Mhe Sitta, Utaweka wapi sura yako?

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,410
Reaction score
14,119
Uchu wa madaraka unapopitiliza kwa kujaribu hata kukwepa matakwa ya wananchi wenyewe waliowaweka wanansiasa madarakani, mwisho wake ni aibu.

Mh Sitta pamaoja na sifa yake ya "Speed and Standards" lakini spidi ya safari hii ilikuwa inaeleekea kuzimu.
Pamoja na maoni ya Tume ya Warioba , ambayo ni maoni ya wananchi, juhudi nyingi zimewekwa kuyaondoa maoni hayo na kuweka maoni ya wanasiasa.


Pamoja na UKAWA kuwa ni wa vyama vya upinzani, lakini katika hili wameonyesha kidogo uzalendo wa kupigania maoini ya wananchi.
Pamoja na hili tunamshukuru Mh JKikwete kwa kuliona hili ili nchi isiingie mtafaruku usio wa lazima.
Hata wana CCM kama Mwigulu Nchemba waliliona hili na mapema.

Hivyo basi ni aibu iliyoje kufikia sasa kuwa hela ya kodi za wananchi imeliwa , na muda mrefu sana umetumika na hakuna cha maana cha kuonyesha kwa matumizi haya ambayo yangeepukwa kwa kutikia maanani maoni ya wananchi.

Maoni ya wananchi mengi sana hayakuwa kichama wala kidini wala kwa manufaa ya kikundi chochote.
Ni mategemeo yetu kuwa walioshinikiza kuendelea na mchakato mufilisi wawajibike kisheria au kisiasa kwa hili.

 
Mpaka sasa SITTA ameibuka kidedea, unachokifanya ni kutapatapa, hivi kama TCD na JK wamekubaliana bunge liendelee mpaka oktoba 4 , nani mshindi?
 
Sasa km mchakato utahairishwa hao mbuzi huko dodoma wanaendelea kujadili nini yaani njaaa mbaya 'hicho wanachojadili kitatupwa na mchakato utaanza upya kwa sheria mpya kwa kuwa makosa yameonekana ni kujaza wanasiasa na kugeuza bunge la jmhuri kuwa la katiba sasa wanajadili nini hao mbuzi waliobaki mjengoni
 
Imekuaje leo mwanaCCM unakubaliana na UKAWA au hii sredi kuna mtu ameandika kwa niaba yako?
 
Ataificha sura yake kwa mkewe na familia yake tu.
 
Mbona anazungukazunguka? Toboa bungw limehailishwa mpaka 2016 back.hao weu watoke huko ddm haraka
 
Pigo siyo kwa Sitta maana yeye alipewa maelekezo kasimamie moja, mbili, tatu.........hicho kikundi kilichotoa maelekezo ya mpaka Raisi afungue Bunge baada ya Rasimu kuwasilishwa na kufutilia mbali tovuti ya Tume ingefaa hiyo majina yao yawekwe wazi ili Watanzania wawafahamu.

Mimi wa kwanza ni Waziri wa Katiba na Sheria - Asha Rose Migire, Tovuti iko wizarani kwake
 
Mpaka sasa SITTA ameibuka kidedea, unachokifanya ni kutapatapa, hivi kama TCD na JK wamekubaliana bunge liendelee mpaka oktoba 4 , nani mshindi?

Mkuu hii ni sheria uliyounda bunge hilo ambayo inaweza kutenguliwa tu na mahakama au BJMT...Aidha Sitta kwa kutumia mawazo yake mgando aliomba hadi tarehe 29 october eti awe amemaliza kazi yote ya katiba ibaki kura ya wananchi! Huu uwehu wa ajabu hivi ndo Sitta alikuwa ameujaza kichwani mwake!!!
 
Mpaka sasa SITTA ameibuka kidedea, unachokifanya ni kutapatapa, hivi kama TCD na JK wamekubaliana bunge liendelee mpaka oktoba 4 , nani mshindi?[/QUOTE


stupid, unachekelea kodi yako kuliwa Kama sad aka? Sad
 
Mpaka sasa SITTA ameibuka kidedea, unachokifanya ni kutapatapa, hivi kama TCD na JK wamekubaliana bunge liendelee mpaka oktoba 4 , nani mshindi?

Ila umburula mwingine inamaana wewe huelew tu,? unafkria kwa kutumia nn mkuu? Hata bondia hupgwa na kuanguka chini mara kadhaa nakuumia lakini refaree akimuuliza unaweza kuendelea hukubali kuendelea hata kama anajua kabisa keshapgwa na hata ajitahid vip hawez kushnda. Ndvyo yanavyofanya maccm hayatak yaonekane yamechemka.
 
Halooo me mbona kama sielewi hilo azimio aiseeeee,
Kama wamekubaliana vikao vya BMK kuendelea mpaka Octoba 4, then mchakato uhairishwe mpaka baada ya uchaguzi mkuu hapo mwakani
Nini cha maana wananchi tulichokivuna kwenye mazungumzo ya Kikwete na TCD, ikiwa kinachoendelea sasa bungeni sio mjadala unaotokana na rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Warioba?

Kama BMK itaendelea mpaka ipatikane katiba iliyopendekezwa, je hiyo si itakuwa batili kwa mujibu wa UKAWA?
Si itakuwa haijatokana na rasimu ya pili iliyoandaliwa na Tume ya Warioba!

Kama UKAWA wamekubali hili, ni wazi wametusaliti sisi wananchi ambao tulikuwa tunasapoti msimamo wao; pia hakukuwa na umuhimu wowote wa wao kususia vikao, ilhali wanakubali kile kitakachozalishwa na mijadala waliyoisusia?

NIMECHANGANYIKIWA HAPA!
 
Sitta mjanja,,baada ya kuikoroga CCM si atajirudia tu ktk chama chake cha CCJ yeye na wenzake akina Nape, Kirango nk…kwa hiyo hapa walioumia ni CCM na wananchi ndio zaidi
 
Ni kweli Sita aliingizwa mkenge,mkuu wa kaya ndiye chanzo cha sakata lote hili,na sasa watu wanampongeza kwa kitu ambacho alijua mwisho wa siku kitakwama na yeye ndiye mkwamuaji,watanzania fungueni macho
 
Its a BIG SHAME TO HON. MZEE SITTA.
Afu naona vibaya au ndo ilivo kuwa kaishaanza KUINAMA?
 
Mkuu hii ni sheria uliyounda bunge hilo ambayo inaweza kutenguliwa tu na mahakama au BJMT...!
Kama ulimsikiliza vizuri Humphrey Polepole katika lile bandiko la "Nilichosema kuhusu katiba chanel 10). utakuwa umegundua kuwa Rais anweza kufuta uteuzi wa wajumbe wote wa BMK kwa kuwa ndiye aliyewateua (mwenye mamlaka ya kuteua ana mamlaka pia ya kutengua) Na rais akiamua kutengua basi kunakuwa hakuna wajumbe; na BMK linakufa kifo cha ghafla!
Bandiko hilo ni https://www.jamiiforums.com/katiba-...channel-10-television-juu-ya-katiba-mpya.html
 
Umepewa nafasi ya kufanya uchaguzi na kupata wajumbe wapya kwa bmk lijalo. Ni juu yako kuwaondoa hao waliopindisha mawazo ya wananchi na kuweka ya kwao. Hii ni fursa nzuri - tuitumie.
Usisahau pia kuwa tutakuwa na rais mwingine ambaye si lazima aje na mawazo kama ya JK. Kumbuka mbunge mmoja aliwahi kusema " anayeshikila nguvu za dola (instruments of power) ndiye mwenye uwezo wa kusema katiba mpya iwepo na ikawa au sitaki katiba mpya na ikawa. Alitoa mfano wa Afrika ya kusini
 
Ni kweli Sita aliingizwa mkenge,mkuu wa kaya ndiye chanzo cha sakata lote hili,na sasa watu wanampongeza kwa kitu ambacho alijua mwisho wa siku kitakwama na yeye ndiye mkwamuaji,watanzania fungueni macho

Sita kama mwanasesere tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…