Mh. Rais wetu, tunaomba angalia Halmashauri ya Wilaya Nsimbo-Katavi

halmashauri husika

  • jukwaa la siasa

    Votes: 0 0.0%
  • mada mchanganyiko

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    0

chengelai

Member
Feb 10, 2016
7
0
Tinashukuru sana Rais wetu kwa utendaji wako wa kazi.wakati wewe unakazana kutumbua majipu vipo vijipu chungu vingi sana hasa katika halmashauri nyingi.tunaomba uangalie kwa makini hasa halmashauri ya Nsimbo katika mkoa wa katavi.hasa kwa haya yafuatayo:

1. DED anafuja pesa za umma na kuwanyima huduma ya maji wakazi wa vijiji zaidi ya vitatu kwa kumlipa mkandarasi pesa kwa asilimia 90 wakati mradi uko tayari kwa 15% ya mradi. Mkandarasi huyo tayari hayupo site baada ya kuwa hana pesa tena baada ya wakubwa kupiga mgao. ChakushangazaTayari mkandarasi mwingine kapewa kazi. Na pesa nyingine. Pesa hizi zingeweza fanya kazi nyingine ya kuhudumia jamii. Mradi huu ni wa Maji upo kijiji cha Mwenge kata ya Nsimbo. Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo

2.Vilevile ametumia zaidi ya Tshs 800M zilizolipwa kama ushuru wa tumbaku bila CMT kujua wala kamati ya fedha uongozi na mipango kuidhinisha. Haijulikani pesa hizi zimefanya nini kwa kuwa hali ya ofisi kila siku ni madeni hadi gari yake mwenyewe kama DED ilizuiwa garage kutokana na madeni sugu ya service za magari
3.Barabara ya katumba complex imepewa wakandarasi watatu tofauti kinyume na taratibu na kuwalipa na hadi leo barabara ni kioja na haieleweki
Cha ajabu sasa PCCB mkoa nao hawana meno ya kuweza kufuatilia masuala ya maendeleo ya halmashauri husika mpaka kutengeneza hisia kwamba nao wanahusika katika matumizi haya mabaya ya pesa za umma.

Tu naomba waziri husika Wa serikali za mitaa aangalie kwa makini maswala hayo tajwa hapo juu.

Tunatambua magari ya serikali kama hamna kazi maalum siku za mwisho Wa wiki huwa ya napaki lakini kwa DED huyu yeye ni safari sumbawanga na gari hilo la walipa kodi bila jukumu maalum.
 
Kuna haja ya kufuatilia jambo hili. Msianze kuita watu wambea msije kuwa wanufaika wakubwa... Kuna madudu mengi sana katika Halmashauri nyingi. Wakurugenzi na watu wa utumishi ni Miungu wadogo.
 
Chengelai hongera kwa kuweka wazi hivyo vijipu uchungu kwenye Halmashauri ya Nsimbo,nami sijajua ule Mradi wa Maji ya Bomba na Visima pale Usevya uliishia wapi?maana matanki yalisambazwa hadi yakajitobokea menyewe chini sikuona cha Maji wala nini,Mzee Chagonja anakuja huko kama RAS,ni mfuatiliaji na mtu wa Kuchukua hatua cha msingi mpeni ushirikiano wa kutosha ili Mkoa wetu usonge mbele,miradi ikipangiwa bajeti lazima itekelezwe na wananchi wapewe taarifa za mara kwa mara
 
Inashangaza sanaa. Badala ya kujiangalia wapi mnateleza mnatajana majina humu. Hivi jumuia ya wana Katavi mna akili sawa kweli? Angalia kilichokuangusha sio ulipoangukia meen!! Natamani kujua uwiano wa kijinsia huko labda naweza pata chanzo cha mihemko inayoonekana hapa jamvini.. Simbachawene hebu chunguza hawa watu ikiwezekana timua waende maeneo mengine yawezekana wamezowea sana maeneo hayo matokeo ndio hayaa.
 
Wana Mpanda yetu ya zamani sasa hivi Katavi tulioko nje ya mpanda na ndani ya Mpanda. Tuwe makini sana kukiwa na tetesi hizi ukweli fulani huwa upo. Jiulizeni kwa nini mihemko? Kuna cha maana kikubwa kipi? Wananchi katika maeneo yetu wanapata huduma bora na kwa wakati ukilinganisha na matumizi ya pesa? Watu wanajineemesha na kuondoka sisi tumekaa kuwaacha watumishi wajiamulie ya kufanya kwa kulindana wanaoweza kulindwa.
 
Kufuatia Kuombea Mh.Rais kuangalia halmashauri husika,Watumishi wanatishiwa na kufuata a fuatwa Kwa vitisho hii Yote Ni kuwafanya wasiwe na Amani katika sehemu zao za kazi.

Na napenda kuuliza Kama ofisi ya Mkuu wa wilaya Kama haina budget ya mafuta kwani
Kila siku Mkuu wa wilaya yuko Kwa ofisi ya DED mr. Nzyungu kuomba mafuta.sasa sijui mkurugenzi anatoa wapi budget ya huyo Mkuu wa wilaya.
Vilevile ofisi ya usalama nazo huomba mafuta sasa Huu Ni matumizi mabaya ya raslimali za umma Kwa kuwa kila idara inapata ruzuku toka serikali kuu.mkurugenzi Kwa kuwa anakaimu ofisi
Hana Hakika na kazi zake hivyo hulazimika kukumbatia Mkuu aw wilaya mulele na usalama ili wamsaidie kuthibitishwa rasmi.

Mh.waziri simbachawene angalia hii kwani Utendaji unaingiliwa sana.
 
Back
Top Bottom