Mhe. Rais vitabu vya taasisi ya elimu ni vibovu kweli

Mapigomoto

Member
Jan 21, 2016
19
11
MHE. RAIS VITABU VYA TAASISI YA ELIMU NI VIBOVU KWELI


Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliunda tume ya kuchunguza ubovu wa vitabu vya Taasisi ya Elimu na kwa nini ilitokea hivyo.


Mhe. Rais, vitabu vya Taasisi ya Elimu kama ilivyoelezwa na kujadiliwa bungeni, vitabu hivyo ni vibovu kweli kweli. Tume hiyo kuwatafuta waliohusika ni sawa. Lakini kwa nini walifanya hivyo sio hoja.


Endapo Taasisi ya Elimu itafanya kazi hiyo kwa utaratibu mwingine hautaleta manufaa yoyote kwa taifa letu. Taasisi ya Elimu hadi sasa ina miaka minne tangu ipewe jukumu la kuandika vitabu vya shule lakini hakuna vitabu vilivyokubalika. Kila inapojaribu, hutoa vitabu vibovu ambavyo huwa vinachomwa moto. Miaka minne hiyo yote shuleni bado hatujapata vitabu. Kwa kweli shule ni vitabu. Wanafunzi bora tutawapataje? Taasisi ya Elimu inahangaika na masilahi ya pesa tu na sio vitabu bora. Hawakujua kuwa vitabu vyao ni vibovu na kuvipeleka shuleni mpaka walipoambiwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wabunge. Ni wazi kuwa wataalamu wa Taasisi ya Elimu wana matatizo ya kitaaluma.


Mapendekezo ya kupata vitabu bora ni kama ifuatavyo:

(a) Serikali iunde Kamati ya kuhakiki ubora wa vitabu na machapisho mengine ya kufundishia shuleni iliyohuru. Wanakamati lazima wawe ni walimu ambao ni bora katika masomo husika. Kazi ya kamati hiyo iwe ni kutoa alama ya ubora wa kila kitabu kinachohakikiwa.

(b) Wizara ya Tamisemi iunde kamati ya kuchagua vitabu vya kutumika shuleni kulingana na taarifa ya kamati hapo juu ya kuhakiki ubora wa vitabu.


Hivyo waandishi wa vitabu waruhusiwe kuandika vitabu ila vipite kwenye machujio hayo mawili. Waandishi, Taasisi ya Elimu, PATA na wadau wengine wakitumia mfumo huo, vitabu vitakavyoenda shuleni vitakuwa bora. Hili litakuwa suluhisho la vitabu vibovu shuleni.
 
Ungeweka picha ya hivyo vitabu ingependeza tuone huo ubovu wao wanakosea wapi
 
Si Waziri alishatoa ahadi za nini arafanya bungeni juzi juzi hapa, au kaachia watoto waendelee kusoma hivyo vitabu?
 
Kama hivi vipya ni vibovu, kwa nini wasitumie vya zamani? Mbona sie tumesomea hivyo hivyo na tuna run Tanzania?
 
S
Kama hivi vipya ni vibovu, kwa nini wasitumie vya zamani? Mbona sie tumesomea hivyo hivyo na tuna run Tanzania?

Vitabu vya wachapishaji binafsi vilitathminiwa na EMAC na ikatoa ithibati kuwa ni vizuri kwa shule. Kwa nini serikali isivinunue na kuleta shuleni wakati waalimu tunahangaika watoto hawana vitabu? Mh Rais tupunguzie mzigo wa kufundisha, tuletee vitabu na vingozi vya mwalimu.
 
Haya mambo ya vitabu bhana. Nayo ni sawa tu na makinikia. Ni ugonjwa uleule. Watu inaelekea hawajali maslahi ya nchi bali mtu unashawishika kusema ni wachumia tumbo. Sijui ni lini mara ya mwisho serikali ilinunua vitabu kwa ajili ya shule. Hii taasisi inachelewesha tu maendeleo ya nchi. ni kisiki kilichokaa njiani.

Sasa iwapo wametumia miaka minne kuandika vitabu VIBOVU, ina maana watoto waliokuwa Darasa la 1, hivi sasa wako Darasa la 4. Wameenda miaka hiyo yote bila vitabu. Je, hiyo haimaanishi kuwa kuna gape ya miaka 4 kitaifa ya mdororo wa elimu? Je, watawapeleka tuition ili kuzipa pengo hilo? Na itakuaje kama suala hili litafumbiwa macho na wakaendelea kupewa muda zaidi wa kuboronga mambo?

Ah! Mambo ya nchi hii kule yalikotoka...!!! Yanachosha. Mheshimiwa Rais hajawahi kutoa tamko kuhusu Elimu. Huenda atafanya hivyo ili kuondokana na hatari hii.
 
Back
Top Bottom