VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kauli zako na matendo yako vinatutisha. Unatoa kauli direct na zile indirect. Mbaya zaidi, kauli nyingi za kutisha huzitoa mbele ya wakuu wa vyombo vya usalama (Usalama wa Taifa, JWTZ, Magereza, Polisi na Uhamiaji). Kwanini?
Uliwahi kusema kuwa wananchi wanapaswa kuviogopa vyombo vya dola. Kuviogopa tena-katika karne hii ya mambo shirikishi? Ukasema tena mbele ya Mawakili kuwa hata wao waweza kukamatwa na kuswekwa rumande wakiwatetea waovu. Pale, IGP-Mkuu wa wakamataji alikuwepo. Kwanini?
Kitisho chako cha kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa na Bunge kutooneshwa mubashara nacho bado kinauma,kukereketa na kufukuta. Juzi tu hapa, uakautamani hadi u-IGP ili utishe wananchi wako kwa vitendo. Kwanini?
Tunajua kwenye uchaguzi huwa kuna mambo mengi. Uchaguzi huacha majeraha mengi. Uchaguzi huzaa kupania na kulipizia, Lakini uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka mitano. Katika kushughulika na yatokanayo na uchaguzi, Mhe. Rais nenda taratibu. Waweza kusomba hata wasiotakiwa.
Tambua ya kuwa watanzania walikuchagua kwa wingi wao wa kura mwaka 2015 kuwa Rais wao kwa kuwa walikuamini, walikuthamini, walikupenda na kukuheshimu. Kwanini usiyalipe hayo ambayo ndizo hazina za wananchi kwako kupitia kauli na matendo yako?
Mhe. Rais, bado tunakuhitaji katika utumishi wa Taifa letu. Tunakuhitaji utuhudumie,ututumikie,utusikie,utuhurumie,uturuhusu kusikia mikutano ya hadhara na Bunge Mubashara na kadhalika. Huna haja ya kuwatisha wanaokupenda!
Happy Valentine Day Mr. President!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam