President of China
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 31,548
- 89,516
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa Sh 50 milioni kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Maria Mtakatifu Mwana wa Mungu, Kabwigwa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
Mbali na Rais kutoa kiasi hicho, fedha zilizochangishwa kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa hilo ni Sh250.2 milioni.
Akitangaza matokeo ya harambee hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC), Masanja Kadogoda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, amesema kwa mapenzi mema, Rais Samia amechangia ujenzi huo baada ya kuombwa kufanya hivyo na Askofu wa Jimbo la Kigoma, Mhashamu Askofu Joseph Mlola.
Kadogosa amesema kuwa katika harambee hiyo Rais Samia pia aliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kampuni ya GSM, Gharib Mohamed huku wapenzi wa timu za Simba na Yanga waumini wa kanisa hilo wakichangia Sh890,000 ambapo wapenzi wa Yanga walichangia Sh528,000 na wa Simba Sh362,000.
Awali Askofu wa Jimbo Katoliki la Kigoma, Mhashamu Joseph Mlola alimshukuru Rais Samia kwa mchango huo na kuongeza kuwa ni kiongozi anayejali watu kwa hali yeyote, sambamba na kuwashukuru wote waliofanikisha harambee hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akisoma taarifa ya ujenzi wa kanisa hilo Katibu wa Kamati ya Ujenzi, Joseph Kahene alisema kuwa lilianzishwa mwaka 1933 ambapo hata hivyo hakukuwa na idadi kubwa ya waumini kama sasa.
Amesema kwa sasa kanisa hilo lina waumini 14,000 limekuwa dogo na lililozeeka hivyo kunahitajika ujenzi wa kanisa jipya.
Kahene amesema kuwa ujenzi wa kanisa jipya unahitaji Sh4 bilioni ili kulikamilisha likiwa na uwezo wa kuchukua waumini 1,800 kwa wakati mmoja, hivyo michango kutoka kwa watu mbalimbali bado inahitajika.