VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Tulianzia kwenye ziara za ghafla.Tukafuata utumbuaji majipu;ukaacha majeraha yasiyo na raha. Yakafuata makatazo: kukakatazwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kukatazwa kwa Bunge mubashara. Ikaja awamu ya bajeti kupangwa na asiyepaswa na hata kupanguliwa isivyotakiwa.
Ikaja zamu ya kauli na matamko ya viongozi waandamizi hadi wale wadogo. Kila mmoja aliagiza,alielekeza na kusema 'nataka mfanye hili au lile; mjenge hiki au kile; mbomoe hiki au kile; mswekeni lupango huyu au yule'. Matamko na maagizo yakatamalaki hadi kubaki. Ukafuata uhakiki wa uhakika na hata kutiliwa shaka.
Sasa tumehamia kwenye 'maigizo' yasiyo na mipangilio. Ni 'maigizo' ya kupambana na mihadarati. Muongozaji alikuwa 'akipanga' na watakaotajwa ili ionekane amethubutu. Hadi kuwalipa 'washukiwa' kunasemwa. 'Maigizo' haya yamezaa mengine lukuki kuanzia mahakamani hadi mitaani. Ni mwendo wa 'maigizo'.
Mambo yamekuwa mchafukoge. Haijulikani kama nchi tunashughulika na nini wakati gani. Sasa ni vigumu kung'amua tofauti ya kauli za kweli na zile za 'kutafutia kiki'. Imekuwa ngumu sasa kuona muendelezo wa jambo fulani la kitaifa, mfano kuhamia Dodoma kwa Serikali. Ni vigumu mno kuona kilichopangwa na kinavyotekelezwa.
Watanzania wamebadilika. Kutoka kujenga hoja hadi kudandia hoja. Kwasasa, kauli ya kiongozi au mwanasiasa na hata msanii huwa national agenda. Tumefika katika wakati wa kutia huruma. Tumefika wakati ambapo haijulikani mipango ya Serikali au hata ya watu binafsi. Wananchi sasa hawamjui 'mkweli' wala 'muongo'. Mambo sasa ni shaghalabaghala!
Ingawa Mhe. Rais husema unainyoosha nchi, lakini nchi sasa inapinda zaidi. Ikifika kupinda kama dawa ya mbu, ikinyooshwa itaishia kuvunjika. Nchi inapaswa kurudishwa kwenye mstari sasa. Suluhisho ni kuiacha demokrasia ichukue mkondo wake. Tuiache siasa iisaidie Serikali kutenda majukumu yake.
Mwafaaaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam