Tunaweza kumchukia Zitto, lakini kuna ukweli mmoja ambao hatuwezi kuufuta. Huyu ni kijana mwenye kiu ya kujua mambo, na hii imemfanya kuwa mtu mwenye weledi wa juu. Binafsi nilikuwa naitilia shaka sana sera ya majimbo kwa kuwa nilikuwa sijapata ufafanuzi wake tangu ilipoanza kunadiwa na Mbowe kwenye kampeni za 2005. Baada ya Zitto kuielezea kwa ufasaha, nami nitakuwa wakili mzuri wa sera hiyo. Wito wangu kwa Zitto (Mmoja wa wanasiasa mahiri wachache) ni kuendelea kupigania haki ili kujenga zaidi imani kwa wananchi. Hayo ya urais, kama alivyosema mwenyewe, muda wake ukifika yatapatikana.