Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,334
- 72,798
Nimeona tena Leo Rais kafanya ziara ya kushtukiza (kama ilivyoripotiwa) katika taasisi nyeti sana nchini nayo ni BOT.
Hapo ndio ambapo anaweza kupata dira na mwelekeo wa hali halisi ya uchumi na nguvu ya taifa kifedha. Hivyo ilikuwa vyema kwa wataalamu wetu pale kuwaandaa kwa ujio wa Rais wa mara ya kwanza ili wajipange na kumueleza kiufasaha nini kinafanyika, changamoto zake, wanahitaji msaada gani toka kwake kama Rais na wamepanga kufanya nini ili uchumi upae na sarafu yetu iwe strong.
Ziara za kushtukiza zimeshajenga picha kuwa ni kukamuana majipu na kufukuzana kazi, na sidhani wataalamu kama utawavamia na kutegemea kupata neno la manufaa kwao kama utapata huku wakiwa na tension kuwa hapa pengine nafukuzwa kazi.
Sasa tembelea maeneo muhimu na ukute wataalamu hata wafanyakazi wa kawaida wakiwa na mood ya kujadiliana nawe nini kifanyike tutoke hapa tulipo hayo ya kuwashtukiza mafisadi,wezi na wabadhilifu achia vyombo vyako vinavyohusika PCCB, POLISI,TISS, nk waendelee lakini chini ya close supervision yako.
Hii itasaidia kuondoa unafiki wa watumishi wakuonapo bali watakupa fact hata za udhaifu wa maamuzi ya serikali na nchi itasonga.