GE2025 Mhandisi Robert Gabriel achukua fomu kugombe ubunge Geita Mjini

GE2025 Mhandisi Robert Gabriel achukua fomu kugombe ubunge Geita Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mapema leo Juni 28, 2025 aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa katika Mikoa ya Geita, Mara na Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, amefika Ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Geita na kuchukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Geita Mjini katika uchaguzi wa mwaka 2025.
Screenshot 2025-06-28 163516.png

Injinia Gabriel ambaye siku zote amesifika kwa kujitoa katika kazi na kuacha alama kwa Wananchi katika Wilaya na Mikoa alikohudumu, kabla ya kushika nyadhifa za Ukuu wa Mkoa aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga mwaka 2016 ambapo mwaka 2017 alipandishwa cheo na Hayati Magufuli na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita alikohudumu kuanzia November 2017 hadi May 2021 na kisha katika awamu ya sita chini ya Rais Samia akahamishiwa katika Mikoa ya Mara na Mwanza.
Screenshot 2025-06-28 163504.png

Chanzo: MillardAyo
 
Back
Top Bottom