Mh.Raisi unaishi na majipu,yakamue

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,384
2,000
Tume ya maadili ya utumishi wa umma ipo chini ya ofisi ya Raisi ambapo inaongozwa na kamishna wa tume ya maadili ya viongozi wa umma

Kimuundo kunakua na makatibu wakuu wawili mmoja akihusika na viongozi wa siasa na mwingine akihusika na watumishi wa umma
Pia zimegawanywa kanda sita ili kurahisisha utendaji/usimamizi wa majukumu yao
Moja ya majukumu yao ni kuhakiki Mali za watumishi wa serikali na wanasiasa ndani ya nchi,ikiwemo rasilimali na madeni yao.Lengo kubwa ni kuwabana watu hao wawe na kipato halali/kisichotiliwa shaka.Tume hii inahakiki mali za viongozi wanapoingia katika utumishi na pale wanapotoka/kustaafu kazi zao

Kwamaelezo hayo nauliza maswali haya
.Je tume hii inatimiza majukumu yake?
.Je nilini walibaini kiongozi kutoka kwenye makundi mawili tajwa hapo juu kama mali zao sio za halali?
.Je tume hii iliyochini ya Raisi imetoa elimu kiasi gani kwa umma wa watanzania kama wafanyavyo polisi,TRA,TCRA nk?

Kwamtazamo chanya nikwamba tume hii inasaidiwa na wanasiasa kubaini wizi na ubadhirifu ndani ya serikali lakini wao bado wamelala tena fofofo.Ninasema hivyo kwani kashfa zote kubwa zinajitokeza kutokana na viongozi kutofuatiliwa mali zao kuanzia waishipo,kwenye mabenki nk.Waibuaji wa kashfa hizo wamekua wanasiasa na wala sijasikia tume ikifuatilia labda TAKUKURU angalau

.Mh.Raisi timua hao wanaitia ofisi yako doa na kulifanya taifa liwe na watumishi wanaoshindana kuiba kwakua wabanaji wamelegeza kamba au pengine nao nisehemu ya wakosaji wanashindwa kuwabana wenzao
Alamsiki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom