha Sauti ya Watetezi wa Haki Vyuoni.