Mhadhiri afumua madudud vyuo vikuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhadhiri afumua madudud vyuo vikuu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by bizzare, Sep 6, 2012.

 1. b

  bizzare Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 25, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="width: 100%, bgcolor: transparent"] Mhadhiri afumua madudu vyuo vikuu
  [/TD]
  [TD="width: 100%, bgcolor: transparent"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"] Tuesday, 04 September 2012 07:08
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Florence Majani
  WAKATI Serikali na wadau wa elimu nchini wakifanya jitihada ya kuongeza idadi ya wahitimu wa shahada huku kampuni zikitoa vipaumbele kwa wenye sifa hizo, imebainika kuwa asilimia 80 ya shahada hizo si halali. W

  alakini wa shahada hizo, umebainika kupitia utafiti uliofanywa na Dk Eliamani Sedoyeka wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar es Salaam. Katika utafiti huo, mhadhiri huyo, amebaini kuwa wahitimu wengi ama wameiba au wamenakili tafiti zao za mwisho kutoka katika tafiti za watu wengine au kwenye mitandao. Mtaalamu huyo wa Kitengo cha Hesabu na Mfumo wa Mawasiliano, alisema tatizo hilo ni kubwa na linaendelea kukua siku hadi siku. Kwa mujibu wa Dk Sedoyeka, baadhi ya wahitimu wanafanyiwa tatizo hizo na kampuni na wahadhiri wa vyuo. Alisema wengine wamekuwa wakipata alama za juu kwa kuibia kwenye mitihani yao.

  Dk Sedoyeka ambaye amefanya utafiti kuhusu sababu za wanafunzi kunakili shahada na kuibia katika mitihani yao, alisema asilimia 80 ya shahada hasa za kwanza pili na shahada za juu zina walakini mkubwa. Alisema tatizo hilo limechangiwa na kukosekana kwa uwiano kati ya idadi kubwa ya wasomi na maendeleo ya nchi. Mhadhiri huyo alisema Serikali inawekeza katika kuzalisha wasomi wengi kwa kutoa mikopo ya elimu ya juu, bila kuangalia ubora na matokeo ya wasomi hao katika maendeleo.

  “Serikali inatakiwa iliangalie suala hili kwa upana kwa sababu tutaendelea kuzalisha wasomi wengi wasiokuwa na tija kwa maendeleo ya taifa,” alisema Dk Sedoyeka. Sababu za wanafunzi kununua au kunakili shahada? Dk Sedoyeka alisema sababu zinazochochea tatizo hili ni wanafunzi kutojituma, matatizo ya kisaikolojia na upungufu wa wahadhiri. Alisema wahadhiri wachache wanaokuwepo vyuoni, wanasongwa na kazi nyingi na hivyo kushindwa kuwasimamia vyema wanafunzi.

  “Mwanafunzi anapofanya ‘research yake’ tunategemea atumie ujuzi wake aliojifunza kwa miaka mitatu au minne. ‘Research anayoifanya itatuonyesha kama yuko tayari kufanya kazi au la,” alisema Dk Sedoyeka. “Anasema mwanafunzi anaponunua ‘research’ au kufanyiwa au kuiba ya mtu hawezi kuwa nguvu kazi yenye tija,” alisisitiza. Alisema kingine kinachochangia kuwapo kwa shahada mbovu i ni wahadhiri wenyewe. Dk Sedoyeka alisema wingi wa vyuo umesababisha kuajiriwa kwa wahadhiri ambao baadhi yao hawana ujuzi wa kina katika kuwasimamia wanafunzi kwenye tafiti zao.

  “Huwezi kumsimamia mwanafunzi katika ‘dissertation’ wakati wewe mwenyewe hukuifanya vyema na hufanyi tafiti yeyote katika maisha yako,” alisema Anasema kinachosababisha shahada nyingi kuwa feki ni kitendo cha kununua au kuiga kugeuka utamaduni wa watanzania.

  “Aghalabu mwanafunzi anasema, kama wengine wanaiba, wananunua na wanaiga, kwa nini na mimi nisifanye hivyo, Kwa kifupi mfumo umeoza,” alisema. Anasema hata kama chuo kinahitaji wanafunzi wengi wafaulu, lakini taaluma inabaki kuwa taaluma na wanachuo wanatakiwa wafaulu kwa uhakika na si kuwalipua kisha kuwatupa duniani wakiwa hawawezi kufanya lolote. Jambo lingine linaongeza kasi ya shahada feki, ni mabadiliko ya siku za karibuni ambapo shahada za juu zinakuwa kigezo cha kupata ajira. Dk Sedoyeka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Usimamizi wa Takwimu, Data na Mipango alisema kinachosababisha tatizo hili kukua kwa kasi ni ari ya vijana kupata elimu kunakoambatana na sheria dhaifu.

  “Katika nchi zilizoendelea, hata kama ni mbunge, waziri au mwenye cheo kikubwa akibainika kuwa matokeo yake ya kitaaluma yana walakini anaachia ngazi,” alisema.

  Anasema tafiti za mwisho za mwanafunzi zina umuhimu mkubwa kwani anapofanya tafiti hizo anajengwa katika kuibua tatizo, kulidhibiti na kulitafutia ufumbuzi. . Mhadhiri huyo anasema aliufanya utafiti wake kuanzia Juni 2011 katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee na kukamilisha sehemu ya kwanza.

  Sasa yupo katika hatua ya pili itakayoangalia tatizo hilo kisaikolojia na kitabia. Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Tumaini Dare s Salaam, Godwin Gondwe alisema anakubaliana na utafiti wa Dk Sedoyeka na kwamba hiyo ni moja ya changamoto katika sekta ya elimu nchini. Gondwe ambaye ni Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano ya Umma alisema chanzo kikuu ni mfumo mbovu wa elimu tangu awali ambapo wanafunzi wengi wanasumbuliwa na lugha ya kiingereza.

  Alisema sababu nyingine ni wahadhiri kuwasimamia wanafunzi wengi katika tafiti zao, jambo ambalo wakati mwingine linachangia wanafunzi kufanya vibaya. Mhadhiri huyo alisema Tanzania haina budi kuwa sera ya elimu itakayosimamia ubora na mwelekeo wa elimu nchini, ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojia katika kuzipima tafiti za wanafunzi. “Tutunge sera ambazo zitasimamia sekta ya elimu kuanzia ngazi ya chini kabisa, ili wahitimu wawe na tija,” alisema Gondwe.

  Hata hivyo Gondwe alisema pamoja na utafiti huo kuonyesha asilimia kubwa ya shahada zina walakini, bado Tanzania ina wasomi ambao ni lulu katika nchi za jirani, kama Kenya, Rwanda na Burundi.

  Aliitaka serikali kuwekeza katika elimu ikiwemo kuweka fungu la kutosha kwa ajili ya kufanya tafiti. Dk Nandera Mhando, Mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Sosholojia alisema amekutana na changamoto za wanafunzi kunakili tafiti zao mara kwa mara. Alitoa mfano kuwa mwaka jana aliwapa sifuri wanafunzi karibu kumi ambao walinakili tafiti zao.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa, alipotafutwa kwa njia ya simu hakuweza kupokea simu yake huku Naibu wake, Philip Mulugo akisema kuwa yupo mkutanoni na kuwa hawezi kuzungumza kwa wakati huo.

  Utafiti uliofanywa na mwandishi ulibaini uwepo wa watu ambao hujipatia riziki kwa njia ya kuwafanyia wanavyuo tafiti. Mwandishi alizungumza na Kijana mmoja (jina linahifadhiwa),ambaye kazi yake ni kuwafanyia wanavyuo tafiti na aliahidi kuifanya tafiti hiyo kwa malipo ya shilingi laki tano kwa tafiti ya shahada ya uzamili. Kijana huyo alianza kwa kuuliza ni aina gani ya kozi, kiwango kipi yaani shahada ya kwanza au ya pili na alinitaka nimpe mada zisizopungua tatu ambazo ningependelea kuzifanyia utafiti.

  Baada ya kumtumia mada aliniuliza ni lini ninahitaji tafiti hiyo. Aidha alinisisitiza kuwa baada ya kumaliza kazi hiyo ni lazima niikariri kwa ajili ya kuitetea kwa wahadhiri kama ada ya tafiti zote zinavyofanyika vyuoni.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. b

  bizzare Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 25, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya wadau karibuni mchangie utafiti wa daktari nimependa hapo kwenye bold nafikiria alikuwa anagusia walioko karibu naye
   
 3. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa style hii tutawalaumu sana Wakenya kuchukua kazi hapa kwetu, na sisi kwao huko ni ndoto kupata kazi.
   
 4. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,065
  Trophy Points: 280
  Huu ni ukweli mtupu na TCU badala ya kusimamia ubora wa elimu unaotolewa na vyuo vikuu wao ndio wanajikita kwenye kufanya selection matokeo yake mwanafunzi yupo Arusha kuna course ambayo ameiomba inapatikana Tumaini - Arusha ambapo ange-save baadhi ya gharama kutokana na kuwa jirani na eneo alilokulia anapelekwa RUCO Iringa matokeo yake maisha yanakuwa magumu huko na kipindi chote alichokaa chuo anakuwa ni mtu wa mawazo, vyuo vilitakiwa vipewe hadhi kidogo kidogo kama walivyofanya mzumbe, muhimbili, Ardhi University, CDTI na ambavyo vimekuwa vikitoa stashahada ya juu / advanced diploma kwa muda mrefu tofauti na sasa watu wanaibuka tu wakipata majengo wanatangaza chuo
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Kuna thread alianzisha mtu -thinly veiled though- ana solicit wateja "awafundishe" kuandika papers/ dissertations.

  Mimi hata sishangai, graduate unamwambia aandike barua hajui pa kuanzia!

  Mtu anasoma business hata components za a business plan hazielewi!

  Anasoma Accounts, hata major principles of accounting zinampiga chenga!

  Unategemea nini? Naibu Waziri wa Sayansi na Elimu ya Juu amefika hapo partly kwa kuiba mitihani, sasa hawa wengine si wanaona mfano bora ndio huo?
   
 6. b

  bizzare Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 25, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ambacho me bado sijaelewa vyuo vya bongo jamani inawezeka vipi mhadhiri msaidizi mwenye masters tu anakuwa lecturer wa darasa la masters na thesis anasimamia jamani hii ni sahii?
   
 7. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Híi ni kweli kabisa. Ndio maana ni kazi kubwa kwa mbongo kupata kazi kenya,uganda na kwengineko ila wa kenya kupata ajira hapa ni km kwao. Elimu yetu ni zima moto tokea chekechea hadi juu.
   
 8. s

  souvenir Senior Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimefurahi sana kukutana na hi mada na Daktari aliyetoa chuo alipo.jamani wadau me nilima masters IFM yani wale wanafunzi tuliokuwa nao waliomaliza hicho ni aibu tupu hadi final wanaingia na vibuti vya kufa mtu tena wanajisifia na kuwasema wale wasiotumia kweli sisi tuliotoka vyuo vikuu vingine tulikuwa tunashangaa sana .
   
 9. mnoel

  mnoel Senior Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 170
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  mtaala wetu wa elimu haujitoshelezi!
  Kwa hapa kwetu tanzania ili kusonga mbele ni lazima upate alama za juu katika mtihani!
  Hii haipimi thinking capacity of students,
  ndio maana mitihani ya form six ikikaribia wanafunzi wanaacha kujishughulisha na kusoma wanahaingaikia kutafuta mtihani maana elimu yetu haijalishi unaelewa kiasi gani bali umepata ngap!
  Ingebidi kwanza mitaala ye2 ibadilishwe kutokea primary school,, ndo tutaweza kuona mabadiliko katika vyuo na asasi nyingne 2lizo nazo
  .
   
 10. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kama ni hivyo, hiyo ni hatari sana
   
 11. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huyo mnafiki tu kwani mwenyewe kafanya nini kipyaaaaaaaaa sana? Hata wachina walianza kwa kuiga na wanaendelea kuiga lakini wako mbali sana. Angeweka yeye resechi zake alizofanya na zimenufaisha nini taifa hili.
   
 12. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hata wanaosoma huko nje mbona kama kuiga wanaiga sana tu mi nina mifano ya watu ambao walikuwa wanasoma uingereza lakini home work anaituma tz watu wanafanya wanampelekea majibu na disertation hivyo hivyo, tena huku nje ndo hatari sana na ikiwezeza ikawa zaidi kuliko hata tanzania. Asikudanganye kuiga kupo sana tu, kama mnabisha mi nitawatumia na sample za paper ambazo watu wameiga na wengine wamebadilisha lugha kwa kimalasia, singapore, kichna nk. Elimu ya sasa ni ya kuiga na kumodify kidogo pale alipoishia mwenzako.

  CHINA BADO WANAIGA MPAKA LEO lakini wako mbali kielimu na kitechnologia kwa hiyo tatizo sio kuiga tatizo ni sera ya nchi.
   
 13. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kaka hiyo ni kasumba tu hamna tofauti kubwa sana kati ya bongo na kenya ama uganda. Hakuna cha ziada walicho nacho zaidi ya kingereza basi lakini kitaaluma watz tunatisha amini usiamini.
   
 14. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kaka hilo ni tatizo la mtu mwenyewe maana siku hizi kumekuwa na katabia kwamba kila mtu kusoma hata wale walioshindikana (mapumba) tunao wafahamu. Ulipoanza mpango huu wa vyuo vingivingi hayo matatizo ndo yameanza kujitokeza na vyuo vingi viko kibiashaza zaidi lkn hata wanafunzi wenyewe wawapo vyuoni hawajishughulishi. Usitegemee kila kitu atakupa mwalimu darasani inatakiwa wewe mwenyewe ndo uwe unashughulika. Watz wengi tunapenda tu kuadika CV zetu kwa fb wakati hamna kitu. Siku hizi kuna vyou vingi sana vya ajabu utasikia Kampala International University, hiki nacho cho kweli? Kuna mwalimu alikuwa anafundisha pale yahani ni ziro kabisaaaaaaaaa. Serikali iangalie upya sera ya elimu na pia watu wengi wanaenda kusoma ili kuongeza vyeo na mishahara.
   
 15. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tusilaumu tulitaka wenyewe vyuo viwe vingi pasipo na malengo sasa hayo ndo tunayaona. Zamani palipokuwa na UDSM, SUA, mambo hayakuwa hivyo na ndio maana siku hizi hata madr nao eti wanaenda kusoma BMA
   
 16. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sedoyeka nae bwana, mbona hata yeye kafanya advanced diploma then hapo hapo akafanya mastaz halaf PhD ina maana inaruhusiwa kuwa na advanced diploma then ukafanya mastaz
   
 17. toto zuli

  toto zuli Senior Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 20, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  hebu rudia tenaaaaaaaaa
   
 18. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145

  acha uongo . na kama hujui uliza . mwanafunzi aliyemaliza university kenya huwezi kumfananisha wa tanzania hata kidogo. na wakikutana kwenye interview au kazini ndio aibu kabisaaaa. yaani huyu wa tanzania mwenye degree ya bongo anakuwa kama mwanafunzi wa primary tu wa kenya. mwanafunzi kamaliza degree UDSM hata kujieleza haweza je anaweza kweli kupanga business plan ya kampuni yenge management ya watu wa mataifa tofauti. au angalia bunge na sikiliza bunge la kenya hivi mbunge anaweza kufanana kimawazo au akili kama JOSEPH MBILINYI ? unaambiwa rais wa RWANDA mheshimiwa KAGAME ana diploma je unaweza kumfananisha na rais wenu anayeitwa dokta ? au dokta wa kenya unaweza kumhananisha na ma dokta wetu eti dokta JOHN KOMBA , dokta NCHIMBI etc . hayo ndio matokeo ya elimu mbovu, nadhani hata ulisikia kuhusu wale wagombea ubunge wetu wa africa mashariki ambao hata kujieleza english hawawezi. na mfano wa mwisho angalia hao wanautaka kugombea urais uchaguzi ujao kina EDWARD LOWASA , MEMBE ,MBOWE etc . je unaweza kufananisha na nchi gani duniani???
   
 19. Geezzle

  Geezzle JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 835
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kaka nna mashaka na thinking capacit yako!wachina wanafanya k2 kiitwacho 'Immitation'co kucopy na kupaste km cc,afu ulvo jinga,unatetea m2 kununua research!unatia HASIRA!
   
 20. K

  Kiny JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  umenena mkuu kama kuiga kupo dunia nzima hata ila watu wamezoea kuipondea tz china vitu vyao ving hawagundui wenyewe ila ni kuiga kuiga huyo prof afanye utafiti wa kidunia ahache kuponda sekta ya elimu tz tu.
   
Loading...