Mh.Raisi wa JMT ndugu JPM akutana na Tucta.Je,hii ina tafsiri gan kwa wafanya kaz?

jayec

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
599
477
Rais Magufuli amekutana na viongozi wa TUCTA Ikulu DSM leo

Edwin Kamugisha TZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli, leo April 20 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano kati yake na wafanyakazi kwa manufaa ya Taifa.

Katika Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema pamoja na kuimarisha ushirikiano huo, Serikali ipo tayari kupokea maoni na ushauri wowote utakaotolewa na vyama vya wafanyakazi wenye lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kuongeza tija kazini.

Rais Magufuli amesema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi na itaendelea kuchukua hatua za kukabiliana nazo kama ambavyo imeanza kufanya hivyo.

“Nataka kuwahakikishia nyinyi viongozi wa TUCTA na wafanyakazi wote kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wafanyakazi na ipo tayari kuwapigania, jambo la msingi tutangulize maslahi ya Taifa, kawaambieni wafanyakazi wachape kazi na Serikali itawalinda”;-Rais Magufuli.

Kwa upande wao Viongozi wa TUCTA wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Tumaini Nyamhokya wamempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali yake kujenga uchumi imara, kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa Serikali, kupambana na rushwa, kuondoa watumishi hewa na kulipa madeni ya watumishi.

Viongozi hao wameahidi kushirikiana na Serikali katika kusimamia haki na wajibu wa wafanyakazi na wameomba Serikali iendelee kufanyia kazi mbalimbali ya wafanyakazi ikiwemo kuwalipa stahili zao na kuboresha mazingira ya kazi
 
Attachments

  • unnamed-1-1.jpg
    unnamed-1-1.jpg
    82.6 KB · Views: 33
Nahitaji mawazo yenu lakin matusi hayaruhusiwi wapendwa
 
Nahitaji mawazo yenu lakin matusi hayaruhusiwi wapendwa
Yaani hawakwenda na Hoja yoyote zaidi ya kupongeza ? Kuhusu Sheria ya Kitwacho FAO LA kujitoa na athari zake kwa watumishi Wa muda maalum au wanaoamua kuacha au kuachishwa kazi na Faida zake kuwa hizo fedha zaweza kuwa mtaji kama watapewa elimu hitajika hawajaliona ?

Natambua kuwa hakuna vyama huru vya wafanyakazi lakini sikutegemea kuwa hawa ni wwzembe kiasi hiki
 
Tucta wanatokota tu.
Yaani wameshindwa kumpa makavu kuwa usanii wake wa kuzuia watu kapanda madaraja na kutopata nyongeza ya mshahara vimeshusha morali ya utendaji?
Wameshindwa kumuuliza atarekebisha huo ukiukaji wa mkataba?
Poor me!
 
Lakin pengine kuna something behind ambacho n positive kwa wafanyakazi
 
Hiyo TUCTA imekua ni kikundi cha watu kisichotumia Noah kuteka haki za wafanyakaz na kuzifutika kwa danganya Toto ya kupigania haki, kiukweli ningetamani wakati ungefika kila mtumishi angelikua huru kujitoa au kubaki
 
Tucta wanatokota tu.
Yaani wameshindwa kumpa makavu kuwa usanii wake wa kuzuia watu kapanda madaraja na kutopata nyongeza ya mshahara vimeshusha morali ya utendaji?
Wameshindwa kumuuliza atarekebisha huo ukiukaji wa mkataba?
Poor me!
Teh teh ungekuwa wewe ungeweza? Ushakunywa juisi ya mkulu unaanzaje?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Teh teh ungekuwa wewe ungeweza? Ushakunywa juisi ya mkulu unaanzaje?
Sikuwa mimi ndo maana nauliza hivyo, mkuu. Mi sio mtu wa kispoti spoti, teh teh
Halafu watakuja kutuhamasisha tuende kusherehekea mei mosi.
Nawaona wafanyakazi wakiandamana kumpongeza rais kwa uongozi wake bora wakati moyoni wanaumia kwa kudhulumiwa haki zao. Utakuwa ni unafiki wa kiwango cha lami
Mi nitaugulia home tu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom