MHARIRI: Jeshi la Polisi linakabiliwa na swali jepesi kwamba katika utumishi wake linamtumikia nani?

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,903
4,051
MAONI YA MHARIRI: KWA HALI ILIVYOFIKIA POLISI WATOE KAULI INAYOELEWEKA
*** Jeshi la Polisi linakabiliwa na swali jepesi kwamba katika utumishi wake linamtumikia nani? Majibu ya swali hili yatawasaidia wananchi kujua kwanini limekuwa likijichanganya linapotoa sababu za kufuta mikutano ya vyama vya siasa.
Katiba ndiyo inatoa haki na uhuru wa wananchi kujumuika bila kuvunja sheria. Ibara ya 18 ya Katiba Sehemu ya (1) inasema bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Sehemu ya (2) inasema kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.
Mbali ya Ibara hiyo ya 18 ya Katiba, sura ya 258 ya Sheria ya Vyama vya Siasa sehemu ya IV inatoa haki kwa chama chochote cha siasa kuandaa mkutano au maandamano. Ibara ya 11 (1) inasema chama chochote chenye usajili wa muda au wa kudumu; (a) kinaruhusiwa kuandaa mikutano yake eneo lolote katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kujitangaza au kutafuta wanachama baada ya kuwapa taarifa polisi wa eneo husika; (b) kinastahili kupewa kinga na msaada wa ulinzi ili kiweze kufanya mkutano wake kwa amani.
http://www.mwananchi.co.tz/Makala/
Kwa-hali-ilivyofikia-polisi-watoe-kauli-inayoeleweka/-/1597592/3284954/-/tf8egf/-/index.html
 
Soma hiyo chini juu ya Jeshi la Polisi kutoka Tovuti ya Serikali;

Jeshi la Polisi






Jeshi hili ni chombo cha muungano na kina mamlaka nchini Tanzania kote na kuundwa kwake huko kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977. Jeshi la Polisi limeundwa chini ya kifungu cha 3, cha sheria ya Jeshi la Polisi, Sura ya 322 ya Sheria za Tanzania kwa ajili ya kulinda amani, kuwapo kwa utawala wa sheria na ufuatiliaji wa utulivu, kuzuia na kubaini uhalifu, kuwakamata na kuwalinda wahalifu na kulinda mali ya nchini Tanzania. Jeshi linalenga kuhakikisha kuwapo kwa ulinzi na usalama wa watu na mali kupitia utunzaji wa amani, kuwapo kwa utawala wa sheria na ufuatiliaji wa utulivu, kuzuia na kubaini uhalifu, kuwakamata na kuwalinda wahalifu na kulinda mali ya Tanzania.

Dhima

Dhima ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha usalama wa raia, ulinzi na kinga ya maisha na mali ya wakazi wote wa jamii yetu, kuratibu na kudhibiti mtiririko wa magari ili kuwezesha nyendo za watu na bidhaa ndani ya miji yetu na kupunguza athari ya uhalifu kwa wakazi wa jamii kupitia upelelezi, kukamata na kubaini watu waliohusika na makosa ya jinai.

Dira

Kuwa na polisi jamii wenye utaalamu, wa kisasa watakaosaidia utunzaji wa amani na utulivu kwa kupunguza matukio ya uhalifu na hofu ya uhalifu; kusimamia haki, utawala wa sheria na utawala bora na usalama wa raia nchini. Jeshi la Polisi lililorekebishwa lazima likubalike na kuaminika na jamii, kutambuliwa kutokana na ushughulikiaji wake wa kitaalamu kwenye uhalifu na matukio katika matumizi ya vipaji vya kisasa, teknolojia na zana,

Maadili ya Msingi ni Utaalamu, Kutii maadili, Kumjali mteja, Uwajibikaji na utimizaji wajibu, Ushirikiano wa pamoja, Kutokuwa na upendeleo, Wajibu katika jamii, Uaminifu, Heshima, Utiifu, Utii wa Sheria na Kanuni, Kuwa tayari kutenda, Kujiamini na kutunza
 
Back
Top Bottom