Mh. Samia atingisha Jimbo la Kibamba, Dar Es Salaam

Mh. Samia atingisha Jimbo la Kibamba, Dar Es Salaam

Mr Chin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
4,625
Reaction score
1,024
[h=2]MAMA SAMIA ATINGISHA JIMBO LA KIBAMBA, DAR ES SALAAM MCHANA HUU[/h]






Wananchi wakimshangilia mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suhlu Hassan alipowasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Mbezi Centre, jimbo la Kibamba wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ua CCM, Mama Samia Suluhu, akiwasalimia wananchi, alipowasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye Vwanja vya Mbezi Centre, jimbo la Kibamba, Dar es Salaam.
Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia, akiwa tayari kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo Viwanja vya Mbezi Centre, jimbo la Kibamba wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na kushoto ni Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCm jimbo la Kibamba Dk. Fenela Mkangara.
Wananchi wakimshangilia mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suhlu Hassan alipowasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Mbezi Centre, jimbo la Kibamba wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akishangaa umati wa wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Mbezi Centre, jimbo la Kibamba, wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM uliofanyika katika wilaya hiyo leo.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Lina Sanga akionyesha manjonjo yake alipotumbuiza katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia uliofanyika viwanja vya Mbezi Centre, Dar es Salaam, leo
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akiwahutubia wananchi katika mkutano wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mbezi Centre, jimbo la Kibamba wilayani humo.

Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, Angela kairuki, akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mbezi Centre, jimbo la Kibamba, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akimwelekeza jambo, Mbunge wa Afrika Mashariki Angela Kizigha, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mbezi Centre jimbo la Kibamba Dar es Salaam. Kushoto ni Mgombea Ubunge jimbo la Kibamba Dk. Fenela Mkangara
Wasanii wa bendi ya Yamoto, wakishambulia jukwaa, wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mbezi Centre, Kibamba jijini Dar es Salaam
Mama Salia akiwatuza wasanii wa bendi hiyo

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akihutuba mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya Mbezi Centre, jimbo la Kibamba Dar es Salaam
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Kibamba, Dk. Fenella Mkangara katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mbezi Centre, jimboni humo leo
 
kila nikimkumbuka Hawa Ngumbi alivyohenyeshwa na mnyika 2010sioni mahali ambapo huyu Fenela Mkangara atakapotokea huu mwaka..Mawaziri wa JK wanabahati mbaya na Mnyika
 
Huko ndio kutingisha Jimbo???? The fall is near
 
Ya moto band na Linnah wametingisha
 
Hamna Lolote,Mnyika Hana Mpinzani. Mikutano ya Campaign ya CCM, Ikiwa Pamoja Ni Huu Unaweza Kudhani Kuna Watu wengi

Waliokwenda Kumsikiliza Mgombea Kumbe Wangi Wanakwenda Kusikilza Mziki. Ni Burudani Inawakusanya Watu na wala sio Mapenzi na

Chama Cha Kijani.
 
Ha ha haaaa. Pamoja na wasanii wooote ila ni makumi ya watu tu wamehudhuria.
Ngoja wasimame chadema ndo mtaona mtingishiko
 
sisi ndo wenye jimbo lenyew la kibamba wenyew hata wawalete p square sisi mziki tutacheza ubwabwa tutakula lakin kura zoote kwa ukawa.. Hv nyie kibamba mnapajua mnapaskia yaan mnyika hana hata haja ya kupiga campaign
 
sisi ndo wenye jimbo lenyew la kibamba wenyew hata wawalete p square sisi mziki tutacheza ubwabwa tutakula lakin kura zoote kwa ukawa.. Hv nyie kibamba mnapajua mnapaskia yaan mnyika hana hata haja ya kupiga campaign

Low self-esteem
 
Nilikuwepo, wengi waliletwa na magari kutoka wilaya zote za dar es salaam, wakazi wa mbezi waliendelea na kazi zao kama kawaida
 
Masikini CCM, Ukiangalia hizo picha unaona mafuso na mabasi waliyotumia kusomba watu na kuwavalisha magwanda yao mabayaaaa!
 
11997514_10205260772823634_1056402572_n.jpg
 
Back
Top Bottom