Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,624
- 3,652
Mkuu hongera kwa kazi ya kulitumikia taifa kwa kadri Mungu alivyo kuwezesha.Lipo tatizo ambalo linaonekana nisugu katika shule zetu ambalo ni madawati na kwashule za sekondari hutumika zaidi meza.Mh.Raisi nchi hii inao wezi wengi mno na suala hili husababishwa na wakurugenzi katika halmashauri zote nchini.Wakisaidiwa na maafisa elimu wazembe,wakurugenzi wameshindwa kusimamia fedha za walipakodi hohehahe ambapo hususan kwa shule za sekondari kila mwanafunzi anayeanza kidato cha kwanza nilazima alipie hela ya kiti na meza kwanza ndio ada na michango mengine hufuata.Sasa jambo la kushangaza ni kwamba kwa asilimia kubwa kila shule haina meza za kutosha,aliyelipia kiti na meza anakosa pakukalia,walimu wanagombea viti na wanafunzi na ajabu ni kwamba hakuna mwanafunzi anaye maliza kidato cha nne akaondoka na kiti au meza yake ila viti na meza bado wanafunzi wanagombea.Hili ni tatizo kubwa,niuzembe kwa Wakurugenzi na maafisa elimu kwani wengine hawajui hata baadhi yataasisi zilizopo kwenye halmashauri zao,naniwizi wa kutisha kwani wakuu wa shule kwa asilimia kubwa ndio mradi wao huo.Ushauri wangu,hao wakuu wa shule wachunguzwe,wabainike wezi wa hila wawajibishwe kwa kushushwa vyeo na wapelekwe mahakamani