Mh. Rais utatumbua watu ila mwisho utajikuta na swali, je wewe?

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,605
12,230
Mh Rais umekuwa na nadharia yakutumbuwa watu kwa namna ambayo sasa inaleta maswali mengi kuliko majibu na uwenda badala yakupata mafanikio chanya unapata mafanikio hasi.

Inawezekana huu ndio utaratibu ulio uwona ni bora sana ktk serikali yako ila uwenda ukawa ndio utaratibu mbovu kabisa serikali yako na hata ukiendakwenye management ya watu aina hii ya uongoz huwa inazalisha aina yawafanyakazi waisio kuwa na uzalendo pamoja na kudumaza talent za watu wake.

Kwanza kwa aina hii ya utumbuwaji unajenga hofu ya watenguliwa na wale wanapata hizo nafasi mpya. Nahili ktk jicho la tatu ukiangalia huwezi kufanya watu kufanya kazi kwa uhuru na kujituma ktk kazi zao maana wanajuwa wakati wowote watatumbuliwa. Kwahiyo unakuta mtu anafanya kazi kwa moyo usio ma furaha na kiukweli kwa hali ilivyo kwa sasa wengi wanaogopa kufanya kazi kwa kisingizio cha kutumbuliwa.

Jambo ambalo hulikumbuki nikuwa hata wewe uliwahi kuwa waziri je kama usingevumiliwa ungefika hapo ulipo? Kiuhalisia jibu ni hapana. Sasa kile ambacho usingependa kufanyiwa usiwafanyie wengine.

Umetumbuwa sana na sasa huna wakutumbuwa unatumbuwa hata zile good cream. Unaweza kuona wewe ni mshindi na hakuna mwenye uwezo wakufanya lolote ila kumbuka unamiaka 10 ya utawala na hata kama ungefanya mazuri kiasi gani baada ya hiyo miaka lazima ukae pembeni sasa huku uraiani yapo maisha na jamii yako je watakukumbuka kwa lipi?

Pia nilazima ujifunze ktk kazi hizi yapo maisha baada ya kazi je unafikiri watu wote wanaweza kubaliana na sera zako na kama ni hapana je uwatumbuwe wote wanakupinga au iweje?

Mkuu system hii unaiongoza yapata miaka hamsin sasa ndio ile ile na wewe unamiaka kumi tu kutawala je waweza kubadilisha muuondo wa system ilio na zaid ya miaka 50 naiwe vile unataka? Jibu ni hapana na kama huwamini subiri uowone mwenyewe. Kiuhalisia kile kinaendelea ni unafiki wanakusikiliza na kukufuwata yale unataka ila baada ya miaka kumi same people watakukosoa sasa nilazima uwe mcheza mpira mwenye kujuwa funga magoli na sio kupiga chenga at the last chenga nyingi bila magoli ni bure.

Kile unakifanya toa huyu bandika huyu ni kama chenga tu kuliko cheza chenga funga magoli.

Marais waliopita walijitaidi kufunga magoli mengi. Wewe chenga nyingi mbaya zaidi chenga hizi wanachama na washabiki wa ccm hawazitaki maana mwisho wasiku sio kazi walio kutuma.

Mwisho ktk huu mchezo wakutumbuwa watu uwenda ukazaa mijitu mijizi. Mtu akijuw kesho uwenda nisiwe nakibaruwa atafanya kitu asije onekana mjinga.

Marekani namiaka zai ya mia bado upo ufisad sembuse sie kinchi cha jana?
Kama unataka kumfuwata Kagame ye west your time Warwanda wanabom ambalo any time litawalipukia sio aina yakiongoz wakumfuwata as role mode.

Kwanza wewe upo kwenye taifa la kidemocrasia. Rwanda ni mtu alie jiweka na mwisho akatengeneza system yakuwa Rais. Kiufupi pamoja na mafanikio mazuri Rwanda wanayo ila bado utawala wao na aina ya serikali ni boom laweza lipuka wakati wowote.

Anagalia Libya kwani walikosa nini sana sana walipata kila kitu ila ilifika mahali waliona bora vita kuliko one man show. Kama watanzania tunapinga one man show tunataka utaifa wetu na haki zetu zilindwe kwa kuw sisi rumechaguwa kuwa na Democrasia.

Alafu mwisho ungejiuliza jeje na mimi ningetumbuliwa na chama changu ingekuwaje? Jibu unalo na ndio maana mmebadilisha katiba ili uwe huna mpingamiz 2020. Sasa kama jibu unalo why uwatumbuwe wenzio je unafikiri watu niwajinga kiasi hiko ktk chama wawe makondoo wasije kukusulubisha?

Mimi nadhani utafakari ubadilike mkuu. Maana mwisho wasiku ccm nikufunga magoli sio chenga jambo lakukumbuka ipo siku utajieleza mbele ya kamati kuu sasa sijajuwa kama utasema majina ya watumbuliwaji kama ndio sera ya chama ulio tekeleza au sijuwi utajibu nini.
 
Upinzani kudakia tena, yale yale...

Mtazoea tu

Hapa kazi tu

Magufuli oyeeeeee
 
Aiseeee mbona wanaolalamika ni wanazi pekee. Akati akina fulani wanawajibishwa mlifurahia Sana na kushangilia, Sasa naona na washangiliaji mnaguswa Sasa kilio kinaendelea kama Kawa.
Mmewakejeli watu Sana hapa ndani kwa kuwaita ni wapinzani. Tulieni tuu kila mmoja ataguswa kwa wakati wake.

Time will tell Boss

Mungu ailaze pahala pema peponi muhanga Kabwe
 
Tuliza akili wewe mawenge usidhani jukwa hili wamerukwa na akili kama wewe.

Changia kama great thinker, hapa siyo kama kilabu cha pombe za kienyeji. Jaribu kuwa matured na siyo na fikira za kiteenager.

Mtanyooka tu

Ha ha haaa u GT kama ndio huo wako na wenzako basi mna safari ndefuuuuu.
 
Huyu mkulu mwisho atajitumbua mwenyewe. Watu hawafanyi kazi kwa ufanisi kwa kuhofia kutumbuliwa kama hio kazi haitamfurahisha mkulu. Kwasa uongozi huu, nikwamba kilakitu nachofanya kama mtumishi, mfurahishe mkulu yaani fanya anachotaka yeye hata kama unakiuka kanuni na taratibu. Dah! Sijui tutaishia wapi?
 
Kabla sijagonga Like niaminishe kama ni wewe kweli unayeandika haya , wewe ni kati ya watu wakatili sana humu jf , ukihamasisha Magufuli atende uharamia kwa watendaji wa serikali , kama nimekusingizia nirekebishwe .

Jf ni mashahidi .
 
Unaweza kuwa kweli ila kumbuka nimeamua kumuandikia ukweli. Ila yote Mungu ajuwa.
 
Unaweza kuwa kweli ila kumbuka nimeamua kumuandikia ukweli. Ila yote Mungu ajuwa.
Lakini kiwango ulichomsapoti Magufuli kinatisha ! Nakumbuka kuna uzi ulihamasisha watu " wamalizwe " ili Magufuli afanye anavyotaka , sasa leo unapoandika haya nawaza je watu wale wangemalizwa kama ulivyopendekeza ingekuwaje ?

Mungu akusamehe sana .
 
Ukiona hivyo ujue ameguswa mtu wake wa karibu
 
Upinzani kudakia tena, yale yale...

Mtazoea tu

Hapa kazi tu

Magufuli oyeeeeee
Kuna watu wanachangia humu kama Bashite. Vipi hamukuona Darasa hata moja hata kukaa tu na wazee? Ukiona huwezi kuchangia kaa kimya usiteletee U-CCM hata kwa vitu vyenye tija kwa taifa
Endeleeni kusifia kwa nyimbo za sifa na mapambio dhidi ya baba Bashite.

Nchi imetoka kwenye reli na kuingia vichakani kwa spidi ya jet.

Aiseeee mbona wanaolalamika ni wanazi pekee. Akati akina fulani wanawajibishwa mlifurahia Sana na kushangilia, Sasa naona na washangiliaji mnaguswa Sasa kilio kinaendelea kama Kawa.
Mmewakejeli watu Sana hapa ndani kwa kuwaita ni wapinzani. Tulieni tuu kila mmoja ataguswa kwa wakati wake.

Time will tell Boss

Mungu ailaze pahala pema peponi muhanga Kabwe

Tanzania ya Viwanda anyway lets see..

Mtanyooka tu

Ha ha haaa u GT kama ndio huo wako na wenzako basi mna safari ndefuuuuu.

Kwa kuwa upo hivyo, usifikirie kila mtu yupo kama wewe.

Kabla sijagonga Like niaminishe kama ni wewe kweli unayeandika haya , wewe ni kati ya watu wakatili sana humu jf , ukihamasisha Magufuli atende uharamia kwa watendaji wa serikali , kama nimekusingizia nirekebishwe .

Jf ni mashahidi .

Usikariri sio kila rais lazima akae madarakani miaka 10!! Nyerere alikaa miaka 22 ikulu na hakuna atakaemfikia,ila huyu miaka mitano tu akae pembeni!!!
 
Back
Top Bottom