Mh. Rais mfikirie Antony Diallo kwenye Baraza lako la Mawaziri

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
5,210
4,172
Nimapendekezo yangu kwa Bwana Mkubwa, Amfikirie Huyu Ndugu Diallo kwenye Baraza lake la Mawaziri ili Awezekutoa Mchango wake kwa Taifa hili.

Wote mliopata fursa ya kumtazama ndugu huyu leo kwenye kipindi cha tuongee Asubui Show. Kinachorushwa na Kituo cha Startv.

Kilichokuwa na mada inayohusu kuanguka kwa thamani ya zao la Pamba.

Mimi kwakweli nimemkubali sana misimamo yake na uwezo wake wa kujenga hoja pamoja na mawazo aliyotoa.

Hivyo basi ni vyema ikimpendeza Ndugu Rais Kumchukua Mtu Huyu ili Atoe Mchango wake kwa Taifa.
 
Keshakuwa waziri kipindi cha mkapa tena kwenye wizara nyeti ya viwanda na biashara. Mchango alotoa umetosha kama mtendaji, kwa sasa ushauri apeleke kwa watendaji
huwezi kuwa kiongozi Mzuri kama ukupata fursa ya kukaa benchi na kuona Makosa.

Hivyo unapopata fursa unakuwa na vitu vizuri ulivyoona nje na kuvitendea kazi Mkuu.
 
Kweli, anaweza kuisaidia serikali hii. Siyo vibaya katika nia yetu ya kuwa na viwanda, tukafikiria watanzania wenzetu walio katika masuala ya viwanda kwa uzoefu wao.
 
Nimapendekezo yangu kwa Bwana Mkubwa, Amfikirie Huyu Ndugu Diallo kwenye Baraza lake la Mawaziri ili Awezekutoa Mchango wake kwa Taifa hili.

Wote mliopata fursa ya kumtazama ndugu huyu leo kwenye kipindi cha tuongee Asubui Show. Kinachorushwa na Kituo cha Startv.

Kilichokuwa na mada inayohusu kuanguka kwa thamani ya zao la Pamba.

Mimi kwakweli nimemkubali sana misimamo yake na uwezo wake wa kujenga hoja pamoja na mawazo aliyotoa.

Hivyo basi ni vyema ikimpendeza Ndugu Rais Kumchukua Mtu Huyu ili Atoe Mchango wake kwa Taifa.
Ama kweli hii nchi kuja kufika hata robo ya south afrika ni ndoto kama vyeo watu wanapewa kwa kupoozana machungu kweli watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Kuongea ni tofauti na kutenda, maana alishawahi kuwa mbunge akatemwa. Halafu huyu si ndio alimsaidia Magu kwenye kampeni akasema hadharani hatomsahau? Sasa mbona Mzilankende na Makonda wanashinda Clouds Tv/Redio na sio StarTv?
 
Afikiriwe vipi? Unamaanisha ateuliwe kama Mbunge kisha baadae awe Waziri?

Kama ni hivyo basi jambo hilo haliwezekani. Tayari wabunge watano jinsia me washatimia kwenye nafasi za uteuzi Viti maalum.

Huyo abaki kuwa mrusha matangazo tu ya Mkulu.
 
Mbona ashawahi kuwa waziri wa maliasili na utalii misitu na wanyama wetu almanusura vipukutike?,.akawa waziri wa maji lkn hata Mwanza maji hayakutosheleza ilihali ziwa Victoria lipo Mza ,ashakuwa waziri wa kilimo hakukuwa na jipya. Cha maana alichofanya ni kampuni zake kuajili watz kibao na kujitoa kwa media zake kuisaidia ccm.

Namshauri mkulu amwezeshe kuimarisha biashara zake ili aajili watanzania wengi zaidi.
 
Huyu jamaa alishakula maisha sana alipokua kwy nyadhifa enzi za BWM atulie na biashara sake na alike kodi!
 
Tuko wengi sana mitaani hatuko kwenye baraza la mawaziri tunatoa michango mikubwa sana kwenye Taifa kuzidi hata wale ambao wako kwenye baraza la mawaziri,na wengi wao wameteuliwa kisiasa na kiundugu,na siyo kwamba wako kwenye baraza hilo kwa maslahi ya Taifa,bali ni kwa maslahi yao wenyewe na familia zao,pamoja na kuzipenda saluti.
 
Ni kweli Mkapa na Kikwete waliibua Mawaziri Majembe sana.

Tatizo lilikua huko kwenye halmashauri na watendaji wengine huko wizarani walikosa uzalendo.
Mfano wa Mawaziri majembe walioibuliwa Kipindi cha Mkapa ni pamoja na,
JPM .
Lowassa.
Kikwete.
Dialo.
Masilingi.
Mwandosya.
Husein Mwinyi.
Na wengine wengi. Aliwaita askari wa Miavuli.

Awamu ya Kikwete pia aliibua mawaziri na watendaji wengine mahiri ,mfano :

Mwigulu Nchemba.
Angela Kairuki.
Benard Membe.
Harison Mwakyembe.
Paul Makonda.
Anne Kilango.
Ummy Mwalimu.
Hendry Mwanry.
Prof. Makame
Mbarawa.

Lukuvi.
Na wengine wengi.

Kwa hiyo kama awamu ya Tano haina sehemu ya kupata majembe ni bora ikayatumia hayo majembe ya zamani chini ya usimamizi imara wa JPM.

Majembe ya zamani pia yanawezekana kutumiwa kwa ushauri hasa kwenye masuala ya uchumi.
Kwa hawa waliopo wamepwaya sana kwenye sekta ya kukuza uchumi. Wamekua wanasiasa sana.
 
Back
Top Bottom