Mhe Gimbi Masaba (MB) amjibu Rais Magufuli

Alice Gisa

Senior Member
Sep 6, 2014
172
417
Baada ya Rais Magufuli kutotekeleza ahadi yake ya kutoa Milion 50 kwa kila kijiji aliyoahidi wakati wa kampeni za urais 2015. Mhe Gimbi Masaba (MB vitimaalum CHADEMA mkoa wa SIMIYU) amefanya jambo la kipekee kwa kuanza kutoa tsh 50,000/= kwa kila kijiji katika wilaya ya Itilima iliyopo mkoani Simiyu. Hadi sasa ameishatoa kiasi hicho cha pesa kwa miezi mitatu mfululizo.

Mhe Gimbi amesema yeye si mtu wa maneno mengi bali vitendo zaidi, Amesema lengo la kutoa pesa hizo ni kuwezesha halmashauri za vijiji katika mipango yao ya maendeleo. Alisisitiza ya kuwa zoezi hilo ni endelevu kwa kipindi chote cha ubunge wake.

Ni wakati wanasiasa wetu hasa Rais wetu Kipenzi kutekeleza yale aliyoahidi wakati wa kampeni zake. Naomba nitumie jukwaa hili kumkumbusha kwa uchache tu yale ninayokumbuka aliyotuahidi.

1. Tanzania ya viwanda.

2. Milion Hamsini kwa kila kata (bibi yangu anazisubiri kwa hamu kubwa)

Asantee.
 
Kwani si siku zote mnasemaga kuwa wabunge wa upinzani kazi yenu si kuleta maendeleo bali kuishauri na kuisimamia serikali? Nini tena hiki?
 
CCM mnamaneno mingi mama waimbaji WA East African Melody. vipi Tanzania ya viwanda imefikia wapi? Haha tatizo maonooooooo noooo
 
Kwani si siku zote mnasemaga kuwa wabunge wa upinzani kazi yenu si kuleta maendeleo bali kuishauri na kuisimamia serikali? Nini tena hiki?
Sio wa upinzani tu, wabunge wote hawalazimiki kutoa fedha zao kwa ajili ya huduma za jamii maeneo yao, hiyo ni kazi ya serikali. Kazi yao ni kuchochea maendeleo kwa kuibana serikali itekeleze wajibu wake kwani serikali ndiyo inayokusanya kodi zote nchini. Kama mbunge anatoa fedha zake mfukoni (sizungumzii za mfuko wa jimbo), basi awe anaungana na wananchi kuchangia juhudi zao za kujikwamua na jambo fulani la dharula linalotokea mara moja moja, kama vile janga la mafuriko, njaa nk. ambapo serikali inawachelewesha, lakini sio huduma endelevu kama kulipa mishahara wafanyakazi, kuendesha miradi ya umeme, kujenga barabara nk
 
Baada ya Rais Magufuli kutotekeleza ahadi yake ya kutoa Milion 50 kwa kila kijiji aliyoahidi wakati wa kampeni za urais 2015. Mhe Gimbi Masaba (MB vitimaalum CHADEMA mkoa wa SIMIYU) amefanya jambo la kipekee kwa kuanza kutoa tsh 50,000/= kwa kila kijiji katika wilaya ya Itilima iliyopo mkoani Simiyu. Hadi sasa ameishatoa kiasi hicho cha pesa kwa miezi mitatu mfululizo.

Mhe Gimbi amesema yeye si mtu wa maneno mengi bali vitendo zaidi, Amesema lengo la kutoa pesa hizo ni kuwezesha halmashauri za vijiji katika mipango yao ya maendeleo. Alisisitiza ya kuwa zoezi hilo ni endelevu kwa kipindi chote cha ubunge wake.

Ni wakati wanasiasa wetu hasa Rais wetu Kipenzi kutekeleza yale aliyoahidi wakati wa kampeni zake. Naomba nitumie jukwaa hili kumkumbusha kwa uchache tu yale ninayokumbuka aliyotuahidi.

1. Tanzania ya viwanda.

2. Milion Hamsini kwa kila kata (bibi yangu anazisubiri kwa hamu kubwa)

Asantee.
Hivi huyo mbunge anajua hata budget inapitishwa na kuanza kutekelezwa lini? Kweli ndio maana ameitwa Gimbi!
 
Eti buku 50?? Hapo ndo kikomo cha ubunifu kinapoishia kwa vijana wa UKAWA?
Hiyo Ni initiative nzuri. Ukitaka kujua hiyo Pesa so haba kawasikilize Wabunge WA CCM wakipinga kukatwa 05% ya kodi.

Hongera Mhe Gimbi Masaba. Usife moyo. Andaa kazi zingine Kubwa na ubunifu zaidi.
 
Ahadi zilikua nyingi kioindi kile cha kampeni....
KUNA AHADI ILITOLEWA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI MASHAMBA YA UBUYU DODOMA,ahadi hiyo itaanza kutekelezwa lini?
 
Na Mie nakumbuka ingine... Kujenga daraja mbadala WA kivuko Kati ya Mza na Sengelema
 
Sitaki kuhoji wala kuuliza hela zimepatikana vipi au zimetoka wapi hadi kumfikia mbunge na kutoa kwenye vijiji, hilo watajua wenyewe, ninachoangalia kama ni kweli hela zimewafikia wananchi wa kawaida wa hali ya chini KAMA NI KWELI basi hongera zake kiasi mana elfu 50 si ya kutegemea kijiji kizima ila kwa kuanzia, kidogo sana angalau bila kujali katoka chama gani hata kama ni kile cha Mwendokasi chenye miteru mingi.
 
Back
Top Bottom