Mh. Rais nakuomba umpe nafasi na ubavu wako, utashangaa!

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,618
12,283
Mh Rais wangu ninaye kupenda nakukuaminia yani kwangu wimbo ni Magufuli. Kiukweli kabisa nakupongeza sana kwa speed unaenda nayo kiukweli taifa limesimama.

Hata hivyo mkuu kwa sasa hata baada ya mapishi mazuri ya kiuongozi chakula kimekosa kiungo fulani amazing ili watu wafurahi na kiungo hicho sio kingine ila ni first Lady. Wakati wewe ni rais wa Jamhuri ya watanzania yeye ni mama wa Jamhuri ya Tanzania kwa wamama na vijana na watoto.

Kiukweli kabisa huyu mama haonekani sana, jambo ambalo kisiasa sio zuri. Mimi kama mshauri tu ningeomba sana team ya ikulu iandae mikakati ya kufanya huyu mama awe anaonekana na kuleta furaha kwa watanzania. Hata kama kumuhoji yupo jikoni akikupikia unajua ingeleta motisha sana kwa watu na wakina mama maana hilo lingebeba slogan ya hapa kazi tu.

Pia kisiasa ili uwazidi watani wako ni muhimu sana huyu mama kuwa mbele kwenye mambo ya kijamii na kwa hakika mkuu wangu utashangaa vile 2020 utakuwa juu.

Siri:

Zipo propaganda zinafanyika kwa wanawake pitia huyu mama sasa usipompa nafasi utatuweka kwenye mtego mkubwa sana kama wanachama na taifa kwa ujumla hasa ukizingatia taifa limekukubali bara na visiwani.

Mungu akubariki wewe na familia yako. Amen.
 
Eti wamuhoji yupo jikoni wewe itakusaidia nini kwenye maendeleo ya familia yako
 
Mwacheni mama wa watu,
mnataka aanze yale ngos ambazo hazina kichwa wala miguu;
 
Back
Top Bottom