Mhe. Lowassa atakuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya CHASO kesho

Status
Not open for further replies.

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Mhe. Edward Lowassa Kesho anatarajiwa Kuwa Mgeni rasmi kwenye Maafali ya Chaso Karimjii Hall pia Atazungumza na Watanzania wote.
IMG-20160617-WA0085.jpg
 
Ni waziri mkuu aliyejiuzuru kutokana na kuhusika kwenye kashifa ya Richmond iliyohusisha wizi wa mabilioni ya pesa.
Pia ni waziri mkuu ambaye licha kwamba mnamtaja sana kwa ufisadi lakini bado tingatinga lenu limekwama kumtumbua na kamwe haliwezi maana linajua kwamba uongo ni mwepesi kushinda ukweli kwani hakuna mwizi wa kugombea urais nchi hii akapigiwa kura 6,000,000+
 
Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kesho Jumamosi anatarajiwa kulitikisa Taifa.

Ni katika mahafali ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali wa mkoa mkoa wa Da es Salaam ambao ni wanachama wa Chadema chini ya Umoja wao ujulikanao kama CHASO.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chadema atakuwa mgeni Rasmi katika shughuli hiyo na anatarajiwa kutoa hotuba mbele ya halaiki hiyo.

Edward Lowassa mwenye mvuto mkubwa katika Taifa hili na mwenye wafuasi kila pembe ya nchi amekuwa akipamba na kuteka vyombo vyote vya habari pale anafungua mdomo wake kutamka jambo lolote.

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanabashiri hotuba ya Lowassa itajikita katika mambo kadhaa ikiwamo vurugu zinazoendelea ndani ya bunge la Tanzania kwa kufukuza hovyo wabunge wa upinzani.Pia anatarajiwa kuzungumzia upigaji marufuku wa shughuli zozote za kisiasa kwa vyama vya upinzani na pia yanayoendelea kutokea Zanzibar.

Maandalizi yote yameshakamilika na shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 4 asubuhi.

Kutokana idadi kubwa sana ya waandishi wa habari waliothibitisha kushiriki wanaombwa ifikapo saa 2 asubuhi wawe wameshakaa kwenye nafasi zao.
 
Ni siku ambayo ilikuwa inasubiri kwa hamu kipenzi cha watanzania Mh Edward Lowasa amekaribishwa kwa heshima kubwa kwenye tukio la kihistoria kukabathi vyeti kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali wakiwepo wanachama wa CHASE mnakaribishwa sana ukumbini karimjee
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom