Mhe. Jerry Silaa tafadhali zingatia uzalendo kwanza


M

miss bobo

New Member
Joined
Jun 28, 2012
Messages
2
Likes
0
Points
0
M

miss bobo

New Member
Joined Jun 28, 2012
2 0 0

Wananchi wa eneo la Ulongoni A - Ukonga/Gongo la mboto hatuna barabara kabisa,yaani mvua ikinyeesha ni balaa tupu.Kipande cha hiyo barabara ile inayounga na daraja la msimbazi ni kidogo sana na kitatumia pesa ndogo kukarabati,lakini kinacho sikitisha halmashauri imeshindwa kabisa kukitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Kinacho nishangaza mhe. umetumia hela nyingi kutengeneza billboards kadhaa kwa ajili ya kumpongeza Rais kuteuliwa kuwa m/kiti wa CCM.Mimi binafsi naona kitendo ulichokifanya ni cha kibinafsi sana. Umeacha wakazi wengi waumie ili umfurahishe mtu mmoja.Kumbuka kwamba wewe ulichaguliwa kwa imani kubwa ya wananchii na kwamba utawatumikia wananchi na sio kukitumikia chama kwa hela ya wananchi.

Inaumiza sana kuona viongozi wa nchi hamna TOUCH/HISIA kabisa kwa wananchi wenu.
Nina uhakika billboard moja ingejaza ile barabara kifusi cha mawe na watu tungepita kwa usalama.

Ndugu zangu viongozi,matatizo ya wananchi ni meng sana,kama hamlijui hilo.Kwa hiyo mtusaidie kupunguza baadhi ya kero ili nasi tuweze kuishi muda mrefu japo kwa hali ya unyonge.

Mungu awaguse viongozi wote,muweze kulitumikia Taifa na sio nyinyi wenyewe au chama chenu au familia zenu.

 
POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
6,691
Likes
17
Points
135
POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
6,691 17 135
Huyu dogo nae analewa sifa sana...Sijui kwa nini vijana wa magamba wanalewaga masifa na kujisahau,
Meya Jerry kaweka mabango ya picha zake sehemu mbalimbali za Ilala, sijaelewa ni kwa nini?:bowl:
 

Forum statistics

Threads 1,236,170
Members 475,019
Posts 29,248,645