Mh. Rais Kikwete; Saga la TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Rais Kikwete; Saga la TANESCO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Jul 31, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Mh. Rais, inajulikana kuwa ni wewe ndiye uliyewateuwa Waheshimiwa wafuatao:- Maswi, Mhando, Mboma, Muhongo, Simbachamwene na Masele. Katika kundi hilo wapo walioidhalilisha Serikali yako kwa kushindwa kazi na kujiingiza katika ubadhilifu dhidi ya TANESCO na Taifa kwa ujumla na wapo wenzao waliotekeleza wajibu wao vyema (wala hawahitaji kusifiwa.). Mh. Rais ukiwa Mkuu wa Serikali yetu, bila kuuma maneno, ungana na Spika wa Bunge na hata Kambi ya Upinzani ktk haya:

  [/FONT]
  [FONT=&quot]i. [/FONT][FONT=&quot]Futa uteuzi wako wa MD. Mhando na umpe kazi Mzalendo-Msomi mwingine (wapo wengi) badala yake. Pia futa uteuzi wako wa Mwenyekiti Ret. General Mboma na kuagiza Waziri aunde upya Bodi hiyo (system aliyoianzisha Muhongo ya watu kutuma maombi kwa ushindani inaheshimika na iwe mfano kwa Bodi zote tupate Watu waadilifu na wenye uwezo si kuwazawadia Wastaafu![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]ii. [/FONT][FONT=&quot]Agiza / Watake Takukuru, CAG na Mwanasheriaa Mkuu wafanye uchunguzi wa kina (wape time framework) kugundua wahusika wengine katika jinai ( rushwa na wizi) wafikishwe mbele ya sheria haraka sana bila kujali ni akina nani. Na wafuatilie kesi zote ambazo zimechukuwa muda mrefu bila kuisha ili zitolewe hukumu.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]iii. [/FONT][FONT=&quot]Kemea kwa nguvu zote vitendo vilivyofanyika vya baadhi ya Wabunge kupokea rushwa (hii si fununu tena sasa) katika harakati za kutaka kumtetea Mhando aliyeshindwa kutekeleza majukumu yake kama ulivyomkabidhi na mbaya zaidi kuwatukana na kutaka kuwadhohofisha Watendaji waliowajibika Wizarani. Wakumbushe maadili ya umma baadhi ya Wabunge na Mawaziri kutokuwa na migongano ya kimaslahi katika kufanya biashara na mashirika wanayoyasimamia na pia hata kwa Watunga sheria ambao tena wanakuwa watetezi mahakamani kupitia kampuni zao za Uwakili mf. Mkono & Mkono Advocates katika kesi na IPTL n.k [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]iv. [/FONT][FONT=&quot](Kama threat iliyotolewa Bungeni na hapa JF ni credible) kuhusu mpango wa kuhujumu uzalishaji au ugavi wa umeme nchini, toa onyo la Amir Jeshi Mkuu kwa mtu yeyote au kikundi cha watu wanaotishia watu maisha yao, mali za serikali na ustawi wetu kwa kuwaagiza makamanda walioko kazini (sio retired) kuwashughulikia watu hao maana Serikali yako haiwezi kutishwa na kinyago tulichokichonga mwenyewe! [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]v. [/FONT][FONT=&quot]Elekeza Makatibu wakuu wa vyama vya Siasa waitishe vikao vyao husika kuwajadili na kuwaadhibu Wabunge wote waliohusika katika kupokea, kuomba au kutoa rushwa. Hivyo ni matumaini yetu kuwa mara moja baada ya Bunge; nawe kama Mwenyekiti wa CCM (T) utaendesha kikao chako kuwaadhibu Wabunge wetu bila huruma ili kurejesha hadhi ya CCM kama chama Tawala. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ni katika kuchukua hatua stahiki, madhubuti na mapema, sisi Wabunge na Wananchi kwa ujumla tutakuunga mkono katika vita dhidi ya rushwa, vinginevyo tutakuwa tunajichora kama vyama vya siasa, kama Bunge na kama Serikali, kuwa vyombo visivyo makini na visivyoaminika katika jamii na hivyo kuhalalisha wengine kuendelea kutubeza kuwa vikundi vya sanaa za maonyesho na hadi kufikia kukutuhumu wewe kuhusika katika hili sakata lote na hatima yake Wananchi watakataa huku wakiuma na meno kuweka alama (tick) husika katika visanduku vya mgombea yeyote wa CCM pindi muda ukiwadia.[/FONT]
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Itakuwa ngumu kwa vile na yeye ni mmoja wapo!!.
   
 3. b

  beyanga Senior Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​kikwete ana maslahi na mambo ya tanesco siku ya siku ataumbuka tu
   
Loading...