Mhasibu TRA kortini kwa hasara ya bil 29/-

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
WATU watatu akiwemo Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Reuben Mwakasa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 29.

Mbali na Mwakasa ambaye ni mkazi wa Msagara wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, wengine ni Meneja wa Tema Enterprises, Ephraim Magete, mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na mfanyabiashara Elizabeth Massawe, naye mkazi wa Makongo Juu jijini Dar es Salaam.

Akiwasomea mashitaka, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo, kati ya Novemba 22, 2013 na Agosti 21, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali wilaya za Temeke na Ilala, Dar es Salaam.

Nchimbi alidai washitakiwa hao kwa pamoja kwa vitendo vyao waliisababishia TRA hasara ya kiasi Sh bilioni 29 kwa kukwepa kulipa kodi kwenye mamlaka hiyo. Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Nchimbi alidai upelelezi haujakamilika na kuomba shauri hilo kuahirishwa hadi tarehe nyingine kwa kutajwa. Hakimu Mwijage aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa walipelekwa rumande.
 
tz raha sana ...kila kesi upelelezi haujakamilika halafu mnawapeleka mahakamani...then mnawaachia huru...
 
Alafu wanapelekwa mahakamani isiyo na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, sasa sijui inakuwaje hivi na mahala sahihi pako
 
MAHAKAMA 22.jpg

​
WATU watatu, akiwamo Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Reuben Mwakasa wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia TRA hasara ya Sh. bilioni 29.

Mbali na Mwakasa ambaye ni mkazi wa Msagara, Moshi mkoani Kilimanjaro, washtakiwa wengine ni Meneja wa kampuni ya Tema Enterprises, Ephraim Magete, mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na mfanyabiashara Elizabeth Massawe, mkazi wa Makongo Juu jijini pia.

Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumatano na kusomewa shtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage.

Akiwasomea shtaka lao, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai washtakiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Novemba 22, 2013 na Agosti 21, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Temeke na Ilala.

Nchimbi alidai washtakiwa hao kwa pamoja kwa vitendo vyao waliisababishia TRA hasara ya kiasi hicho kwa kukwepa kulipa kodi kwenye mamlaka hiyo.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Nchimbi alidai upelelezi haujakamilika na kuomba shauri hilo kuahirishwa hadi tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa walipelekwa rumande na kesi imepangwa kutajwa Septemba 29, mwaka huu.

Chanzo: Nipashe
 
Aisee,
Hukawii kusikia DPP hana nia ya kuendelea na kesi hivyo shauri limefutwa
 
Mnakujaga kwa mbwembwe halafu DPP anaamua kusema

SINA NIA YA KUENDELEA NA KESI
 
Mchanga kutuhumiwa Wizi sio Breaking news Kama Mzaramo kusutwa kwa Umbea!
 
WATU watatu akiwemo Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Reuben Mwakasa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 29.

Mbali na Mwakasa ambaye ni mkazi wa Msagara wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, wengine ni Meneja wa Tema Enterprises, Ephraim Magete, mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na mfanyabiashara Elizabeth Massawe, naye mkazi wa Makongo Juu jijini Dar es Salaam.

Akiwasomea mashitaka, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo, kati ya Novemba 22, 2013 na Agosti 21, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali wilaya za Temeke na Ilala, Dar es Salaam.

Nchimbi alidai washitakiwa hao kwa pamoja kwa vitendo vyao waliisababishia TRA hasara ya kiasi Sh bilioni 29 kwa kukwepa kulipa kodi kwenye mamlaka hiyo. Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Nchimbi alidai upelelezi haujakamilika na kuomba shauri hilo kuahirishwa hadi tarehe nyingine kwa kutajwa. Hakimu Mwijage aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa walipelekwa rumande.
 
Hizi mshakama nazo huwaga njinga sana, eti hawakutakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo!! Sasa kama hamna uwezo kwa nini unaruhusu kesi ifunguliwe hapo? Mimi huwa siwaelewi!!
 
Back
Top Bottom