Mh Rais kuna taarifa zinaenea kuwa wafanyabiashara wakubwa kwa kushirikiana na viongozi wa serikali yako wameungana kukushauri ukubali wafanyabiashara waingize mchele ya Thailand bila kulipa kodi, kwa kisingizio kuwa nchi ina njaa ya Mchele. Mh Rais hili wazo naomba usilikubali kwani ndani ya washauri wako wamepanga kula commission ya udalali ya kuruhusu mchele kuingizwa nchini bila kulipa kodi.
Ukweli ni kwamba Tanzania tuna upungufu wa Mahindi na si mchele hivyo usidanganyike na kutoa maamuzi ya kunufaisha watu wachache, kwa raha zao halafu ukawaumiza wakulima wadogo wa Tanzania.
Wakati wafanyabiashara hao wakijigamba kuwa wameleta andiko serikalini ili waingize mchele wa Thailand bila ushuru kwa kisingizo cha kuwa mchele umepanda, hao hao hawakuwasaidia wakulima kupata soko la nyanya mwezi wa tano, wakati nyanya nyingi zilizalishwa na kukoswa soko. Waliishia kukudhihaki kuwa unawambia wafanye kazi wakati Masoko hakuna. Ni wakulima hao hao waliopoteza kipato kwenye nyanya ndo wamevuna mpunga vizuri mwaka huu na sasa wanauza kwa bei bora kiasi.
Mh Rais naomba sana kwa hili ujali watanzania wako na uachane na watu kuleta mchele wa Thailand, kwani nchi haijafikia hali ya upungufu unaotajwa. Ukiruhusu watu kuingiza mchele bila kodi stahiki, watu wengi na hasa vijana hawatawekeza kwenye kilimo kwani wataona hakuna faida.
Ni hayo tu mh Rais la kutaka usikubali mchele uingizwe nchini bila ushuru kwani utaua wakulima wa mpunga Tanzania.