Mh. Waitara umetusaliti Mara mbili

Mh. Waitara umetusaliti Mara mbili

BOB LUSE

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
3,760
Reaction score
3,270
Jimbo la Ukonga limeathirika sana na Mvua zinazoendelea.

Mbunge wetu hajafika kuona adha zetu.
Ulituaminisha kuwa ulikoenda ndio kuna utatuzi wa kero zetu za Barabara kumbe ulijari Maslahi yako.

Serikali Sikivu imegeuka kuwa serikali kiziwi! Mtavuna mnachokipanda karibuni malipo ni hapahapa Duniani.

Huku Maeneo ya Mwanagati,Magore,kivule,Mkolemba ukiwa na Mgonjwa anayehitaji Matibabu katika Hospitali za rufaa maisha yake yanakuwa hatarini kwasababu Barabara zote Zimejaa Mashimo Makubwa!

Hela zilizotumika Kukununua Ukahama Chama na kupata Uwaziri kwa kurudia uchaguzi zingetosha Kuziba haya Mashimo japo kwa Kifusi.

Mchezo wa Wanasiasa ni Mauti ya wananchi!
 
Tatizo aliwadanganya kwamba eti barabara hazijengwi kwa sababu yeye yuko CDM, sasa akihamia Sisiem ndio barabara zitajengwa. Sasa naona hakuna kilichofanyika
 
Wanasiasa watu walaghai mnoo
Tatizo aliwadanganya kwamba eti barabara hazijengwi kwa sababu yeye yuko CDM, sasa akihamia Sisiem ndio barabara zitajengwa. Sasa naona hakuna kilichofanyika
 
Sijui nani aliwadanganya wadanganyika kwamba mbunge ni tajiri ama mfadhili wa kuwajengea miundombinu. Poor Tanzanians!!
Kukaa kimya ni busara pia. Kwaakili yako unaona Mbunge hahusiki na miundombinu, fungua brain
 
Kukaa kimya ni busara pia. Kwaakili yako unaona Mbunge hahusiki na miundombinu, fungua brain
Hapo ndiyo mwisho wako wa kufikiri. Mbunge anahusika vipi na miundombinu? Kwani mbunge ana fungu la kujengea miundombinu? Mbunge hana vote (fungu).
 
Aidha Suala la barabara ni karibu Maeneo Yote! Ukienda Chanika ni balaaa!
Barabara Mbovu husababisha ajali nyingi.
 
Ajiandae kuoga Mayai mabovu akija kuomba kura huku,uzuri mayai tunazalisha wenyewe hili jimbo

Uchaguzi wa 2020.. uwe wa Uhuru na Haki.. sio kutumia vyombo vya Dola na ujanja ujanja..

Tume huru na Katiba mpya.
 
Hivi siku hizi pombe ananywea wapi? Bado analewea kule Nyantira na kulala baa au amehamia pombe za Serena Hotel????
 
Serikali Sikivu imegeuka kuwa serikali kiziwi! Mtavuna mnachokipanda karibuni malipo ni hapahapa Duniani.
Hizo kauli za mfa maji wala hazistui mtu
Hata kwenye uchaguzi wa marudio mlimuambia hayo maneno huyo waitara
 
Back
Top Bottom