Mhe. Kuyeko Atembelea Kata ya Ilala

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala mhe. Charles Kuyeko amefanya ziara ya ghafla katika Kata ya Ilala, mtaa wa sharifu shamba. Lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea adha kubwa inayowakabiri wakaazi wa eneo hilo, ambayo ni kulika/kumomonyoka kwa kuta za mto unaotenganisha Kata ya Ilala na Kata ya Buguruni.

Adha hiyo imesababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam. Kumomonyoka kwa kuta za MTO huo kumeathiri vibaya nyumba za wakaazi wa eneo hilo baadhi ya nyumba zimeanguka na zingine kupata nyufa zilizo sababisha wananchi kuzihama nyumba hizo.

Mbali na madhara ya mto huo, wananchi pia wamewalalamikia wamiliki wa guest katika eneo hilo kwa kutiririsha Maji machafu na kutupa taka ngumu katika mto huo na kutishia afya za wakaazi wa eneo hilo.

Aidha baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamekuwa na tabia ya kutoa takataka majumbani mwao na kutupa kwenye mto na kusababisha Maji kutotiririka vizuri.

Mhe. Kuyeko akizungumza na wananchi wa eneo hilo,aliwapa pole kutokana na adha inayowakabili wananchi hao na amewaomba kuwa na subira wakati serikali ikishughulikia kero hiyo ambapo amewaahidi kuwa yeye na wakuu wa idara zinazohusika na suala hilo watalifanyia kazi ndani ya muda mfupi, ambapo aliwaagiza wakuu wa Idara za ujenzi, Idara ya mazingira, na mipango miji kufika eneo la tukio na kutatua kero inayowakabiri wananchi hao Mara moja.

Mhe. Kuyeko amewataka kuacha mara moja wale wote wanaochafua mto huo na mazingira kwa ujumla.

Kupitia ziara hiyo Mhe. Kuyeko amewaomba wananchi wa manispaa ya ilala kujenga tabia ya kupenda kutunza mazingira yao, kuanzia majumbani mwao na nje ya nyumba zao.

Katika ziara hiyo Mhe. Kuyeko aliongozana na Diwani wa Kata ya Ilala Mhe. Kimji na maafisa mbalimbali kutoka Manispaa ya Ilala na Kata ya Ilala. Wananchi wa Kata ya Ilala hususani mtaa wa sharifu shamba wamemshukru Mstahiki Meya, Mhe. Kuyeko kwa kuweza kufika eneo hilo na kwamba wanaamini atawasaidia kuondokana na adha hiyo. Wananchi hao pia walimtakia mhe. Kuyeko afya njema na maisha marefu na Mwenyezi Mungu amjaalie hekima na busara katika uongozi wake.

Imetolewa Leo tarehe 25/04/2016
Na. Alex Massaba,
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala.
0656 568256.
 

Attachments

  • IMG-20160425-WA0035.jpg
    IMG-20160425-WA0035.jpg
    131 KB · Views: 46
  • IMG-20160425-WA0034.jpg
    IMG-20160425-WA0034.jpg
    119.4 KB · Views: 57
  • IMG-20160425-WA0032.jpg
    IMG-20160425-WA0032.jpg
    117.1 KB · Views: 51
Back
Top Bottom