Mhe. Rais, mpaka na Jerry Muro nae yumoooo!

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Wakati Rais Kikwete anaongoza nchi hii kati ya 2005-2012, kuna wakati aliwapa sana vijana nafasi za uwaziri na hilo lilimpelekea baadhi kumpongeza na wengine kumlaumu. JK alikuwa na imani na vijana na aliwapa nafasi. Kuna baadhi walifanya kazi, kuna baadhi walimwangusha. Mwaka 2012 alifanya mabadiliko ya uongozi hasa katika baraza la mawaziri na vijana kibao “wakapigwa chini”. Na “watu wazima” wakiwamo akina Prof. Mhongo kuingia kupiga kazi.

Rais JPM nae, kawa na imani na vijana kama alivyofanya mtangulizi wake JK. Wakuu waliopita akiwamo Mwl. Nyerere alifanya kazi na vijana wakati huo kama akina Sita kama Waziri, Warioba kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Tumesoma katika historia pia, kati ya mwaka 1980-83 Balozi Mahiga alikaimu ukurugenzi wa TISS akiwa na miaka 35 kwa miaka 3. Aidha kabla ya hapo alikuwa mkurugenzi wa Mafunzo Ofisi ya Rais akiwa na miaka 32. Hii inaonesha mifumo serikalini toka mwanzo imekuwa ikiwapa nafasi vijana.
Kwa upande wa vijana ambao walifanya vyema toka huko nyuma wamekuwa wakipanda toka ngazi moja kwenda juu. Aidha kuna wengine wamekuwa wakihamishwa kwenda kufanya kazi za kibalozi kama walivyo akina Dr. Nchimbi. Ikumbukwe, Nchimbi aliwahi kupoteza kazi ya uwaziri wa mambo ya ndani na leo hii ni balozi nchi Brazil.

Historia pia inaonesha kuna vijana ambao vibarua viliwahi “kuota magugu” akiwamo Mhe. Gambo ambae kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Arusha. Wakati wa JK, Mrisho Gambo alipoteza kazi ya U-DC, ila baadae alikumbukwa na kuingia tena uwanjani “dakika za mwishoni” mwa awamu ya JK. Apoingia JPM, Mrisho Gambo alifanya kazi akiwa DC Kigoma, baadae DC Arusha na kisha baadae tena U-RC Arusha.

Viongozi vijana akina Jerry Muro, Jokate, David Kafulila, Pastrobas Katambi, Eric Kitwala, Moses Machali na wengineo, Mhe. Rais kawaamini sana kufanya kazi wakati wake ili kuwatumikia Watanzania.
Mnayo fursa ya kufanya vyema mkapaa kwenda juu hali kadhalika mnaweza kutotimiza malengo ya “muajiri” na ipo siku mkawekwa pembeni kama livyotokea kwa wengine ambao walitolewa ili hali walikuwa na nguvu.
Katika mabadiliko haya, ya Ma-DC kuna vijana ambao wametolewa kwa kukosa ubunifu na kwenda sawia na kasi ya “mkuu” ambae yeye anataka nafasi ya madaraka iwe ni utumishi kwa umma hali kadhalika kutatua kero za “waajiri wake” ambao ni wapiga kura.

Biblia imeandika, kwa kukosa maono watu hupotea. Na siku za mwisho hizi, vijana wataona maono. Kuna fursa kubwa ya utumishi ambayo mmepewa wote ambao “weekend” hii pongezi zimekuwa nyingi sana kwenu. Mkiwa na vision ambayo inashabihiana na dira ya maendeleo 2025 kufikia uchumi wa kati kwa Watanzania walio wengi, mtapaa tuu.
Tafsiri rahisi ambayo JPM aliwahi kuisema, ukipewa jukumu la uteuliwa kwanza jipe pole, maana yeye yuko “interested na deliverables”. Mna kazi kubwa nasi tunawaombea kwa Mola ili mkifanya vyema, wakati ujao, mteuaji achungulie tena katika “pool” ya vijana na kuwakumbuka wengine ambao watamsaidia katika kuifukuzia dira ya maendeleo 2025 na utekelezaji wa ILANI ya CCM 2015-20.

Kwa wale mliotoka uwanjani, karibuni benchi, bila shaka mkajipanga upya na mnaweza mkarejea kwa nguvu na ubunifu mpya. Cheo ni dhamana, inakuwa na furaja ukitumikia dhamana mpaka kustaafu kama ilivyo kwa wengine waliostaafu kwa kufikisha umri. Ila, kuanguka, ipo suku unaweza kuibuka, kama akina Mzee Mwinyi waliwahi kutoka katika nafasi ya uwaziri na miaka ya baadae, waka-bounce back na kufikia cheo ya Urais wa Zanzibar na baadae Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati mmoja Makongoro Nyerere akiwa Dodoma lijitabainisha kama mchezaji alie benchi. Na walio benchi ni wengi saaana kuliko walio ndani. Sitaki kuamini walio benchi wanaombea mabaya mlio uwanjani mfeli. Bali wanakuombeeni heri ili kumtumikia “mkuu wa kaya” ambae kwa sasa katiba yetu imempa madaraka ambayo watoto wa mjini wanasema “ku-hire” na “ku-fire”.
Njia pekee ambayo itawafanya mdumu kwa muda mrefu na kuwa na ubunifu wa hali ya juu kutatua kero za Watanzania na kuweka rekodi iliyotukuka katika maeneo yenu ya kazi. Bila shaka, wananchi watawasifu na kuwaombea heri nanyi mtapaa zaidi. Tanzania ina mambo mengi ya kufanya kama mnajipanga kimkakati kwa nia njema ya kuwatumikia Watanzania, kesho yenu itakuwa bora kuliko jana na leo yenu.

Kila la heri katika utumishi kwa wote mlioteuliwa na poleni kwa wale ambao mmeanguka ili hali umri na nia ya kutumika ilikuwepo!
 
Mleta mada kuna kitu hukielewi watetea serikali hutakiwa kusimama Na serikali iliyopo madarakani no matter what ili kulinda image ya serikali mbele ya public hadi raisi aliyepo amalize muda wake salama.Mfano escrow kipindi cha Kikwete ingesababisha nchi kupinduliwa Na CCM kushindwa uchaguzi.Raisi Kikwete alitangaza wazi kuwa zile pesa si za serikali pamoja Na presha za bunge Na maushahidi kibao watetezi wa serikali walisimama kidete kujenga hoja serikali ionekane iko sahivi Kikwete amalize ngwe yake salama Na nchi isipate msukosuko kuwa kama kiko tatizo litashughulikiwa mbele Kwa mbele baada ya nchi kuruka salama.Pesa za escrow zilipolipwa tu zilienda kugharimia kampeni za Lowasa Na Ukawa!!!! Sasa mara ingine hutokea ikagundulika kuwa waliopinga escrow walikuwa sahihi Na mamlaka za uteuzi kuwapa uteuzi Na baadaye wakiguundua kuwa Na Wale waliounga mkono raisi Kikwete kuwa zile pesa hazikuwa za serikali pia kuwa walikuwa sahhi in good faith for national interest waweza rudishiwa vyeo vyao hata kuwa promoted vyeo vikubwa kuliko walivyokuwa navyo.Hakuna Kazi ngumu duniani kama kutetea taifa lisiangamie.Kwa hiyo usishangae.Unaona mtu kabwagwa uteuzi baadaye anaibuka juu sana kuna factors nyingi
 
Nimekuja mbio nikidhani umemcritisize Jiwe kwa kumteua Jerry Muro huku ukiambatanisha na madudu take!! Hujakitendea haki kichwa au uzi umekosa kichwa kinachoendana nao
 
Eti anawapa fursa vijana!!! Hivi hamwonagi uwoga au aibu kuandika hivi? Ok, piga kazi hata muro nae alikuwaga na hoja kama hizi hizi kama wewe, hatimaye kala shavu nawe zamu yako yaja. Kila la heri mkuu wa wilaya mtalajiwa.
 
Wakati Rais Kikwete anaongoza nchi hii kati ya 2005-2012, kuna wakati aliwapa sana vijana nafasi za uwaziri na hilo lilimpelekea baadhi kumpongeza na wengine kumlaumu. JK alikuwa na imani na vijana na aliwapa nafasi. Kuna baadhi walifanya kazi, kuna baadhi walimwangusha. Mwaka 2012 alifanya mabadiliko ya uongozi hasa katika baraza la mawaziri na vijana kibao “wakapigwa chini”. Na “watu wazima” wakiwamo akina Prof. Mhongo kuingia kupiga kazi.

Rais JPM nae, kawa na imani na vijana kama alivyofanya mtangulizi wake JK. Wakuu waliopita akiwamo Mwl. Nyerere alifanya kazi na vijana wakati huo kama akina Sita kama Waziri, Warioba kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Tumesoma katika historia pia, kati ya mwaka 1980-83 Balozi Mahiga alikaimu ukurugenzi wa TISS akiwa na miaka 35 kwa miaka 3. Aidha kabla ya hapo alikuwa mkurugenzi wa Mafunzo Ofisi ya Rais akiwa na miaka 32. Hii inaonesha mifumo serikalini toka mwanzo imekuwa ikiwapa nafasi vijana.
Kwa upande wa vijana ambao walifanya vyema toka huko nyuma wamekuwa wakipanda toka ngazi moja kwenda juu. Aidha kuna wengine wamekuwa wakihamishwa kwenda kufanya kazi za kibalozi kama walivyo akina Dr. Nchimbi. Ikumbukwe, Nchimbi aliwahi kupoteza kazi ya uwaziri wa mambo ya ndani na leo hii ni balozi nchi Brazil.

Historia pia inaonesha kuna vijana ambao vibarua viliwahi “kuota magugu” akiwamo Mhe. Gambo ambae kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Arusha. Wakati wa JK, Mrisho Gambo alipoteza kazi ya U-DC, ila baadae alikumbukwa na kuingia tena uwanjani “dakika za mwishoni” mwa awamu ya JK. Apoingia JPM, Mrisho Gambo alifanya kazi akiwa DC Kigoma, baadae DC Arusha na kisha baadae tena U-RC Arusha.

Viongozi vijana akina Jerry Muro, Jokate, David Kafulila, Pastrobas Katambi, Eric Kitwala, Moses Machali na wengineo, Mhe. Rais kawaamini sana kufanya kazi wakati wake ili kuwatumikia Watanzania.
Mnayo fursa ya kufanya vyema mkapaa kwenda juu hali kadhalika mnaweza kutotimiza malengo ya “muajiri” na ipo siku mkawekwa pembeni kama livyotokea kwa wengine ambao walitolewa ili hali walikuwa na nguvu.
Katika mabadiliko haya, ya Ma-DC kuna vijana ambao wametolewa kwa kukosa ubunifu na kwenda sawia na kasi ya “mkuu” ambae yeye anataka nafasi ya madaraka iwe ni utumishi kwa umma hali kadhalika kutatua kero za “waajiri wake” ambao ni wapiga kura.

Biblia imeandika, kwa kukosa maono watu hupotea. Na siku za mwisho hizi, vijana wataona maono. Kuna fursa kubwa ya utumishi ambayo mmepewa wote ambao “weekend” hii pongezi zimekuwa nyingi sana kwenu. Mkiwa na vision ambayo inashabihiana na dira ya maendeleo 2025 kufikia uchumi wa kati kwa Watanzania walio wengi, mtapaa tuu.
Tafsiri rahisi ambayo JPM aliwahi kuisema, ukipewa jukumu la uteuliwa kwanza jipe pole, maana yeye yuko “interested na deliverables”. Mna kazi kubwa nasi tunawaombea kwa Mola ili mkifanya vyema, wakati ujao, mteuaji achungulie tena katika “pool” ya vijana na kuwakumbuka wengine ambao watamsaidia katika kuifukuzia dira ya maendeleo 2025 na utekelezaji wa ILANI ya CCM 2015-20.

Kwa wale mliotoka uwanjani, karibuni benchi, bila shaka mkajipanga upya na mnaweza mkarejea kwa nguvu na ubunifu mpya. Cheo ni dhamana, inakuwa na furaja ukitumikia dhamana mpaka kustaafu kama ilivyo kwa wengine waliostaafu kwa kufikisha umri. Ila, kuanguka, ipo suku unaweza kuibuka, kama akina Mzee Mwinyi waliwahi kutoka katika nafasi ya uwaziri na miaka ya baadae, waka-bounce back na kufikia cheo ya Urais wa Zanzibar na baadae Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati mmoja Makongoro Nyerere akiwa Dodoma lijitabainisha kama mchezaji alie benchi. Na walio benchi ni wengi saaana kuliko walio ndani. Sitaki kuamini walio benchi wanaombea mabaya mlio uwanjani mfeli. Bali wanakuombeeni heri ili kumtumikia “mkuu wa kaya” ambae kwa sasa katiba yetu imempa madaraka ambayo watoto wa mjini wanasema “ku-hire” na “ku-fire”.
Njia pekee ambayo itawafanya mdumu kwa muda mrefu na kuwa na ubunifu wa hali ya juu kutatua kero za Watanzania na kuweka rekodi iliyotukuka katika maeneo yenu ya kazi. Bila shaka, wananchi watawasifu na kuwaombea heri nanyi mtapaa zaidi. Tanzania ina mambo mengi ya kufanya kama mnajipanga kimkakati kwa nia njema ya kuwatumikia Watanzania, kesho yenu itakuwa bora kuliko jana na leo yenu.

Kila la heri katika utumishi kwa wote mlioteuliwa na poleni kwa wale ambao mmeanguka ili hali umri na nia ya kutumika ilikuwepo!
WAPUNGUZI SIASA WASAIDIE MAENDELEO YA SEHEMU HUSIKA!!!!!!!
 
Kwani ilihitaji utabiri...!?? Ilijuliakana aina ya madc wa jiwe... Na jerry alikuwa na sifa hizo..lilikuwa ni swala la muda tu..kwa hiyo wasijisifu sana...maana aliutafuta kwa udi na uvumba...kuwa msemaji wa chama zaidi ya polepole
 
Back
Top Bottom